Jukwaa la wapenzi wa mambo ya muziki wa Tanzania-

Breaking

Tuesday, April 20, 2010

Those were the days


Those were the days my friend,
We thought they would never end,
We would sing and dance for ever and a day.
We'd live the life we chose,
We'd fight and never loose ,
Cause we were young O yes we were young. Katika picha.. Patrick Balisidya na Salim Willis enzi za Afro 70

20 comments:

Anonymous said...

Afrosa aisee ilikuwa ni bendi komesha hapa TZ. Nilisikitika sana kusikia eti ni serikali ndiyo iliwafanya walostike baada ya kurubuniwa vyombo vyao. Na serikali hiyo hiyo ilikuwa inataka wanamuziki waamasishe umma kwa kuimba nyimbo za kimapinduzi, kisha serikali hiyo hiyo inaiita wanamuziki wahuni. Ivi uhuni ni asili ama hurka ya mtu? Pia serikali baada ya kuwaita wanamuziki wa TZ wahuni, serikali hiyo hiyo ndiyo iliyokodi ndege kwenda Kinshasa kumchukua muhuni wa kimataifa aitwaye Tabu Ley aje kuwaimbia wabunge kule Dodoma katika campaign za CCM. Leo hii tukae chini na tujiulize, kati ya mawaziri, wabunge, na viongozi serikalini nani ni muhuni zaidi ya mwanamuziki? Utakuta kwa asili mia moja watu wa serikali ndiyo wanaongoza kwa ufuska hapa TZ ila kwa kuwa hawataki kushindana na watu wa chini ndiyo maana wanawapakazia wanamuziki, kisha wanataka kusifiwa bila sababu. Yaani TZ kweli imeoza.

Patrick Tsere said...

Anonymous hayo uliyoyasema sikubaliani nayo. Siyo sera ya serikali kuita muziki ni uhuni la sivyo isingekuwepo idara ya utamaduni wala wizara inayoshughulikia utamaduni. Naomba usiwe na hasira ndugu yangu. Usichanganye maoni na facts. Mimi nikisema muziki ni uhuni hayo ni maoni yangu na wala siyo ukweli. Please be objective in your arguments.

Pia muziki ungekuwa ni uhuni basi hata makanisani usingeruhusiwa wala wakati wa mikutano iwe ya kisiasa au ya elimu nina hakika muziki ungepigwa marufuku. Ni nchi ya Somali tu ndio serikali iliyopo inaona muziki ni uhuni.

Mimi ninaamini muziki ulianzia mbinguni. Hata ukisoma misahafu hususan biblia inasema Lucifer kabla ya kumkosea Mungu alikuwa msimamizi wa idara ya Muziki. Fanya utafiti mtoto akiwa bado mchanga kabisa anapolia ukimwimbia tu anakuwa on full alert why? Because of music. Kwa hiyo Muziki siyo uhuni hata kidogo. Muziki ni karama na kipaji kutoka kwa Muumba Subhana wa Taala.

BLACKMANNEN said...

Ndugu yangu "Anonymous",

Usiingie hapa na ushabiki wa kichama. Afro 70 iliingizwa kwenye mkenge na Viongozi wa serikali miaka ya 1975. CCM wakati huo ilikuwa bado kuzaliwa.

Viongozi wa serikali wa Tanzania wakati huo kabla ya mwaka 1977, ilikuwa ni pamoja na wa vyama vya upinzani.

Tabu Ley alikuja Tanzania mwaka 1974. Je, wakati huo kulikuwa na kampeni za CCM ipi?

Wewe "Anon", kaa chini mwenyewe ujiulize, kati ya Viongozi wa serikali ya wakati huo na wewe mwenyewe sasa hivi, mhuni ni nani!

This Is Black=Blackmannen

Anonymous said...

HONGERA BW.KITIME KWA KUTUPATIA KIJIWE HIKI. BADO SWALI LANGU HUJANIJIBU...NI NANI MMILIKI WA NYIMBO ZA BENDI ZILIZOREKODIWA PALE RTD?

Anonymous said...

Patrick I will always remember not only your art and creativity but also your humble behaviour . RIP.

John Mwakitime said...

