Posts

Showing posts from January, 2010
Image
Hebu jaribu kupata picha, umelima shamba lamba lako na kupanda mahindi ambayo umeyatunza vizuri na yako tayari kuvuna….. unaamka siku moja na kukuta kuna mtu kayavuna na ameanzisha biashara anapata fedha nzuri wewe huna hata fedha ya kula.Au umenunua suti nzuri akaja mtu akaivaa harusini, kesho yake anakuja kukutaarifu jinsi walivyomsifia harusini.Hiyo ndio picha ilivyo katika shughuli za sanaa Tanzania. Na haswa katika mambo ya muziki na filamu.Wasanii hufanya kazi ngumu ya kutunga na kufanya mazoezi kisha kurekodi kazi zao, kabala hawajafaidi kazi zao hukuta shamba lao likiwa linavunwa kwa njia mbalimbali. Wengine hurudufu kazi zao, wengine huzitumia kutangaza biashara zao. Wengine huzitumia kuhamasisha mikutano yao, wengine huziuza kwa kuwarekodia watu katika simu, katika yote haya mwenye shamba haoni mafao yoyote.Kutokana na matumizi mengi ambayo yanaweza kutokana na kazi zilizotungwa, na kutokana na ugumu wa kudhibiti kazi hizi sheria zinazitwa za Hakimiliki hutumika katika kulin…