Pages

Tuesday, August 9, 2022

MWANAMUZIKI SHAABAN KIBENGO KABUMBI -CADET BONGOMAN HATUNAE TENA




Marehemu SHAABAN KIBENGO- CADET BONGOMAN


Mwanamuziki Shaaban Kibengo  Kabumbi, aliyewahi kuwa muimbaji wa bendi kadhaa nchini kama Akudo Sound, Bicco Stars, na African Revolutions. Amefariki dunia alfajiri ya leo. Shaaban alikuwa maarufu kwa jina la Cadet Bongoman, jina  alilolipata enzi alipokuwa dansa miaka ya 90 kutokana na umahiri wake wa kumuiga vizuri Kanda Bongoman.
Katika miaka ya karibuni alikuwa akipiga muziki na kundi la Mambosasa Mini Band katika hoteli mbalimbali na kwa muda mrefu katika hoteli ya Concord Kariakoo. 

Mazishi ya Shaaban yalitegemewa kufanyika Kimara Mwisho leo 9 Agosti 2022


 

Shaaban kulia akiwa na marehemu Papa Wemba katika moja ya maonyesho



MUNGU AMLAZE PEMA SHAABAN KIBENGO 

1 comment:

  1. Anonymous20:31

    🙏🏾Pumzika kwa amani Shaaban Kibengo.Amen.

    ReplyDelete