YOUTUBE PLAYLIST

Wednesday, June 16, 2010

Saba saba 2

Kama ambavyo niliwataarifu ni kweli wanamuziki wa zamani wamepania kufanya show moja ya pamoja siku ya Sabasaba katika ukumbi wa Karimjee. Pia imeonekana shughuli hii iwe inafanyika kila mwaka na ilenge kuwa tamasha la muziki la kila mwaka hapa Tanzania Bara. Wanamuziki wamekuwa wakifanya mazoezi ambayo kwa kweli yatawafurahisha wapenzi wa muziki wa Tanzania. Nawaletea picha mbalimbali za wanamuziki waliomo katika mazoezi hayo nina uhakika mtakuwa mnawafahamu wengi








8 comments:

  1. Anonymous12:00

    asante sana Bwana John kwa mpangilio mzima wa swala hili, kweli watu wataburudika sana na burudani hii, sasa ombi kwa akina fulani kama sie ambao tuko mbali na nyumbani na kwa namna moja au nyingine tutapitwa na burudani hii, twatamani sana kama tungekuwepo, kama itawezekana kurekodiwa DVD au VIDEO kuuzwa ili tuweze kuzipata, nasi japo tufarijike kwa kuona wanamuziki wa kweli walivyofanya mambo siku hiyo, ikiwezekana pia copy hizo zitasaidia kufundisha hawa watoto wanaojiita kizazi kipya maana halisi ya music, maana wameua muziki wa nyumbani, nasikia siku hiyo wote mutapiga black and white kama uniform je ni kweli? sipati picha hiyo siku itakuaje, wish were there, all the best siku ifanikiwe.

    ReplyDelete
  2. Mzee Mwakitime,

    Tutambulishe kwa majina na bendi zao badala ya kuweka picha zao pekee yake.

    Unajua wengi wao wamebadilika sura kutokana na umri kusogea mbele na hata wakati mwingine ni kwa ajili ya ugumu wa maisha mtu anageuka sura.

    This Is Black=Blackmannen

    ReplyDelete
  3. ZeroBrain15:52

    Kitime pole Kaka.

    Nimekuona kule kwa Michuzi unafanya mazoezi na hao Sabasaba 2, kumbe ndo mana umeisahau hii bulogi yako huku kwa muda mrefu kumbe bize nyingi za mazoezi ya sabasaba?

    Pole sana Kaka. Ndo ukubwa huo.

    ReplyDelete
  4. Anonymous02:22

    mzee wetu mimi ni mjukuu ila katika hili la kushirikiana me nakuomba unisaidie najua mna wapigaa gitaa wengi na wazuri sasa me ninawazo hamwezi kupeleka ombi gerezani mkamshirikisha mzee nguza kaika gitaa ilikupata ladha fulani?huku mzee kalala huku nguza he ivi itanogaje?dah kama inawezekana jaribu kuomba unijulishe tafadhali ulaya mambo haya yapo wasanii wanatungamiziki wakiwa jela na watoa ila hapa kwetu sijui ila nakuomba ujaribu ili tufurahie sote najua umahili wa mzee nguza me sina la kukwambia coz we unamjua zaidi yangu kazi njema babu baba yangu ndo hupenda kukuongelea akitwambia kua we ni babu yetu nasi tumezoea ivyo husema niwe keeni cd ya babu yenu yani wewe

    ReplyDelete
  5. Anonymous11:06

    Keep it up mzee Gurumo ndani ya nyumba "Kamandaa", sitakosa siku hiyo

    ReplyDelete
  6. Najaraibu kumsaidia Blackmannen.

    Na.1. Hamza Kalala na Abdul Salvador (Vijana Jazz/Njatanjata)
    2. Shabani Dede na mzee Said Mabera (Sikinde/Msondo)
    3. Mafumu Bilal Bombega (Bicco Stars/African Beats)
    5. Kalala
    6. Muhidini Maalim "Gurumo" na Mabera (Msondo Music Band)
    7. Shabani Dede na King Kikii "Bwana Mkubwa" (Sikinde/King Kikii Double O/La Capitale - "Wazee wa La Prima inawaka "muto" =moto)

    Nimejaribu tu wadau mtanisahihisha

    ReplyDelete
  7. Ahsante sana "Bana" kwa msaada wako wa kunitambulisha majina yao na bendi zao hao Wakulu wetu.

    Wadau tuuendeleze moyo wa aina hii wa kusaidiana pale mwenzetu anapoomba kupewa msaada.

    Hadi dakika hii ninapoandika hapa, nausubiri mzigo wangu wa CD wa nyimbo za zamani. Nilipewa msaada kwa kupewa contact za TBC na "Mdau" mwenzetu. Ninamshukuru sana kwa msaada wake.

    This Is Black=Blackmannen

    ReplyDelete
  8. Anonymous20:20

    sasa Blackmannen ukipokea mzigo nami naomba anagalau nakala.shukran

    ReplyDelete

SAFARI ZANGU NA BENDI sehemu ya kwanza.

  TANCUT ALMASI ORCHESTRA  wakiwa Jamhuri Stadium Dodoma   Sikumbuki ni safari ngapi za kimuziki nilizowahi kuzifanya hapa nchini katika m...