YOUTUBE PLAYLIST

Friday, February 18, 2011

Super Kamanyola ya Mwanza


Beno Villa Anthony

Beno

Mukumbule Parash

Super Kamanyola


Ally Yahaya na Roy Mukuna

Beno na Parash



Anna Mwaole

John Hamisi




Mwaka 2006,wanamauziki kadhaa wa zamani walijikusanya na kuanzisha bendi ambayo ilijulikana kama Tanza Muzika, bendi hii ilikuwa na wanamuziki kama akina Kasongo Mpinda Clayton, Issa Nundu, Mukumbule Parashi na wengine wengi wazuri. Pamoja na kuwa bendi nzuri walikosa vyombo na hivyo kuwa chini ya himaya ya jamaa walioweza kuwa na vyombo, ambao nao mwaka 2007 wakajitoa na hivyo kundi hilo kuvunjika. Wanamuziki wachache wakahamia Mwanza na kuungana na  kundi la Mwanza Carnival, hao walikuwa Roy Mukuna, Seseme Omary,Mukumbula Parashi,Issa Nundu, Bonny Chande . Miezi michache baada ya kuanza kwa kundi hili mfadhili wa kikundi akaanza kuugua na hivyo kundi hilo kusambaratika tena.. Wanamuziki wakaamua kurudi Dar Es Salaam na huko Ally Yahaya, ambaye ni mpiga trumpet nae akajiunga nao na wakajipa jina jipya Super Kamanyola. Na ni wakati huu wakaalikwa kwenye bonanza la Villa Park Mwanza, si muda mrefu baada ya hapo uongozi wa Mwanza Villa Park ukaingia katika makubaliano ya  kuifanya Super Kamanyola kuwa resident Band. May 2010 bendi ikahamia rasmi Mwanza. Kundi hili lina wanamuziki wafuatao.Roy Mukuna, Saxophonist na Kiongozi wa Bendi, Ally Yahaya Trumpetist Katibu wa bendi, Seseme Omary Solo guitar na uimbaji, Beno Villa Anthony mwimbaji na mpiga Keyboards, na pia mshauri wa bendi, Mukumbule Parashi muimbaji, Rashid Mwezigo mwimbaji, Anna Mwaole muimbaji, Bonny Chande Bass guitar, John Hamisi rhythm guitar, na Duncan Matembe Drums. Kwa kweli ni burudani kuisikiliza bendi hii ambayo ikiwa inapiga nyimbo za zamani za Maquis, OSS, Tancut Almasi, TP OK Jazz, African Fiesta, utadhani unazisikia bendi zenyewe.



7 comments:

  1. Perez15:10

    "...Ufitinaaa..
    na upelelzi ni sumu ya mapeeenzi,

    Ufitina aaaaa,
    na upelelezi ni sumu ya mapeeenzi...
    Mimi kupendwa na yeye...
    Ninyi mwakerwa na nini hee hee hee heee...

    Yeye kanipenda nami nampenda..."

    Mukumbule Lulembo Parash huyo mwanangu.
    Sauti yake ya mawimbimawimbi huwa inaniuwa sana.

    We acha tu.

    ReplyDelete
  2. Dear Friends of Tanzania Wanamuziki kusema lugha yao, lakini mimi katika tafsiri hii ambayo inanifanya internet kwa lugha yako nzuri Natumaini nisamehe lakini mimi hasa upendo huu muziki mimi kutoka Colombia na hapa kusikia mengi hii music kubwa na kwamba ni kwa nini nataka kujua kama kuna uwezekano wa baadhi ya nyimbo kwamba naweza kutoa kwa ajili ya matumizi yangu binafsi, mimi kwa kweli upendo wa aina hii ya bendi ya magharibi music jazz, Simba Wanyika, asante kwa mawazo yako na kiambatanisho mail yangu ambayo nataka kushirikiana katika habari hii wadoso@hotmail.com, mimi kusema Kihispania na natumaini jibu yako itakuwa kuangalia matatizo yoyote pongezi nyingi juu ya blog bora na ...

    ReplyDelete
  3. Anonymous03:58

    Kaka habari za kazi, pole na shughuli za kila siku, mimi nipo na ombi moja naomba kujua jina mwanamuziki mkongwe king kiki naomba kujua jina lake kamili. pia ikiwezekana unaweza kunitumia katika email yangu ya tajiridogo@hotmail.com au kama utap[ost na wengine wanaweza kufaidika pia.
    natangulia shukrani

    ReplyDelete
  4. Anonymous19:03

    Nilikuwa Mwanza wiki mbili zilizopita na kwa kweli Super Kamanyola wako juu. Hakuna bendi itakayoweza kusimama nayo kwa sasa.

    ReplyDelete
  5. Mkuu chokonoa adoado na huku siku moja moja!Mie Mshabiki wa classics

    ReplyDelete
  6. Nimefurahi sana kuisoma habari hii na kujua waliko wanamuziki hawa mashuhuri. Nitajitahidi nikifika Mwanza nikawaone kwa macho. Nawatakia heri wanamuziki hao na kukupongeza sana Mwenye Blog hii. Huu ni mfano wa matumizi bora ya mitandao. Bigup !

    ReplyDelete
  7. Zamani mambo yalikuwa poa.kama ni gitaa utalisikia na kuliona.lakini wakati huu ni mwendo mdundo

    ReplyDelete

SAFARI ZANGU NA BENDI sehemu ya kwanza.

  TANCUT ALMASI ORCHESTRA  wakiwa Jamhuri Stadium Dodoma   Sikumbuki ni safari ngapi za kimuziki nilizowahi kuzifanya hapa nchini katika m...