Kimsingi nyimbo zilizorekodiwa pale ni mali ya watunzi. Lakini kuna matatizo ya kukosa records sahihi za nani ana sifa ya kuitwa mtunzi. Hivyo ikiwa unataka kutumia nyimbo ni vizuri uonane japo na aliyetajwa kuwa mtunzi na ndie mwenye haki. Radio wanauza kanda za nyimbo hizo lakini thats makosa , nimeshajaribu kuutarifu uongozi unaonekana hauoni tatizo, lakini siku mtu ataenda kudai chake kupitia mahakama that will be the day

Anonymous said...

Ninataka kuandika maoni lakini sijui kwa nini nakuwa mzito?

Anonymous said...

Mwakitime,kuna swala umezungumza hapo chini,kuhusu nani mmiriki wa wimbo husika.na ukazunhumzia juhudi zako kuhusu jinsi nyimbo hizi zinavyo uzwa ama kutumika na chombo husika cha serikari.mimi binafsi nafikiri kwa miziki yote iliyo pigwa na kurekodiwa na iliyokuwa RTD zamani kuna ulazima wa kuangalia upya nini kifanyike ili kila mtu afaidike na muziki huo.ukisema sasa hivi iliyokuwa RTD zamani haina hakina hizo nyimbo mimi naona nikosa,kwa sababu wao ndiyo walio zirekodi nakuzi promoti bila gharama yoyote kutoka kwabendi husika,nahatimaye leo hii tunazisifia na kuzitukuza.vilevile nawao wanamuzik kwa upande wao wamjitahidi kutunga nakukubali zipigwe iliwanachi waburudike.wakati fulani huwa napata wasiwasi sana kuhusu jambo hili kuhusu miziki yote iliyo rekodiwa na RTD nini kifanyike ili haki itendeke.kwani hata wanamuziki wenyewe hawana uhakika kama baadhi ya nyimbo ni halala kwa miongoni mwao kudai umiliki.nahii ni kutokana namfumo mzima wajinsi bendi zetu zilikuwa zikiendeshwa. waweza kufikiri zuewena ya marijani ilitungwa na marijani kumbe lakini ukweli ukaambiwa siyeye,nakwa wakati ule kiongozi wa band alishaika hatamusana,na nyimbo zilikuwa niza band siyo mtubinafsi.hivyo kama kutakuwa na malipo mimi aona iwe kwa wahusika wote kwa wakati ule kila mtu alikuwa na mchango.nihayo tu mawazo yangu,ila swala hili ni budi liangaliwe kwa undani zaidi,nani au tufanyeje kuhusu jasho hili la zamani.mdau uk

Anonymous said...

Patrick Tsere, thanks for your thoughts. I am the one who wrote the above comments pale jana. I wrote hiyo habari because I know I am right, kwa sababu Mze wangu alikuwa serikalini na kwetu viongozi wengi tu walikuwa wanakuja pale nyumbani kumuona swahiba yao Baba yetu. Mara nyingi wakiwa pale utawasikia hawa wanamuziki wa Tanzania ni wahuni tu hawana kitu. Hapo hapo wanamsikiliza tabu Ley ama Franco kwenye kanda ambazo Baba alikuwa nazo. Sawa huenda ni maoni ya watu binafsi lakini hii kitu/imani ya kusema wanamuziki ni wahuni viongozi wa serikali wakati ule na sasa bado wanayo kichwani.

Blackemenn, naona wewe ni kichwa cha panzi ama labda huna la kuongea. Humu mimi nimezungumzia serikali ya C.C.M. ilkodi ndege ya ATC kwenda kumchukua muhuni wa kimataifa in Tabu Ley aje kutumbuiza wabunge kule dodoma katika kampeni zao za uchaguzi mwaka 1985. Niambie, TANU ilikuwa ina exist at that time? Nimesema vile because I have all the facts sibishani kwa ujinga. Uliza baba yako ama viongozi wa serikali Tabu Ley alikuja lini nchini na Mbilia bel? Acha upumbavu usio na akili. Ndio nyie watu wa Bongo fleva unabisha kitu usichokijuwa.

Anonymous said...

ASANTE SANA BW.KITIME KWA JIBU LAKO AMBALO LIMENIPA MWANGA KUHUSU SUALA HILI LA MILIKI YA NYIMBO ZILIZOREKODIWA RTD. NINAOMBA UFAFANUZI ZAIDI...NINI NAFASI YA BENDI AU MMILIKI WA BENDI JUU YA UMILIKI WA TUNZI ZA BENDI HUSIKA?

