Jukwaa la wapenzi wa mambo ya muziki wa Tanzania-

Breaking

Wednesday, February 3, 2010Tancut Almasi Orchestra, bendi iliyokuwa namakazi yake Iringa kuanzia 1987, ilikuwa chini ya Kiwanda cha kuchonga almasi cha hapo Iringa, Diamond Cutting Company. Bahati mbaya wengi ni marehemu. Kutoka kushoto Buhero Bakari inasemekana ni mganga wa dawa za asili kwa sasa,marehemu Kyanga Songa, Kasaloo Kyanga yupo Dar anaendelea na muziki,Kabeya Badu, yuko na King Kiki na wazee sugu, Marehemu Kalala Mbwebwe, Abdul Mngatwa, yuko Iringa ameacha muziki, Akuliake Salehe aka King Maluu yupo Dar anaendelea na muziki

5 comments:

Moses Gasana said...

Hapo Shaban Yohana "Wanted" alikuwa wapi kaka Kitime? alikuwa ameshajiunga na bendi ya Tancut? pacha mmoja umesema yuko Dar je anafanya nini sasa? Shaban Wanted bado yuko Botswana? kaka siwezi kukuficha sijawahi kuona mpiga gitaa mahiri kama Wanted! yule jamaa mchawi wa solo gitaa.Je una contacts zake?
Moses Gasana
City University London

John F Kitime said...

Wakati picha hii inapigwa ilikuwa mwishoni mwa mwaka 1989 wakati wa Top ten Show. Shaaban Wanted alikuwa amekwisha acha na kuelekea Vijana Jazz. Kasaloo yupo Dar Es Salaam anapiga muziki katika bendi inaitwa Sandton Sound , sina contact za Shaaban lakini ukitafuta kwenye youtube utapata nyimbo zake za sasa kwenye video, Bado yuko Botswana

Mzee wa Changamoto said...

Uncle Kitime.
Ningependa kuuliza hili kutoa "utata" nilionao. Ni kweli kuwa Shaaban Yohana "Wanted" na Miraji Shakashia "CID" (kama sikosei nick name) walipachikwa majina haya kwa ushabiki wa ushindani wa kimuziki baina yao?
Kama ni kweli, ni nani alianza kupewa jina na ni vipi walihusiana nje ya jukwaa?
Shukrani

John F Kitime said...

Baada ya Shaaban 'Wanted' Yohana kuhama Vijana Jazz na kujiunga na Ngorongoro Heroes katika danganya toto moja ya kisiasa, Vijana Jazz walimfuata Mohammed Shakashia ambae hata wakati huo alikuwa kwenye bendi ya MK Group, alipokuja Vijana ndo akapachikwa jina hilo la CID,kuwa ye ndo 'CID' atakempata 'WANTED'. Najua Shakashia alikuwa anamheshimu Wanted kiumri na kikazi

Mzee wa Changamoto said...

Asante saana Uncle.
Nami sasa niko "up to date" katika tetesi nilizokuwa nazo.
Natanguliza samahani kwani ntasumbua kwa maswali kuhusu muziki na wanamuziki.
Sababu kubwa ni kuwa SINA PENGINE PA KUULIZA NA KUPATA UHAKIKA
HESHIMA NA BARAKA KWAKO.

Adbox