YOUTUBE PLAYLIST

Tuesday, June 22, 2010

Saba saba..............

KWA KWELI KILA TUKIMALIZA MAZOEZI NATOKA NIMEFARIJIKA KUWA TANZANIA TUNA WANAMUZIKI WA KIWANGO CHA JUU ILA TARATIBU ZETU NDIO MBAYA. KWA WALE WATAKAOHUDHURIA ONYESHO LA HAWA WANAMUZIKI WAKONGWE WATAONA NINI MAANA YA NINACHOSEMA. NA LA KUSIKITISHA NI AINA YA MUZIKI UNAOPIGWA HAPA NAONA NDIO UKO UKINGONI KUONDOKA NA WAZEE HAWA

23 comments:

  1. Anonymous11:00

    Nikweli John, Hawa vijana wetu wa sasa kuna kazi kweli kweli ya kuwapa elimu ya muziki.
    Ninaamini kwa onesho hili tunaweza kutoka na aina ya muziki wa kitanzania kama tukitulia na kufuatilia kwa umakini.Je wazo la kupata wadhamini na kufanya ziara umelionaje?
    Je mwaweza kutengeneza walau mkanda wa activities zozote za maandalizi ya onesho hilo?

    ReplyDelete
  2. Msela13:38

    Eee Bwana Kitime ee,

    Hivi yule Demu PAULINE ZONGO siku hizi yuko wapi?

    Nilikuwa namzimia sana anavyopiga gitaa na kuimba.
    Halafu na ule MWANYA wake ndo usiseme?

    Yuko wapi wangu?

    ReplyDelete
  3. Ngumu kupata ufadhili wa aina hiyo, japo we are planing kwa kujichangisha na kufanya ziara ya mkoa mmoja

    ReplyDelete
  4. Ngumu kupata ufadhili wa aina hiyo, japo we are planing kwa kujichangisha na kufanya ziara ya mkoa mmoja

    ReplyDelete
  5. Anonymous08:37

    kitime hiyo ni kazi rahisi sana kupata wafadhili,naomba ufanye haya yafuatayo:
    1.Nenda kwenye makampuni ya Bia serengeti na Tbl au Makampuni ya simu TTCL,zAIN,zANTEL,tIGO,vODACOM nA Sasatel waombe ufadhili wa kwenda mikoani kuhamasisha huduma zao au vinywaji vyao lakini lazima uwe umeandaaproject proposal ya hiyo shughuli mnayotaka kuifanya

    2.Nenda kwenye miradi iliyo chini ya wizara ya afya kama vile Malaria,kifua kikuu na ukoma,Matende na Mabusha uwaeleze idea yako utapata ufadhili wa kwenda mikoani.

    3.Nenda Taasisi kama TACAIDS,TUME YA UCHAGUZI Ongea nao na uwaeleze idea yako hiyo

    4.Mashirika ya umoja wa mataifa kama vile UNICEF,ILO,WFP,WHO,UNHCR Kuna hela za kusaidia program kama hizo.

    NB;Kama utashindwa tafadhali tuwasiliane.

    ReplyDelete
  6. SENETA WA MSONDO09:50

    KILA LA KHERI ILA HILO LA MKANDA ALILOSHAURI MDAU MLIFANYIE KAZI HATA MNAWEZA KURIKODI NYIMBO KAMA HIZO ZA ZAMANI MKAZIRUDIA KATIKA UBORA WA HALI YA JUU MKAZIUZA PAMOJA NA HUO MKANDA WA SHUGHULI YENU NZIMA,VIKAWA NI VYANZO VIZURI VYA MAPATO

    ReplyDelete
  7. Msela15:09

    We Kitime nimekuuliza PAULINA ZONGO yuko wapi siku hizi? Hutaki kunijibu!

    ReplyDelete
  8. Naomba email yako

    ReplyDelete
  9. Msela, kwanza napata taabu kujibu mtu anaetumia lugha ya kuita mamam zetu ' DEMU', pili blog hii haishughuliki na uzurui wa sura za wasanii, tatu umri wa Pauline unamfanya asihusike humu. kuna blogs nyingi ambazo zingekujibu vizuri kuhusu maswali na maoni yako kuhusu mwanamuziki huyo. Aksante

    ReplyDelete
  10. Anon 22:37 plz naomba e mail yako, yangu ni jkitime@gmail.com

    ReplyDelete
  11. Msela18:56

    Poa mtu wangu. Nimekufaham.

    Nilisahau kumbe hii bulogi ya WAZEE.

    Ngoja me nijiSEPEE zangu.

    Kila la kheri.

    ReplyDelete
  12. Anonymous04:25

    Pole na majukumu kaka Kitime.