John Mwakitime said...

Taraditionaly mwanamuziki huenda kuomba kujiunga na bendi na atasema fani zake zote , utunzi inakuwa by the way, hapo ndo mistake ya kwanza inaanza. Utunzii ndio kila kitu. Hivyo akitunga nyimbo hata yeye haimjii kuwa ni shareholder katika ule muziki zaidi ya sifa. Pili, owner wa bendi huwa analipa mishahara ya washiriki wote na hata vombo ni vyake hivyo huhitajika kuweko na mkataba juu ya nani atakuwa mwenye hakimiliki ya tungo zitakazopatikana, kwa sheria ya Tanzania kama hakuna mkataba , tungo ni mali ya mwenye bendi!!!! Radio Tanzania hawakufanya promotion bure kama alivyosema mchangiaji mmoja, walitumia nyimbo katika vipindi na walilipwa na sponsors wa vipindi, wanamuziki hawakuambulia chochote katika mgao huo, jambo ambalo linaendelea mpaka leo.

John Mwakitime said...

Naomba turudi kwemye lugha ya wapenzi wa muziki please. Kupingana mawazo ndo utamu wa sanaa

Anonymous said...

BW.KITIME,NASHUKURU KWA UFAFANUZI HUO JUU YA UMILIKI WA NYIMBO. NAOMBA USINICHOKE...KWANI NINA MENGI AMBAYO NINGEPENDA KUYAFAHAMU KUHUSU MUZIKI, NA HASA HUO WA ENZI HIZO. MIMI NILIANZA KUHUDHURIA MADANSI MIAKA YA MWISHO YA SABINI,AMBAPO NILIKUTA VYOMBO AINA YA RANGER VIMESHAMILI NA VILIKUWA VINATIKISA HASA...IMAGINE SHOWS KWENYE UWANJA WA MPIRA LAKINI VYOMBO VINASIKIKA KISAWASAWA!!SWALI 1. HIVI VILIKUWA VYA UWEZO GANI YAANI AMPERAGE(WATTS) KWA HEAD (AMP) NA CABINET? NA JE VYOMBO KAMA ORANGE, HATKE, PEAVEY VYAWEZA KUTOA MAMBO MAZITO KAMA YA RANGER FBT? 2. NINI TOFAUTI YA UTENGENEZAJI(DESIGN) KATI YA GITAA LA SOLO NA RITHYM? KWANI NIMEZUNGUKIA AINA MBALI MBALI ZA MAGITAA NINACHOONA NI GUITAR AND BASS!! 3. NINI TOFAUTI YA GUITAR LA GIBSON (LES PAUL) NA FENDER (STRATOCASTER) KAMA YANAVYOTUMIKA KWENYE AINA YETU YA MUZIKI? 4. NA ULE MLIO WA GITAA LA DAR JAZZ 'WOW...WOW...WOW' NI NINI HASA, GITAA LENYEWE AU AMP? SAMAHANI NAKUCHOSHA,LAKINI UMENIAMSHA!

John Mwakitime said...

Ranger zilikuwa na watt 250, ila PA za ranger wakati huo zilikuwa Watts 1000. Unajua kuna wakati enzi za social evenings kwenye mashule wanafunzi wa shule 2 au 3 hivyo kiasi cha watu 600 waliweza kusikia na kucheza dansi kwa kutumia Phillips Changer yenye watts zisizozidi 30!!!!. Siku hizi party ya darasa inakodisha mzigo wa watts 3000, nadhani ni swala la kuongelea masikio yetu yameharibika? Hakuna tofauti ya design ya gita la solo na rythm ila ni jinsi ya upigaji na ton ambayo huwa nzito kidogo kuliko solo.Hizo ni design za magitaa na zinatumika kama nyingine katika muziki hapa, tatizo ni upatikanaji, na magitaa ambayo ni gharama kutokana na ubora wake. Sauti katika gitaa la Michael Enoch lilitokana na effects pedal ambayo huitwa Wah wah au mara nyingine 'cry baby'

Anonymous said...

SWADAKTA MWAKITIME, UMENIMALIZA! ASANTE SANA. ILA NITARUDI BAADAE!

Anonymous said...

