YOUTUBE PLAYLIST

Thursday, July 15, 2010

Atomic Jazz Band


Atomic ilikuwa moja kati ya bendi zilizowika sana nchi hii. Bendi iliyokuwa na makazi yake Tanga, Tanga wakati huo ikiwa na vikundi vingi maarufu vya muziki, kama vile Jamhuri, White Star, Amboni, Lucky Star, Black Star. Bass katika bendi hii kwa kweli lilikuwa likiingiza upigaji wa bezi katika kiwango kipya,wapigaji wake walileta changamoto hata walipokuja hamia katika bendi mpya. Pichani toka kushoto John Mbula -Saxophone,Rodgers- mwimbaji, John Kilua-Thumba(huyu alikuwa ni ndugu ya Julius Kiluwa ambaye ndiye alikuwa mwenye bendi),John Kijiko-Solo gitaa, Hemed Mganga-rythm gitaa (niliwahi kupiga bedni moja na mzee Mganga kwa wakati fulani. Tulikuwa wote Orchestra Makassy na ndie baba mzazi wa mwimbaji wa kizazi kipya Kassim Mganga),Mohamed Mzee-Bass.
Picha hii ilikuwa ni jarada la santuri iliyokuwa na wimbo maarufu Mado Mpenzi Wangu. Wimbo ulikuwa ni ujumbe wa kweli kutoka kwa mwanamuziki mmoja kwenda kwa mpenzi wake ambae jina kidogo linafanana na Mado ili kuficha ukweli. Mtunzi wa wimbo huu alikuwa mpenzi sana wa bendi hii na bado kwa rafiki zake anajulikana kwa jina la Mado. Siku hizi amekuwa mpenzi tu wa kawaida wa muziki.

3 comments:

  1. Anonymous17:56

    Nawakumbuka Atomic Jazz enzi zile za kina kilua na kibao cha mafunzo

    "KWENDA NA KUPUMZIKA SIO MOJA KWA MOJA,NA NYUMA PIA UTAZAME UONE YALOTEKEA"

    kweli walitikisa saana,walinifanya niwe nakwenda Tanga week end nyingi,yananikumbusha mengi ya zamani kule nilipokuwa nafikia chumbageni enzi za Da zake mwanahabari LUI GUY na bila ya kuwasahau kina Aisha na Baby wa Mzee Maharage the Great...Tanga kulikuwa ni msitu wa mziki wa aina zote.

    Mickey Jones

    ReplyDelete
  2. Perez19:03

    "Leo nakupasulia ee,
    Mpenzi wangu nikupendae...
    Usione ninatesekaa,
    Niwe peke nikupendae... X 2

    ...nduugu we nihurumiee mwenzio ee niko mashakani,
    Niisije nikapoteae oho oho niko mashakani..."

    Yaani. We acah tu.

    ReplyDelete
  3. Anonymous20:51

    Inaonekana wanamuziki na pia wanamichezo wa zamani walikuwa na afya nzuri kwa muonekano wa hii picha na picha zingine za zamani nilizoona.

    Je, Balozi Kitime nini ilikuwa siri ya afya njema enzi hizo?

    ReplyDelete

SAFARI ZANGU NA BENDI sehemu ya kwanza.

  TANCUT ALMASI ORCHESTRA  wakiwa Jamhuri Stadium Dodoma   Sikumbuki ni safari ngapi za kimuziki nilizowahi kuzifanya hapa nchini katika m...