YOUTUBE PLAYLIST

Monday, July 5, 2010

Orchestra Mambo Bado





Orchestra Mambo Bado ilikuwa bendi ambayo haikukaa kwa muda mrefu katika anga za muziki. Bendi hii ilianza mwaka 1981, ikiwa chini ya 'Mtoto Mzuri' Tchimanga Assossa ikajulikana sana kwa ajili na mtindo wake ulioitwa Bomoa Tutajenga kesho. Pichani Sadi Mnala Drums (yuko Msondo), William Maselenge rythm guitar(marehemu), Andre Milongo(?), Bass na Second Solo, Kazembe wa Kazembe(marehemu) Solo guitar. Pamoja nao walikuweko John Kitime(Njenje), Jenipher Ndesile (?), George Mzee(Marehemu), Likisi Matola(Moonlight Band),Lucas Faustin(Police Brass Band) na Huluka Uvuruge(Msondo), baadae Athumani Cholilo(Marehemu) na Banza Tax(Marehemu), Selemani Nyanga(Uholanzi), Nana Njige(Marehemu). Wimbo wao Bomoa Tutajenga Kesho ulipigwa marufuku.

5 comments:

  1. Asante sana mzee Mwakitime, siku-note kama nawe ulikuwemo kikosini, bravo kaka. Hii bendi ilidumu muda mfupi lakini ilikuwa na vibao moto sana. Umenifanya nimkumbuke tena marehemu Nana Njige kwa kweli huyu dada alikuwa ni unique kama Kida Waziri kwa sauti zao zinazojipambanua. Umenikumbusha kibao "Ilikuwa jambo dogo, Ilikuwa jambo dogo tu mama, mitaani kote limeshaeneaa jamaaa...angalia sasaa...angalia sasaa umeshazeeka".
    Sauti ya Nana hapo ilichombezea kwa raha tamu inayopita sikioni hadi moyoni

    ReplyDelete
  2. Sie ndo tulikuwa wanzilishi, tukiwa na nyimbo kama Bomoa tutajenga kesho,mawazo, kutokuelewana, wakati huo mwimbaji wa kike alikuwa Jenifa Ndesile

    ReplyDelete
  3. Anonymous16:35

    Kitime shukrani sana kutukumbusha Orch.Mambo Bado na hongera sana kwa Tshimanga Assosa kwa vile anazidi kulisukuma libeneke(Bana Maquiz).
    Bendi karibu ya Mwisho ambayo mpiga solo Kazembe wa Kazembe alikua nayo kabla hajatangulia kwa Mola ilikua Chamwino Stars alikua akishirikiana na Dekula Kahanga(Vumbi)na makao makuu yao ilikua pale Tandale...kiisha Kazembe kachukuliwa na Wafaransa fulani...Dekula Kahanga naye kachukuliwa na Maquis hapo ilikua mwaka 1985

    ReplyDelete
  4. Anonymous15:53

    Sakubaa, sakuba sakuba - mambo ya siku hizi
    Discoee, Disco agwaya

    Wew acha tu

    ReplyDelete
  5. Anonymous19:48

    Mdau hapo juu, hicho kilikuwa ni kionjo cha Orchestra Makassy, sio Mamba Bado. Makassy hiyo ilikuwa ni enzi za akina Assosa na Maliki Star.

    ReplyDelete

SAFARI ZANGU NA BENDI sehemu ya kwanza.

  TANCUT ALMASI ORCHESTRA  wakiwa Jamhuri Stadium Dodoma   Sikumbuki ni safari ngapi za kimuziki nilizowahi kuzifanya hapa nchini katika m...