Jukwaa la wapenzi wa mambo ya muziki wa Tanzania-

Breaking

Wednesday, August 25, 2010

Blog Mpya ya haki za wasanii Tanzania

Nimekuwa napewa changamoto kubwa kuhusu namna ya kusaidia wasanii wenzangu katika mapambano yao ya kupata haki kutokana na kazi zao mbalimbali walizorekodi au kushiriki. Hivyo basi nimeanzisha blog inayoitwa Wasanii wa Tanzania na Haki Zao ambapo patakuwa jukwaa la kutoa elimu kuhusu haki kama vile Hakimiliki, mikataba ya kazi mbalimbali, pia sehemu ya kupeana maoni na taarifa mbalimbali kuhusu biashara nataratibu nzima za shughuli za sanaa hapa nchini Tanzania. Nategemea wadau mtaweza kuchangia maoni na kuitangaza ili iwe kweli chombo muhimu kwa wasanii wa Tanzania

2 comments:

Anonymous said...

John!
Nikupongeze sana kwa kuutumia muda wako huu walikizo kwa kuweza kuanzishakitu cha kuwasaidia wasanii wetu vijana kwa wazee. Ninaimani ktk kipindi hiki ambacho bendi yenu iko likizo utakuwa ni wakati mzuri sana wa kuweza kutoa elimu na ufahamu kupitia blog hizi mbili ulizo anzisha, japo najua kwa wasanii wa kizazi hiki ni wagumu sana kusoma jambo ambalo ndio kikwazo kikubwa katika maendeleo yao.
Hata hivyo usikate tamaa. Nimependa sana makala yanayoelezea kwa kina kazi za cosota na mambo mengine meengi ambayo ninahakika wengi wetu tulikuwa hatuyajui.
Ombi langu kwa wale tutakao jaaliwa kutembelea site hii tujaribu kueneza ujumbe huu hasa wa wasanii wa filamu na muziki wapate wasaa wa kusoma maandiko haya na yawe na manufaa kwao.
Pia wenzetu wa TRA wangepata nafasi ya kutupatia machache kuhusiana na mkakati wao wa kukusanya mapato mengi katika tasnia ya muziki.Mfano mzirini band yetu ya the kilimanjaro ninahakika mlijisajili VAT na kwa kiasi fulani mna mchango ktk mapato ya taifa.

Anonymous said...

Asante ndugu Kitime kwa kuwa na mawazo mbali mbali kuhusu namna ya kutetea wasanii hapa nchini,kwa mtu kama wewe unafaa sana hata kuwa kiongizi mkuu wa kutetea haki za wasanii lakini kwa upande wangu sioni sababu ya kuwa nawatu kama akinabwana Mkinga kwenye mambo haya,mtu kama huyu ndiye anayezidi ksababisha ugumu kwenye mambo yote ya saanaa hapa nchini,Sisi wasanii tunapotaka kuktana nae ili tuongee kuhusu maswala ya haki zetu kwa ujumla yeye huwa hapatikani ofisini,unaweza kumtafuta hata mwezi mzima kila siku yeye hayupo ofisini sasa huyu mtu wa nini kwenye sana,na habari zilizopo mitaani huyu bwana ndiye ananyonya jasho la wasanii pamoja na wahindi
pia inasemekana ni mcheza kamari maarufu sasa qwatu kama hwa wa nini kwenye sanaa???waondolewe haraka ili kauleta sura mpya na mabadilio katika harakati za kutetea haki za wasanii Tazania.

Adbox