Thursday, February 17, 2011

Super Kamanyola ya Mwanza


Beno Villa Anthony

Beno

Mukumbule Parash

Super Kamanyola


Ally Yahaya na Roy Mukuna

Beno na ParashAnna Mwaole

John Hamisi
Mwaka 2006,wanamauziki kadhaa wa zamani walijikusanya na kuanzisha bendi ambayo ilijulikana kama Tanza Muzika, bendi hii ilikuwa na wanamuziki kama akina Kasongo Mpinda Clayton, Issa Nundu, Mukumbule Parashi na wengine wengi wazuri. Pamoja na kuwa bendi nzuri walikosa vyombo na hivyo kuwa chini ya himaya ya jamaa walioweza kuwa na vyombo, ambao nao mwaka 2007 wakajitoa na hivyo kundi hilo kuvunjika. Wanamuziki wachache wakahamia Mwanza na kuungana na  kundi la Mwanza Carnival, hao walikuwa Roy Mukuna, Seseme Omary,Mukumbula Parashi,Issa Nundu, Bonny Chande . Miezi michache baada ya kuanza kwa kundi hili mfadhili wa kikundi akaanza kuugua na hivyo kundi hilo kusambaratika tena.. Wanamuziki wakaamua kurudi Dar Es Salaam na huko Ally Yahaya, ambaye ni mpiga trumpet nae akajiunga nao na wakajipa jina jipya Super Kamanyola. Na ni wakati huu wakaalikwa kwenye bonanza la Villa Park Mwanza, si muda mrefu baada ya hapo uongozi wa Mwanza Villa Park ukaingia katika makubaliano ya  kuifanya Super Kamanyola kuwa resident Band. May 2010 bendi ikahamia rasmi Mwanza. Kundi hili lina wanamuziki wafuatao.Roy Mukuna, Saxophonist na Kiongozi wa Bendi, Ally Yahaya Trumpetist Katibu wa bendi, Seseme Omary Solo guitar na uimbaji, Beno Villa Anthony mwimbaji na mpiga Keyboards, na pia mshauri wa bendi, Mukumbule Parashi muimbaji, Rashid Mwezigo mwimbaji, Anna Mwaole muimbaji, Bonny Chande Bass guitar, John Hamisi rhythm guitar, na Duncan Matembe Drums. Kwa kweli ni burudani kuisikiliza bendi hii ambayo ikiwa inapiga nyimbo za zamani za Maquis, OSS, Tancut Almasi, TP OK Jazz, African Fiesta, utadhani unazisikia bendi zenyewe.Mwanzo