Huu mjadala iwapo wanamuziki ni wahuni au la unanikumbusha jinsi chama na serikali enzi hizo vilivyokuwa vinadhibiti na hata kuua ubunifu wa wanamuziki. Nakumbuka kibao cha ‘Bomoa Tutajenga Kesho’ cha Orchestra Mambo Bado ya Tshimanga Assosa kilivyopigwa marufuku kwa sababu za kipuuzi mwaka 1983. Haya ni maneno tu ya kimuziki ambayo Assosa aliyaazima kutoka kibao cha Tabu Ley cha ‘Ibeba’ chenye maneno ‘Ibeba lelo tokobongisa lobi’. Ni ujinga ulioje kudai kwamba Assosa alikuwa akihamasisha watu kubomoa nchi. Wapenzi wa muziki pia watakumbuka jinsi wataalam wa Redio Tanzania kwa shinikizo la wakubwa walivyofuta kionjo cha ‘hii kali’ kilichotamkwa na Maneti (RIP) katika kibao cha ‘Wifi Zangu’ cha Vijana Jazz. Hivi maneno haya yana ubaya gani? Marehemu Mbaraka Mwinshehe alisuswa na chama na serikali kwa sababu tu alifia Kenya alikoenda kusaka maslahi zaidi. Tanzania wakati huo ilikuwa na uhasama na Kenya kiasi cha kufunga mipaka yake na nchi hiyo. Lazima tukubali kwamba watawala enzi hizo walikuwa hawawatakii mema wanamuziki wetu.

John Mwakitime said...

Bahati nzuri mi ni mmoja wa waimbaji wa kibao Bomoa Tutajenga Kesho. Inawezekan ni co incidence maneno yakafanana na wimbo wa TabuLey,lakini kibao hiki kilitungwa kutokana na tukio nililoshiriki. Tulikuwa tunafanya mazoezi kwenye ukumbi wa Lango la Chuma kule Mabibo, ukumbi ulikuwa umekarabatiwa vizuri,na uzinduzi wa ukumbi ulikuwa uende sambamba na uzinduzi wa bendi Orchestra Mambo Bado, lakini kwenye gate kubwa palikuwa na ufa na katika kutaniana na mwenye ukumbi wanamuziki wakamwambia siku ya uzinduzi wa bendi watu watabomoa geti, yeye akajibu 'bomoa tutajenga kesho', wazo la wimbo likazaliwa.

Anonymous said...

wadau naomba tutoe maoni kwa mada husika hapa tunatakiwa tumzungumze Patric na Afro 70 yake tusitoke nje na kujadili mengine nina imani Kitime atatufikisha kila kona.
Big up kitime.

Anonymous said...

Sasa angalia huo ujinga wa chama. Nyie mlikuwa na mawazo tofauti kabisa kuita ule wimbo bomoa tutajenga kesho kutokana n tukio lile. Baada ya serikali kuwauliza wahusika walikuwa na maana gani kusema vile, wao wakatumia ubabe. Tanzania bwana, yaani wakati mwingine mtu unashikwa na hasira na hawa viongozi wetu. Ila mambo bado mlikuwa wakali bwana, yaani pale mlipoanza, mliingia kwa mbinde sana, nakumbuka sana vibao vyenu imara.

Anonymous said...

Nawaunga mkono Patrick Tsere na Blackmannen. (1)Mimi nilikuwa katika fani za sanaa na muziki (japo si "professional"). Nakumbuka tangu miaka ya 1970's, pale Tancot House kulikuwa na Idara ya Sanaa -including music chini ya Wizara ya Utamaduni (enzi za Maj. Gen Sarakikya). (2)Hali kadhalika, utafiti unaonyesha kuwa Baraza la Muziki la Taifa liliundwa na serikali, kwa sheria ya Bunge, ili "kukuza fani za muziki asilia na wa kisasa". (3)1985 hakukuwa na vyama vingi TZ; uchaguzi wa kwanza wa kurejeshwa tena vyama vingi ulifanyika 1995.
(4)Sijawahi asilani kusikia tamko lolote rasmi la serikali TZ likiwaita wanamuziki "wahuni". (5) Kurudi kwenye mada yetu, John M, ahsante sana kwa kutupeleka sisi "wazee" down the memory lane...oh, yes, those were the days my friend..... Mdau wa sanaa.

Adbox