YOUTUBE PLAYLIST

Sunday, July 18, 2010

Drums

Ukisema drums katika anga za muziki utakuwa umeeleweka kuwa unaongelea zile ngoma za kizungu ambazo hupigwa kwa kutumia miguu na mikono. Uwingi wa drums huanzia ngoma kubwa moja na ndogo moja (snare), na tasa moja (Hi hat), na kuendelea kwa uwingi kadri ya utajiri na uwezo wa mpiga drum. Katika nyimbo za Dar es Salaam Jazz ambazo zilirekodiwa kwenye miaka ya 30, drums zilitumika hivyo si chombo kigeni katika muziki wa Tanzania. Katika miaka ya sitin chombo hiki kilitoweka katika bendi nyingi za muziki wa rumba, lakini kikarudi tena kwa nguvu baada ya kuingia kwa staili ya kavacha kutoka Kongo. Bendi ambazo zilikuwa zikipiga muziki wenye mahadhi ya kimagharibi ziliendelea na drums katika kipindi chote na kuweza kuunganisha na tungo za zao za rumba kwa ufanisi mkubwa kama ilivyotokea kwa bendi kama Afro70. Drum huwa chombo kinacholinda spidi ya wimbo, na staili ya wimbo, kama ni chacha, tango, waltz au ngoma ya Kimakonde au Kipogoro. Drums huweza kuleta utamu sana kama zikimpata mpigaji.
Siku hizi kuna drums za umeme, hizi huwa na uwezo wa kuongeza au kupunguza sauti, na kuzibadili zikalia milio mbalimbali, kwa mfano kulia kama ngoma za kihindi au kulia kama tumba au hata nyingine zinaweza zikipigwa zikawa zinatoa milio ya ndege!!!.Bendi ya kwanza kuwa na electronic drums ilikuwa Chezimba, wakati huo drums zikipigwa na Charles Mhuto, Tanzanite nao wakanunua zao, na kwa upande wa bendi za rumba MK Group, ikifuatiwa na Vijana Jazz na Bima Lee walikuwa wa mwanzo kuwa na drums hizi

3 comments:

  1. Asante saana Uncle kwa kufafanua hili.
    Tukingali pamoja na tunaendelea kufuatilia, kujifunza na kuheshimu kazi ya hawa wengi uwazungumziao humu
    BARAKA KWAKO

    ReplyDelete
  2. Anonymous21:26

    Kwa Kuongezea wadau wa blog hii ya Balozi Kitime:
    Ukitaka kuona jinsi mpiga drums wa muziki wa dansi anavyotia mashamushamu ktk miziki yetu ya dansi ya Kiswahili tembelea webusaiti ya Youtube halafu search: 'Track4.mp4' hapo utawaona kina Kawelee Mutimwana (ex- Tancut Almasi)na timu nzima wakifanya mambo, maana siku hizi muziki proper wa dansi ni adimu kuuona 'live' .

    ReplyDelete
  3. Anonymous11:57

    Mdau hapo juu nakubaliana nawewe inapokuja upigaji stadi wa drums. Huyu bwana Kawalee Mutimwana anajua anachofanya. Hata huyu ndugu anaepiga tumba pia anajua kazi yake. Rythm inapigwa vizuri kwenye huu wimbo na ipo kwenye mfumo wa second solo. Solo linapigwa kwa ufundi na hasa pale anapopiga kwa kushika nyuzi mbili mbili kabla ya chorus. Keyboard kimepigwa vyema. Hapa kimetumika namna ambavyo gitaa la rythm linapaswa kupigwa hivyo hakukuwa na makelele. Na nakiri ujumbe wa mziki upo juu maana unawakumbuka mashujaa wa Africa sio kutaja taja mapedeshee.

    Tatizo langu kubwa lipo kwenye waimbaji. Ukiachilia mbali huyu bwana anaepiga second solo (aliyevaa t-shirt ya jeshi) vocalist wengine wanautata. mmoja wapo anaimba off-key kabisa. huyu mwingine anaitikia kwa kusita kabla ya chorus na inapofika chorus lead vocal yake inashindwa kupata timing nzuri anajikuta akiacha beat (drums). Ndio maana nalia kila siku na akina mzee Kitime, hebu fundisheni vijana muziki. Huu wimbo wanaoimba ni mzuri mno ila unaharibiwa na vitu vidogo vidogo nilivyosema. KWanini vijana hamtaki kwenda shule ya mziki. Kama hamuwezi basi kaeni kwanza makanisani mjifunze kwenye kwaya kama mimi au misikitini kwenye kaswida kama Banza Stone kabla ya kuutaka uanamuziki.

    ReplyDelete

SAFARI ZANGU NA BENDI sehemu ya kwanza.

  TANCUT ALMASI ORCHESTRA  wakiwa Jamhuri Stadium Dodoma   Sikumbuki ni safari ngapi za kimuziki nilizowahi kuzifanya hapa nchini katika m...