Jukwaa la wapenzi wa mambo ya muziki wa Tanzania-

Breaking

Friday, August 20, 2010

Vijana Jazz enzi za Ngapulila
Kati ya awamu nyingi za Vijana Jazz Band moja iliyoleta changamoto na furaha ni ile awamu ya nyimbo , Ngapulila, Ogopa Tapeli, Adza. Pichani baadhi wa wanamuziki wa wakati huo. Picha ya kwanz a juu- Mzee Joseph Nyerere akiwa na Kulwa Milonge na Hamis Mnyupe, picha ya pili wapiga trumpet marehemu Chondoma, Hamis Mnyupe, na Kulwa Milonge. Picha ya chini ni kundi zima la Vijana Jazz wakiwa na Mheshmiwa Seif Khatib, hapa wanaonekana akina Shaaban Dogodogo, Hemed Maneti,Shaaban Wanted, Abou Semhando na wengine wengi.Kama unavyoona alama za x wengi hawapo tena nasi duniani.

12 comments:

Anonymous said...

Naikubali hii awamu ya Vijana Jazz. Pale kulikuwa na muziki wa kutosha. Lakini pia marehemu Jerry Nashon alileta uhai mzito alipojiunga na Vijana. Vibao kama Top Queen hadi leo ni moto wa kuotea mbali. Pengine huo ndio ulikuwa mwisho wa Vijana Jazz ya ukweli. Siku izi wanaimba kwaya kama TOT wala wanachopiga hakieleweki ingawa naona wamejaruibu kurudia baadhi ya nyimbo studio. Vijana Jazz na Washirika Tanzania Stars walikuwa mwisho wa matatizo. Nilipendelea sana hawa maana walikuwa kwenye utoto wangu. Hii haimaanishi JUWATA, DDC, OSS na marquis hawakuwa vyema, ila nyakati zangu hao ndo walikuwa juu.

Anonymous said...

Naikubali hii awamu ya Vijana Jazz. Pale kulikuwa na muziki wa kutosha. Lakini pia marehemu Jerry Nashon alileta uhai mzito alipojiunga na Vijana. Vibao kama Top Queen hadi leo ni moto wa kuotea mbali. Pengine huo ndio ulikuwa mwisho wa Vijana Jazz ya ukweli. Siku izi wanaimba kwaya kama TOT wala wanachopiga hakieleweki ingawa naona wamejaruibu kurudia baadhi ya nyimbo studio. Vijana Jazz na Washirika Tanzania Stars walikuwa mwisho wa matatizo. Nilipendelea sana hawa maana walikuwa kwenye utoto wangu. Hii haimaanishi JUWATA, DDC, OSS na marquis hawakuwa vyema, ila nyakati zangu hao ndo walikuwa juu.

Anonymous said...

Mimi naomba msaada kwa yoyote ajuaye, Hivi huu wimbo wa Ngapulila aliutunga nani? na pili ukiusikiliza huu wimbo mwanzoni kuna muimbaji anasema hey ngapulila;Namkumbuka vizuri sana alikuwa ana cheza ile mbaya hivi ni nani kwa jina na yuko wapi hivi sasa, Maana hakukaa sana Vijana jazz I have no idea why, Help please,
Big fan,Lilian,Orlando,Fl.

John Mwakitime said...

Nadhani unamuongelea Adam Bakari aka Sauti ya zege. Yeye ndie alikuwa mwimbaji wa wimbo huu wakishirikiana na Eddy Sheggy, na ndie alikuwa anacheza sana. Bahati mbaya kwa sasa ni marehemu

Mdau Usa said...

Hivi Kitime yule jamaa alikuwa anapuliza trumpet Everist Bitto yupo wapi nakumbuka mara ya mwisho nilimwona Vijana jazz akitokea Dar international

John Mwakitime said...

Kwa bahati mbaya Evarist Bitto alikwishafariki miaka mingi iliyopita

Madaraka said...

Mtu ambaye sikutegemea kabisa kumuona humu ni Mzee Joseph Nyerere. Lakini inaonyesha jinsi gani muziki unagusa watu wote, wa kila rika.

Na Mzee wetu tunamkumbuka alikuwa mpenzi mkubwa wa muziki.

Ile picha ya Patrick Balisidya nimeipata, nitakutumia punde.

Anonymous said...

Hii group ilikuwa na nguvu ya aina yake, nakumbuka walikuwa wanaweka libeneke pale kinondoni vijana hostel siku ya jumapili mchana, halafu mwimbo wa mwisho wakati bado unapigwa, nusu ya vyombo vya muziki vimeshapakiwa katika fuso au canter ile? Halafu saa tatu,nne hivi, wapo African stereo bar na kuanza show nyigine upyaaa!!!! Hiyo ilikuwa ni energy ya Kitime & co. Au unasemaje Bro?

Kitime J said...

Enzi za Vijana kupiga Kinondoni Stereo Kitime alikuwa bado hajajiunga na bendi hii. Kitime kajiunga mara baada ya recordig ya Ngapulila ambapo Adam Bakari, Eddy Sheggy na Hamza Kalala walikuwa wamehamia Washirika Tanzania Stars.

Anonymous said...

Nashukuru kwa kunisahihisha unajua tena ni miaka mingi imepita kwa hiyo ni rahisi kuchanganya mambo kidogo.Unajua kwa zaidi ya miaka 20 nimeweka makazi katika nchi za skandinavia, na mazungumzo haya huku hakuna kwa hiyo hii blog inanikumbusha sana vile vijiwe ambapo maongezi haya ni kawaida. Kuna wakati Hamza Kalala ilikuwa arudi Vijana Jazz na kuendelea na Pamba moto awamu ya tatu. Iliishia vipi?

Kitime J said...

Kurudia bendi ya zamani huwa ni ngumu maana watu wapya, muziki umeshakuwa mwingine, alikaa siku chache akaacha

Anonymous said...

Big Up John. ningependa pia ujaribu kutukumbusha mashindani ya kumi bora enzi zile za miaka ya 80's na kuna vibendi vidogo vidogo ambavyo navyo vilitikisa kwa muda kama vile Salna Five Brothers N.k. pale nakumbuka kulikuwa na akina Kapelembe Kokoo na Binki Binsalim sijui wapo wapi kwa sasa hawa jamaa. kama una taarifa zao na wengine wengi wadau tungependa kuzijua.

Adbox