Jukwaa la wapenzi wa mambo ya muziki wa Tanzania-

Breaking

Sunday, April 18, 2010

Hunaaaaaaa mwana hunaaaaaa

Baada ya Marijan na Safari Trippers kuimba kibao Hanifa, na katika chorus kuimba neno 'huna'. Liligeuka kuwa neno ambalo lilitumika kama vile leo neno 'kufulia' linavyotumika. Ungemsikia binti akimwambia mwanaume 'Hunaaa" na liliweza kuleta ngumi neno hilo. Haya picha ya hali wakati huo kwa wasomaji wa Kiingereza
.

8 comments:

Anonymous said...

Mkuu,

Hii dose unayotupa siyo mbili mbili kutwa mara tatu ni mia mia kutwa mara moja, ukiimaliza kuinywa unabaki na kiwewe!

Sina la kusema nimebaki nacheka cheka tu! Haki ya Mungu. "Mbifile kweli kweli! Tuonana pambele tutadua!"

Asante sana tena mno.

Anonymous said...

Bw. Kitime ahsante sana kwa utoaji wako wa habari. Hapa nabaki najiuliza kwa nini vijana wa sasa wasiwe kama wewe? Maana unaleta habari zinazotulenga sie watanzania na sio wamarekani weusi ama watu tu wa nje na wasio na lolote kwetu. Jamani tutunze heshima yetu, tuachane na hii tabia ya kutaka kujua vitu vya watu wa nje wakati nasi tuna historia kubwa tu tena nzuri zaidi. Ahasante sana Bw. Kitime...Michuzi unaona haya? Tuletee nawe post kama hizi.

Anonymous said...

Mkuu,

Samahani naomba kuuliza Marehemu Doser alifia na kuzikwa Mwanza?

Anonymous said...

hizi dozi kaka unatumaliza, basi haya!

John Mwakitime said...

Dozer alifia nyumbani kwake Dar na alizikwa makaburi ya Kisutu

Anonymous said...

Mkuu,

Asante sana kwa majibu.

Mwaka 1995 nilikuwa nimepania sana kuandika makala kuhusu Marehemu Doser. Nilikuwa nimeshachagua na gazeti la kuitoa makala hiyo. Ilikuwa niitoe kwenye gazeti la Uhuru la Jumamosi ukurasa wa mwisho kwa ndani. Nilikuwa nimeshapata kichwa cha habari cha makala yenyewe ambayo nilitaka kuiita Kumomonyoka Kwa Jabali -Alipotokea na Alipo Leo Marijani Rajabu.

Haikuwa kama nilivyokuwa natarajia. Miezi miwili kabla ya kufunga safari kwenda kutimiza azma yangu jamaa yangu mmoja akanitaarifu kwamba Jabali limemomonyoka kabisa na halipo tena.

Shujaa mwingine akawa ameondoka bila kutangazwa kwenye taarifa ya habari au kuwekwa kwenye ukurasa wa mbele wa magazeti ya Chama na Serikali. Bila siku saba za maomboleza ya kitaifa, bendera nusu mlingoti, gwaride, saluti wala mizinga ishirini na moja. Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema Amrehemu Marehemu Doser kwa Amani. Ameni.

Anonymous said...


...Brother John Hapa ndipo muziki wetu ulipokuwa umefika! Nakumbuka hii article ilitoka kwenye gazeti la burudani la TRUST la Kenya mwaka 1975 nami kuisoma pale Musoma Alliance wakati nikisoma Form One na kiranja wangu wa Bweni akiwa Mwamoyo Hamza aliye VOA sasa. Those were the dayz.

Anonymous said...


...Brother John Hapa ndipo muziki wetu ulipokuwa umefika! Nakumbuka hii article ilitoka kwenye gazeti la burudani la TRUST la Kenya mwaka 1975 nami kuisoma pale Musoma Alliance wakati nikisoma Form One na kiranja wangu wa Bweni akiwa Mwamoyo Hamza aliye VOA sasa. Those were the dayz.

Adbox