Jukwaa la wapenzi wa mambo ya muziki wa Tanzania-

Breaking

Saturday, July 10, 2010

SITI BINTI SAAD


Kwa kila hali Siti Binti Sadi anastahili kuenziwa. Kwa akina mama, mwanamke huyu shujaa aliyetoka katika familia maskini ya kijijini, ataenziwa kwa kuwa aliweza kushinda mfumo uliokuwa ukizuia wanawake kujichagulia mfumo wa maisha yao, na kuweza kujitokeza kufanya yale ambayo hayakuwezekana kwa mwanamke wa aina yake kabla. Alijitokeza na kuwa mwanamke mwimbaji mwenye nguvu za kuendesha shughuli za muziki katika mfumo uliotawaliwa na wanaume.

Kwa akina mama wanamuziki katika Taarabu, alikuwa ndio ufunguo ya mfumo uliopo ambao taarab inaongozwa na waimbaji wa kike.

Alikuwa ndie mwasisi wa kuimba taarab kwa Kiswahili.

Kwa wanamuziki wote kwa ujumla Siti Binti Sadi ni super star wa kweli.

- Alirekodi santuri zaidi ya 150

- Alikuwa wa kwanza kwenda kurekodi nyimbo zake India May 1928

- Umaarufu wake ulisababisha Columbia Records kujenga studio Zanzibar katika enzi yake ili tu kumrekodi.

Oktoba 1936 aliwahi kufanya onyesho moja huko Pangani na kupata shilingi 1200. Kwa thamani ya pesa wakati ule, mtu aliweza kupanga chumba kwa shilingi 1 kwa mwezi. Na Pangani ilikuwa na wastani wa watu 1500. Si rahisi msanii yoyote wa leo hapa nchini kuweza kufikia Usuper Star huo.

Siti alizaliwa mnamo mwaka 1880 na kufariki 1950.

12 comments:

Anonymous said...

KUMBE NI MWANAMUZIKI WA TANZANIA NDIO ALIANZA KUREKODI KATIKA RECORDING COMPANY YA KIMATAIFA "COLOMBIA RECORDS",HII KABLA HATA YA DRCONGO...NAOMBA WANAMUZIKI TUMUENZI HUYU ICON SITI BINTI SADI

Fadhy Mtanga said...

Uncle JK, ningependa kufahamu hiyo studio ya Columbia ilifia wapi?

Kweli mwanamuziki huyo anafaa kuenziwa. Ingependeza kungekuwa na tuzo ya muziki wa taarabu kwa jina lake.. Maana tukisema ile tuzo ya KTMA hata aliyeibuni tu haenziwi.

John Mwakitime said...

Kumbuka studio siku hizo zilikuwa mobile, tape recorder na microphone moja

Anonymous said...

Ni hakika kabisa huyu mama anastahili kuenziwa kwa namna ya pekee. Marehemu Shaabani Robert aliwahi kunukuu vijembe vya taarabu ya wapinzani wa Siti:

"Siti biti Sadi, ulikuwa mtu lini?
Ulitoka shamba, na kaniki mbili chini,
Kama si muziki, ungekula nini?"

Mistari hii yaonesha Muziki enzi hizo ulikuwa ukilipa na Siti alaikua tajiri kwa ajili ya muziki,ni mfano wa kuiga.

Wakati huo aliweza kuonyesha kuwa Afrika ina wanamuziki wenye vipaji. Mwakitime umenikumbusha magitaa ya kizamani, wakitumia gumbusi, udi nk.

Anonymous said...

Ingekuwa vizuri kama tungejulishwa hizi picha ni za mwaka gani.

Anonymous said...

Nikiwa ni mpenzi mkubwa wa blog hii na muziki wa Tanzania kwa ujumla, nakushauri balozi uwe unai-update blog hii mara kwa mara maana naona imekuwa ikisuasua katika siku za karibuni. Kwa mfano, ninapoandika maoni haya ni siku ya tatu sioni kilichobadilika humu. Sumu ya blog ni kutoweka taarifa mpya mara kwa mara. Mtu ukifungua blog siku tatu mfululizo na kukuta ‘content’ ni ile ile, kinachofuata ni kuachana nayo. Mwisho wa siku, inakuwa haina maana kuwa na blog ambayo haitembelewi na mtu.

John Mwakitime said...

Nakubali makosa

Anonymous said...

Niliwahi kusoma pahali kuwa katika moja ya safari za Siti binti Sadi za kwenda India kurekodi kwa jahazi la injini ("steamer")(kama sikosei katika 1930's) Bi Kidude pia alikuweko kama mmoja wa waitikiaji ("chorus girls") akiwa ni msichana wa miaka 16 au 17. Hii ina maana kuwa tukichukulia kwa mantiki hiyo kuwa Bi Kidude alizaliwa around 1920 ina maana sasa ana kiasi cha miaka 90!!! na bado yuko active. Kama kuna mtu ana data kuhusu hilo nitashukuru tukiipata hapa. Kama sikosei katika miaka ya 1980's na 1990's kulikuwa na jarida la TAMWA likiitwa 'Sauti ya Siti'; je hilo jarida bado liko? (sijaliona miaka mingi). Jimmy.

John Mwakitime said...

Ni kweli kwa kufuata matamshi yake mwenyewe, kuhusu kumfahamu na mahusiano yake na Siti Binti Saad inaonyesha kuwa Bi Kidude lazima ana miaka zaidi ya 90, japo mwenyewe hajawahi kusema kama aliwahi kwenda India na Siti Binti Saad

Anonymous said...

You are right nimecheki na mzee mmoja wa Zenji leo naye ameniambia kuwa Bi Kidude walijuana na Siti lakini naye huyu mzee hajawahi kusikia kuwa alikuwa katika msafara wa Siti wa India.

Anonymous said...

Mkuu, katika 1970's mpiga bass wa sunbursts alikuwa ni Bashir (Mzenji). Late 1970's Bashir na ndugu zake (pamoja na sista wake mmoja) walikuwa na bendi yao ambayo walipiga kwa muda pale Selander Bridge Club (formely Italian Club). Niliwahi kumuona baba yake Bashir - Mwalimu Iddi - ambaye alikuwa ni mwalimu wa sanaa na muziki ZBR wakati akija DSM na Malindi Musical Club 1980's na 90's. Nilisikia Bashir amerudi ZBR kutoka Dubai. Kama wazee kama Maalim Iddi bado wapo nadhani hao ni hazina kubwa ya historia ya muziki TZ (tukumbuke kuwa zamani wakati wa pasaka timu za mpira na bendi za muziki na klabu mbalimbali zilikuwa zikitembeleana kwa zamu kila mwaka kati ya DSM na ZBR hadi 1970's). Of course kuna wazee wengine kama vile kina mzee Ali Sykes ambao wana hazina kubwa ya historia ya zamani. Itakuwa vizuri kama Wizara ya Utamaduni na Baraza la Muziki la Taifa wataanza kukusanya simulizi ya historia ya muziki na utamaduni kwa jumla na kuiandika kabla historia hiyo haijasahaulika. Eddy.

TANCOMPUTER said...

Ombi langu kwako kaka JK ni kutaka utuwekee baadhi ya nyimbo alizowahi kuimba Siti Binti Sadi ili tuzisikie na tuone tofauti ya nyimbo za taarabu za leo.

Adbox