Jukwaa la wapenzi wa mambo ya muziki wa Tanzania-

Breaking

Thursday, October 7, 2010

Upanga Story extra

Picha hii ina maana nyingi kwa wapenzi wa Groove Makers. Hapa ni wakali wawili wa GrooveMakers wakiwa katika mazoezi ya Karate. Hakuna zawadi kwa kuwataja japo itakuwa vizuri kupata taarifa ya kipindi hiki

10 comments:

Anonymous said...

Kutoka kushoto ni Marijan Rajabu

kitime said...

Loh hapana huyo wa kushoto mzima kabisa tena naona atajibu mwenyewe

Sam Mnkande said...

Kushoto ni Balozi Maharage,na kulia marehemu Herbert Lukindo, boy I remember those days

Anonymous said...

Hi Sam Mnkande.

Whats UP !!

umekwisha jibu kitendawili sina cha kuongezea.
Mambo yalikuwa -Down Town- Whimpy na Mansons Corner Pub-Independence Avenue.
Hapo hakuna mwngine zaidi ya balozi MMJ "James Brown of all time" na late Lukindo "The Grate Herb - always cool & shy boy

Mickey Jones

Anonymous said...

Mkuu Mickey,

Cozzy Cafe Mkwepu na Makunganya Street Roundabout oppposite na Mbowe na Emms Hotel Independence Avenue, vipi? Dolphines Mkwepu Street na ile Tea Room ya Jamhuri na Mkwepu Street jina lake limenitoka. Kiambaza cha NBC City Drive Branch? Dengu Beach?

Forodhani Hotel, Afrosa wanajifua kuelekea Lagos, Nigeria Fiestac 77' au '78. Trippers inaanza kuyoyoma. Hizi ndiyo tunaweza kuhesabu zilikuwa dakika za majeruhi before things fall apart.

Babake TTC inaungurumisha mahoteli mijini, kanda za Bahari na nyikani. Grill Room kila hotel. Leta safu za mameneja kina Kibogoyo, Kadu, Njunwa, Kabendera, Tibenda, Ali Short naomba uendeleze ........, ......,

Shuttle inakubeba toka New Africa inakuacha Kunduchi Beach. Halafu inakubeba toka Kunduchi Beach inakurudisha New Africa.

Juhudi zako tu shule bure na kazi utapata! Balaa tupu, raha mtindo mmoja, hakuna kuchoka, hakuna stress. ukibamba yale mambo tetlacycline(njano na nyekundu) inamaliza mambo. Gnawing old dry bones is not good, mghh!?

Anonymous said...

Man oh man, hata mimi nimepata nostalgia kali sana. Salaams kwa monsieur l'ambassadeur (MMJ). Herbert, rest in Peace. Jimmy.

SamMnkande said...

Mickey, Bado nipo nipo tuu my bro. Still chasing the almighty dollar here in the US. BTW are you on facebook ? and if not you gotta join man. I have managed to convince a lot of our old friend to join and it would be great to have you on there. Until then Cheers and Ciao

Anonymous said...

Nakumbuka vijana hawa late Lukindo na balozi MMM enzi zile walikuwa wanaongopa kuenda mitaa ya uswahilini karikakoo ,kama vile mtaa wa Livingstone kwa marehem Kintosa..heti wata..

Anonymous said...

poa

Freddy Macha said...

Nakumbuka Groove Makers ilipoundwa...ilivuma kwa muda kisha ikanyauka. Tulikuwa na bendi kibao za vijana mjini baada ya mwana-Blues- Buddy Guy kuja Tanzania (1969). Sparks, Comets, Tonics, Afro 70, Barkeys (siku hizi Tanzanites), Sunburst, Rifters nk. Bahati mbaya enzi hizo hakukuwa na TV wala tasnia ya muziki kama ilivyo leo na Bongo Flava. Ingekuwa hivyo tungefika mbali. Ndiyo maana Blog lako John Kitime ni mwenge pekee unaomulika siku hizo...bila hivyo hakuna mtu angewakumbuka marehem Herbert Lukindo...na wengine wengi- Kassim Magati, James Mpungo, Choge Sly, nk

Adbox