    Nilikuwa naomba kujua toka kwako au wadua wengine juu ya msanii aliyepiga Saxophone katika wimbo wa 'Cleopatra' ulioimbwa na Zahir Ally na bendi ya Sambulumaa chini ya Nguza Vicking 'Big Sound'. Nilikuwa nafikiri somebody Mlanzi lakini sina uhakika.

    Nitashukuru kwa majibu yenu.

    Mdau wa Bakulutu

    ReplyDelete
  13. Anonymous13:42

    Wewe Msela una matatizo. Hii sio blog ya wazee kama unavyotaka kusema. Mimi kiumri sio mzee lakini nakubali nyimbo za enzi hizo. Nakumbuka nikiwa mdogo sana kulikuwa na utamu wa kishindani kati ya Vijana Jazz na Washirika Tanzania Stars bendi iliyoundwa na wanamuziki wengi waliotoka Vijana.

    Hapa nilipo nimetoka kusikiliza nyimbo za Vijana kama vile Top Queen, Mfitini, VIP na Ngapula na zile za washirika kama vile Kety, Madeni, July, Watoto wamekuja juu na yaliyopita si ndwele. Sijapata mshindi mpaka saa izi. Mi naona ngoma draw. Kwa mawazo yangu, miziki iliishia miaka iyo naamini ilikuwa katikati ya miaka ya tisini. Mimi naamini kulinganisha miziki kama ile na ya watu kama Zongo ni kukufuru. Hii ya leo sio miziki ni kuropoka (bongo fleva)na kutajataja majina ya mapedeshee (wanaojiita wanamuziki wa dansi). Nawaheshimu hawa wazee ingawa enzi za DDC, Juwata na zinginezo nilikuwa mdogo mno kuzikumbuka.

    ReplyDelete
  14. Anonymous23:15

    Ndugu yangu Msela!
    Kwa unyenyekevu sana ninadiriki kusema umechemka kushiriki nasi kikombe hiki. Hustahili na ninakushauri kama uu mtu wa busara ni vyema ukajipanga kuchangia katika blog hii bila ya shuruti yoyote. Kuufananisha muziki wa Binti Zongo ama kutaka kujua alipo kwa sasa hapa sii mahali pake. Pia majina magumu unayotumia kuwaita hawa mama zetu tafadhali yaepuke maana japo sikufahamu kwa sura ninashawishika kukutafsiri kupitia lugha zako. Karibu sana pale utakapo kuwa na busara ya kuchangia tafadhali. ninaamini utafanya hivyo kwa kuzingatia machache tuliyokueleza.

    ReplyDelete
  15. Anonymous14:16

    Mchangiaji 22.37 ushauri wa kupata wadhamini katika "project" muhimu yahitaji msaada wako kwa kujihusisha kikamilifu kuwafahamisha watayarishaji watumie njia gani kujiwakilisha na haya mashirika uliyoyapendekeza kuna umuhimu wewe binafsi kujihusisha kikamilifu na wadhamini kuona kama kuna uwezekano wa michango au makubaliano ya kibiashara baadaye kuwahisisha watayarishaji kupitia mawasiliano barua pepe ya watayarishaji.
    Mziki wa zamani umechangia na utamaduni wetu, tusipouhifadhi kikamilifu utakufa pamoja na wanamuziki wa zamani,tutakuwa tumewanyima haki za mziki wa uatamaduni wetu kizai kijacho.

    Mickey "Mikidadi" Jones
    Denmark

    ReplyDelete
  16. Anonymous14:29

    Msela 08:56

    Haujafanya makosa kuingia ukumbi wetu wa wazee,hakuna aliyefikiria una makosa ya kufukuzwa kwa hiyo hauna haja ya kujifukuza wewe mwenyewe kama unalo jipya kuchangia wazee na vijana unakaribishwa,kuna vijana kama wewe wanachangia kuhusu mziki wa zamani wenye mila na utamaduni wetu, uangalifu wa lugha gani unayoitumia humu ndani ya ukumbi wa wazee ndiyo muhimu kwetu.

    Mickey "MIKIDADI" Jones
    Denmark

    ReplyDelete
  17. Anonymous11:41

    Mzee John Kitime mimi nilitaka tu niwashauri muende UNDP mtapata msaada. Nasema hivi manake kabla ya kuondoka Tz nilikuwa nafanya hapo na ninajua mambo yalivyo hapo. Mnachotakiwa tu kufanya ni kuonyesha kwamba muziki wenu (iwe wakati wa sab saba au baada) unawaelimisha watanzania kuhusu uchaguzi ujao. mambo ya kuzingatia ni umuhimu wa kupiga kura, amani, mwamko wa wanawake na uhuru wa uchaguzi. Nendeni kwenye ofisi zao pale Kinondoni (karibu na daraja la salendar) halafu uliza mtu anaitwa Amon Manyama. Yeye ni Assistant Country Representative wa UNDP kwenye maswala ya governance (utawala bora).

