Jukwaa la wapenzi wa mambo ya muziki wa Tanzania-

Breaking

Friday, February 19, 2010

Jerry Nashon aka Dudumizi


Nimeweza kumpata mtu ambae ndiye aliyemlea Jerry Nashon kimuziki na haya ndo aliyoniambia kuhusu Jerry. Nae si mwingine bali ni Bwana Ruyembe ambae kwa sasa ni kiongozi pale Baraza la Sanaa la Taifa

Jerry alikulia Musoma Mjini kijiji kiitwacho Kigera kilichopo Halmashauri ya Manispaa ya Musoma jirani na shule ya Sekondari Mara. Nilikutana naye mara ya kwanza akiwa Musoma Catholic Mission club ambayo leo ni Mwembeni secondary School akiwa anajifunza kupiga gitaa. Alikuwa ana mazoea ya kwenda kwenye hiyo social club ya kanisa iliyowaunganisha vijana wanamichezo mbalimbali. Nilimchukua katika Bendi yangu niliyokuwa nimeiunda muda huo 1980s ikiitwa Special Baruti Band. Nilimuunganisha na Mpiga rhythm wangu akiitwa Charles Koya ambaye hivi sasa anapiga na Bendi ya Mwanza Hotel (solo guitar), ili amwendeleze na akiwa pia mwana Bendi wetu. Alikuwa mwanafunzi mzuri alikuwa na bidii na akaweza baada ya muda mfupi kupiga programu yetu kubwa! Mimi nilikuwa mtunzi na mwimbaji licha ya kumiliki Bendi hiyo. Tulirekodi naye mara ya kwanza TFC pia RTD na baadaye tulirekodi Kenya katika studios mbalimbali na producers mbalimbali na tumepiga muziki clubs mbalimbali Nairobi ikiwa kama vile Bombax Hotel, Kaka Night Club, Rwadhia Night Club na nje ya Jiji katika mikoa takribani yote ya Kenya kasoro Mombasa na Kisumu! Hapa tulishirikiana na mwanamuziki hodari Joseph Kamaru. Muda huo yeye akipiga gitaa la rythm na Bendi yetu wakisaidiana na Koya. Jerry alivutiwa na uimbaji pia utunzi baada ya kuona nafasi niliyokuwa nayo na umaarufu nilioupata enzi hizo Nairobi. Alijifunza nikampa mwanga na kipaji chake kikajitokeza katika kuimba na utunzi pia!.Hatimaye Jeshi la Magereza Musoma walimchukua kwa nia ya kumleta Dar ajiunge na Bendi yao ya Magereza. Alipitia mafunzo na aliondoka baada ya kuwa na Special Baruti kwa miaka miwili na nusu hivi au mitatu. Muda huo Musoma kulikuwa na Musoma Jazz Band(segese) ambayo mimi na wanamuziki wengi wa Special Baruti tulipigia baadaye tukahama na kuiacha hali mbaya! Ilikuwepo pia Mara Jazz Band(Sensera) hizi ndizo zilikuwa Band maarufu mjini hapo wakati huo. Aidha ilikuwapo bendi iliyomilikiwa na Parokia ya Catholic Mission Makoko Seminary ikiitwa Juja Jazz Band lakini ilikuwa ndogo sana na haikuwa kwa misingi ya kibiashara zaidi!. jerry Baadae alijiunga na Bima Orchestra na kisha Vijana Jazz mpaka mauti yake.


11 comments:

Baraka Mfunguo said...

Jerry Nashon alikuwa akijulikana kama Dudumizi. Jamaa alikuwa na sauti nzuri Wimbo wa "Theresa" aliouimba na Selemani Mbwembwe wakiwa vijana ulinivutia sana. Jamaa alikuwa na sauti nzuri kiukweli na nimeshamwona akiimba na BIMA LEE pale "Hunters Club" maeneo ya Ubungo sasa hivi ni Kanisa la walokole.

Anonymous said...

Kakaaa umenikumbusha enzi za wimbo wa immaculata (RIP) Jerry Nashon 'Dudumizi'

Mdau

Muddy

Anonymous said...

Hapa kweli kuna gundu nilitegemea leo ningekuta habari za Hamis kitambi kwani kunajamaa juzi alinigusa sana alivyotoa taarifa za mzee wetu kwani sikuwa najua kama alipata ajali na kutelekezwa na habari nilizozipata kwa jamaa mwingine baada ya kumuelezea akaniambi kuwa Mzee Kitime ni kiongozi wa chamudata sasa hebu tupe habari huyo mzee nasi tujue
mdau wa uk

John F Kitime said...

Kitime aliacha uongozi na uanachama wa Chamudata SEPTEMBER 1999. hujapata taarifa sahihi

Anonymous said...

Nimekupa vizuri mzee Kitime inawezekana alienieleza alikuwa hajui kama haupo tena ktk uongozi. Sasa mzee kwa tahazma na upendo tunaomba utupe taarifa za huyu mzee mwenzio usingeje hadi afe kama kina Dudumizi ndio uweke taarifa zake.
Mdau UK

Anonymous said...

Hello mzee Kitime habari za bongo mimi nilikuwa na swali tofauti kidogo huku tukisubili habari za Hamisi Kitambi najua fika unazishugulikia. swali langu ni juu ya hiyo bendi yenu ya Kilimanjaro (njenje)hivi kwanini huwa mnachelewa kutoa nyimbo mpya. kwani hii albam yenu ya Gere mimi nafikili huu ni mwaka 5 au 6 na hata ya kinyanyau ilikuwa hivyo hivyo kabla hamjatoa ya gere manake hata kama mlikuwa mnasubili mauzo hivi sasa nafikili hamna anae nunua tena hizo Albam labda sasa mtoe video ya gere mnaweza kuuza. sasa swali langu ni kwanini mnachelewa kutoa Albam mpya? kama mnataka msaada kwa wapenzi wenu ili mrekodi tunaomba mtufahamishe ili nasi tushiriki kwani mimi ni mmoja wa njenje famili.
Wako James

Anonymous said...

Mimi nakumbuka Jerry Alitoka Vijana jazz na kuingia Bima lee
Mdau
Kisiju pwani

John F Kitime said...

Wakati Jerry yuko Vijana BIma Lee ilikuwa imekwisha kufa. Na Jerry alifia Vijana na mwili wake kusafirishwa kwenda Musoma na Umoja wa Vijana

Anonymous said...

Jerry alikufa kwa ajali jijini Dar akiwa Vijana Jazz na akasafirishwa na kwenda kuzikwa kwao Musoma, mwaka sikumbuki

kitime said...

Hapana Jerry hakufa kwa ajali aliugua na kufariki, lakini hiyo ajali aliwahi kupata miezi kadhaa kabla kifo chake

Anonymous said...

Jaman ingawa kiumri Ni mdogo lkn Leo mmenikumbusha mbali saaana.kwny msiba wa jerry nashon nilikuwepo ingawa nilikuwa Na miaka 8 hv huko kwetu musoma Na kumjua kwang jerry Ni kutokana Na mzee wangu alipenda Sana kumtaja kila nyimbo zake zilipopigwa redio tanzania

Adbox