Jukwaa la wapenzi wa mambo ya muziki wa Tanzania-

Breaking

Thursday, February 25, 2010

Vumbi

Kwa wapenzi wa Maquis Original jina la "Vumbi" ni la kutia kumbukumbu nyingi sana, na kwa wale ambao wamekuwa wakiusikia ule wimbo wa Chatanda Ngalula walisikia tena na tena Tchimanga Assossa akilitaja jina hilo wakati Vumbi anacharaza gitaa tamu la solo kwenye wimbo huo. Vumbi kwa sasa anaendelea na muziki huko Sweden na maelezo ya maisha yake kimuziki ni haya. Jina lake kamili ni Alain Kahanga Dekula , alizaliwa katika jimbo la Kivu katika Jamhuri ya Kongo. Baada ya kumaliza High School alianza kupiga gitaa katika bendi ya Bavy National iliyokuweko Uvira Kusini mwa Kivu. Baadae akiwa na kaka yake Rachid King wakajiunga katika bendi ya Grand's Mike Jazz Band wakati huo ikiwa na wanamuziki kama Remmy Ongala,Kasaloo Kyanga,na Kawele Mutimanwa. Akaja Tanzania na kujiunga na Orch.Maquis Original na kati ya nyimbo ambazo anajulikana nazo sana ni Ngalula and Makumbele.Wakiwa na mtindo wa Zembwela-Sendema,alikuwa jukwaa moja na miamba wa magitaa wakati huo akina Nguza Viking "Big Sound" na marehemu Ilunga Lubaba. Vumbi kwa sasa yuko Sweden akiwa na yule mwanamuziki maarufu toka Uganda Sammy Kasule wakiwa na bendi ya Ba makonde wamekwisha toa album CD mbili- Bamakonde na Asante. Akiwa na bendi ya kaka yake Rachid King Orch Grand’s Mike wametoa album ya CD Bolingo Ekeseni


1 comment:

John Mwaipopo said...

Ngalula and Makumbele! we acha tu. masongi haya yakipigwa unatamani kwa nini yasingekuwa dakika 15 hivi. yaani yasiishe. kumbe siri ya urembo ilikuwa dekula. asante tena.

Adbox