Flaming Stars


Familia ya akina Sabuni ilikuwa maarufu sana katika makundi ya vijana wapenzi wa muziki wa Buggy , John , Cuthbert, Raphael wote walikuwa wanamuziki, na kundi la Flaming Stars lilikuwa ni la akina Sabuni. Katika picha hii ya Flaming Stars unawatambua wangapi.?

Comments

Patrick Tsere said…
John hapo ninawatambua wafuatao:Cuthbert Sabuni, Michael Mhuto, Peter Kondowe (PEKO)na John Sabuni. Ninakumbuka baadhi ya nyimbo zao kama vile 'Mpenzi Maria sisahaux2 Hata nyota nazo nayo pia mbalamwezi..Mariaaa. Usiku huu mi nalia nikikumbuka oh Maria ohooo Maria kitu kama hicho.
waterdeenullo said…
Nafurahi sana kupata huo uhondo wa kipindi hichoo. nafurahi sana bwana kitime
Anonymous said…
Flamming Stars waliporudi kutoka nchi za nje ukimtoa Michael Mhuto ambaye alibakia nyumbani na band ya "The Commets" pamoja na mwimbaji maarufu wa kike Stella Amri ilikuwa band yetu sisi vijana wakati huo tukiitwa "ma-bitoz" tuliupaka rangi"rainbow" mji wa Dar es salaam.
Nakumbuka Flamming Stars walirudi kwa vishindo na katika "show" ya kwanza tokea warudi walitusisimua na kile kibao cha kuigiza cha The Beatles "Dont Let me Down" wakati ule kilikuwa katika "Top Ten" kwa sisi ma-bitoz.
Kama bado wapo ningependa kujuwa wapo wapi?

Mickey Jones
Denmark
Anonymous said…
Nakumbuka 1969, nilipokuwa form iv nilikwenda kwenye boogie moja ya Rifters either Splendid (sasa kuna jengo la extelecoms) au New Palace (baadaye Mbowe hotel). Wakati wa mapumziko Flaming Stars walipewa "lift" wakapiga nyimbo chache including ya Beatles. Nalini wimbo ambao naukumbuka mpaka leo (baada ya miaka 40) ni "amen" wa otis reding uliowafany watu wawe mesmesized!!!Eddy.

Popular posts from this blog

Marijani Rajabu

SITI BINTI SAAD

Western Jazz Band

Sikujua kama utabadilika - Simba wa Nyika

Mlimani Park Orchestra

Super Kamanyola ya Mwanza