    Wadau bado mpaka sasa sijapata mshindi kama nilivyosema hapo juu kati ya Vijana Jazz na Washirika Tanzania Stars. Yani nimchague Edy Sheggy au Jerry Nashon? Commandoo au Shaban Yohana? Hivi jamani nani kama Abdul Salvador, father kivu kwenye keyboard? Nasema tena, japo mwaka wa 92 bado nilikuwa na miaka 12 na nusu, bado nakumbuka utamu wa muziki ule. Nani kasema hiyo ilikuwa miziki ya wazee? Mbona mie siyo.

    ReplyDelete
  18. Anonymous15:17

    John,

    Wakati tunasubiri mambo ya sabasaba tafadhali endelea kutupa uhondo wa muziki wetu wa zamani.....naona kama umevuta hand break kabisa...

    Muarubaini.

    ReplyDelete
  19. Anonymous12:05

    Simsemeo mzee Kitime lakini hii blog sio ya wazee, bali ni ya wote. Isipokuwa maudhui yanalenga kuenzi juhudu zilizofanywa na kizazi kilichopita pia ili kukumbuka mchango wao kwa maana ya kujifunza na kuona leo hii tumetokea wapi. Mimi binafsi nina umri usiofika miaka 32 lakini kila siku nafungua ukurasa huu na pengine ninafahamu historia za wanamuziki wengi tu kwa njia mbalimbali. Babu zangu wawili ni wanamuziki mzee Shem na marehemu Jumbe Batamwanya wa Bima. Hivyo Msela usiondoke, pengine dhana yako ya kumuulizia Zongo ni kwamba at least anaenzi muziki halisi kwa kuweza kuimba kuimba na kupiga chombo kitu ambacho wanamuziki wengi wa leo hawawezi hivyo ni njia ya kuigwa kwani miaka 50 ijayo hawa kina Zongo ndio watakuwa wazee wa zama hizo.

    ReplyDelete
  20. Anonymous11:11

    Wadau!
    Jana majira ya saa moja na nusu usuku nilipata bahati ya kuiona clip ya wakongwe wetu wa muziki wakiwa katika matayarisho ya show yao. Kwa kweli ni kitu cha kuvutia sana na bila shaka panapo uhai sii show ya kukosa.

    Nitumie pia nafasi hii kumshukuru Brand manager wa Bia ya kilimanjaro bwana Geoge Kavishe kwa msaada wake wa kutengeneza tiketi kwaajili ya onesho hilo. Pia watu wa TBC1 kwa kuweza kutayarisha clip na kuirusha. Shukrani za pekee niwashukuru pia WANAMUZIKI wote wanaoshiriki kwenye maandalizi haya maana nimekuwa nikiwaona wengi wakiwasili kwa usafiri wa jamii daladala bila kujali muda wao.
    Wadau wenzangu ni wakati wa kupata ladha halisi za kale na adhimu.
    Ombi rasmi KWA RAIS WANGU KIKWETE. Najua umetumiwa mualiko tafadhali hata kwa saa moja ya muda wako uhudhurie onesho hili kwani wewe uu mpenzi wa muziki. Wadau tununue tiketi zetu mapema tuwape support wakongwe wetu

    ReplyDelete
  21. Anonymous20:53

    duh.huwezi kupata mshindi kati ya washirika watunjata njata na vijana.kwani waliounda watunjata njata ni wanamuziki toka vijana.kama utakumbuka nimekusamehe lakini sitokusahau.lilikuwa dongo hamza alimpiga mtu.nina imani kitime anajua vema aseme ukweli.hamza kalala alilazwa hospital.
    mdau norway

    ReplyDelete
  22. Anonymous04:25

    kitime umechuna??au nimekukera??
    tunapanuana mawazo,naomna kujua bifu la kalala na vujana jazz.mpaka hamza kalala kutunga wimbo.wa nimekusamehe lakini sitokusahau,

    ReplyDelete
  23. Anonymous03:31

    Mimi nashauri wanamuziki vijana wa sasa warudi kwenye back to basics: wajifunze kwanza kuimba na kupiga ala za muziki vizuri halafu ndipo wajaribu kuji-express huku wakitumia miundo na mitindo ambayo inaweza kuwavutia watu, badala ya kuchukua short-cuts zisizo na ubunifu wowote na kuwa na uimbaji usio mwanana na mipigo ya ala isiyo na mvuto wa ndani. All the best balozi jkitime.

    ReplyDelete

SAFARI ZANGU NA BENDI sehemu ya kwanza.

  TANCUT ALMASI ORCHESTRA  wakiwa Jamhuri Stadium Dodoma   Sikumbuki ni safari ngapi za kimuziki nilizowahi kuzifanya hapa nchini katika m...