Posts

Showing posts from 2014

MAPENDEKEZO YA WASANII KATIKA RASIMU YA KATIBA MPYA.

Utangulizi Baada ya maagizo kutoka Tume ya Katiba ya kuwa kila kundi kutayarisha mapendekezo ya rasimu ya Katiba, wasanii nao chini ya mashirikisho yao manne Shirikisho la Filamu, Shirikisho la Muziki, Shirikisho la Sanaa za maonyesho na Shirikisho la Sanaa za ufundi waliweza kuja na mapendekezo kadhaa ambayo waliyawasilisha katika Tume, kwa bahati mbaya hakuna kipengele chochote cha mapendekezo hayo kilicho ingizwa katika Rasimu ya Katiba. Kwa ushirikiano, Mashirikisho haya ya sanaa yameamua kufikisha mapendekezo yao moja kwa moja kwa Wabunge wa Bunge la Katiba ili kuwezesha vipengele hivyo kuweko katika Katiba yetu mpya. Mapendekezo 1.Kutambuliwa kwa wasanii kama kundi maalumu katika Katiba. Katika Rasimu ya Katika kuna makundi maalumu kadhaa ambayo yametajwa, kama vile wakulima, wavuvi, wafugaji, na kadhalikana hivyo kutambuliwa kikatiba. Wasanii ni kundi kubwa katika jamii ya Kitanzania. Wasanii wapo karibu katika kila kaya Tanzania. Wafinyanzi, wasusi, wapambaji, wanamuziki waigizaji…