Jukwaa la wapenzi wa mambo ya muziki wa Tanzania-

Breaking

Wednesday, July 28, 2010

Kida Waziri arudi ulingoni

Kida waziri miaka ya 90.

Kida Waziri au kama alivyokuwa akiitwa enzi zake Vijana Jazz Stone Lady amerudi na album yake yenye nyimbo 6 ikiwa na nyimbo kama Wifi zangu, Shingo Feni, Penzi haligawanyiki na nyinginezo, pia ameimba wimbo wa Mary Maria akishirikiana na mwanae Waziri, ambae kajitahidi kuimba zile sehemu za uimbaji wa marehemu babake.

Kida Waziri alivyo sasa.

9 comments:

Anonymous said...

Hongera sana Kida Waziri kwa vile umeamua kurudi tena na kusukuma Libeneke la Muziki wa Dansi tuna subiri hiyo Albam kwa hamu kweli...
Pia natoa hongera kwa Mwanao kwa kufwata nyayo za Baba'ke Maneti, Simba uzaa Simba.

Anonymous said...

Hapa Balozi Kitime bado sijaelewa. Hivi Maneti alizaa na Kida Waziri?

John Mwakitime said...

ndo hivyo

Anonymous said...

Ndugu yangu Mwakitime, tafadhali tujulishe concert ya vigogo wakati wa sabasaba ilienda vipi na kama kuna mpango wa vigogo hao kurekodi pamija. Mimi ninaishi nje lakini nitakuwa Bongo karibuni, je nitakupata vipi tufunge mikakakta ya kuendeleza muziki wa dansi?

Anonymous said...

Inawia vigumu kuamini kuwa mara ya mwisho kumuona Kida Waziri akiwa jukwaani ni zaidi ya miaka 20 iliyopita. Inanipa faraja kuona kuwa bado yuko katika hali nzuri kiafya tofauti na wanamuziki wengi (wa kike na kiume) waliotamba enzi zake. Nampongeza sana kwa kujitunza na ninasubiri kwa hamu vibao vyake vya zamani alivyovitoa upya.

Anonymous said...

Ebwana we si mchezo, inabidi tujue ni wapi tukakumbushie enzi, mambo supa ...oh Kida. Hebu sikiliza hapa "kwanza wangeniulizaaa...kipi ananipendeaaa...wanadhani miti shambaaa....na mapenzi hayana dawa jamani nifanye nini..". binti alikuwa na sauti tamu sana huyu.

Maselepa
Kimara Suka

Bana said...

Afanalek! Bravo Kida Waziri. Kwa kweli habari hii imeniamshia simanzi kubwa sana kila nikikumbuka enzi zile za Vijana. Natamani ingewezekana ikarudi upya kama hivi kumbe Kida bado yuko bomba na ameweza kurudi kwenye game. Sijajua hizo nyimbo amezirudia na Vijana ya sasa au Zingzong. Tatizo Vijana imeuawa na TOT, baada ya kuundwa TOT nguvu zimeelekezwa huko ingawa bendi hiyo haiuziki na kuisahau Vijana. Kama ingewezekana Mzee Mwakitime fufueni Vijana ipate nguvu na Kida kama hivi yupo enzi zitarudi tu.

Bana
USA

Anonymous said...

Mdau Bana nafagilia pendekezo lako kumbe wengi wana hisia kama mimi, mimi nashangaa kwanini CCM haiwapi shavu Vijana. Enzi zile kampeni za CVCM ilikuwa ni Vijana Jazz hata ule wimbo wa Ali Hassan Mwinyi apewe kura za Ndiyo. Leo watu wanang'ang'ania kupoteza fedha kugharamia bendi ambayo haiuziki ya TOT. Waliounda TOT na hasa Komba wanawajibika kutoa maelezo kwanini TYOT na Vijana zisiungane ili hadhi ya bendi irudi kama zamani. Komba Vijana itakulilia hata kaburini

Maselepa

"Mzee wa Zamani"
Kama Zamani Sports Club
Kimara Suka

lindsey said...

Mimi si mpenzi sana wa kuchangia lakini nimekunwa na observations za mkaka Maselepa na ndugu Bana. Kwa kweli hata mimi nashangaa TOT inasubiri nini isizikwe, maana alikuwa Banza akatoka akaja Choki akatoka then Badi Bakule akakimbia pia then Pauline Zongo akatolewa kwenye bongo flavour ili TOT iinuke but ikawa hoi kisha akachukuliwa Muumin bado ikawa hoi hadi sasa ipo kwa ajili ya kusubiri kampeni mtu mmoja avune mamilioni kujaza tumbo lake. Hii ni lana ya kuidhoofisha Vijana Jazz inawarudia. Kwa kweli Vijana ilikuwa moto namkumbuka yule Gotagota na Jerry ilikuwa balaa.

Adbox