YOUTUBE PLAYLIST

Friday, May 7, 2010

Wanamuziki ndugu 3


Kitendawili kingine. Picha hii ilipigwa Seaview 1974, kuna wanamuziki wa Afro70, na wanamuziki ndugu ambao nao wametoa mchango mkubwa katika fani ya muziki, unawatambua ni akina nani hapo?

16 comments:

  1. Anonymous23:01

    Hapa naona kijana willis tu wengine siwatambui hata kidogo.

    ReplyDelete
  2. Anonymous14:51

    AFRO 70
    Nawakumbuka AFROSA walikuwa jirani zangu Tandika/Temeke Bar ya Mchaga-Temeke Comunity Center.
    Sitokumbuka majina yote lakini nawakumbuka Patrick na Steven Balisidya,Patrick Dick Unga,willis na Shabby mpiga bass.

    Hata hivyo bado sijapata jibu la hawa ndugu watatu yaelekea ni ndugu au watoto wa wanamuziki mashuhuri miaka ya late 60`s na 70`s,naendelea kufutilizia kusikia kwa wengine wenye kumbukumbu ya hawa ndugu watatu.
    Mickey Jones

    ReplyDelete
  3. Anonymous16:17

    Wa pili kushoto ni Salim Willis au...???

    ReplyDelete
  4. Anonymous21:13

    Hapa nawaona vijana wadogo ndugu wawili ambao ni ni George Kapinga wannne toka kushoto na Abraham Kapinga aleshika guitar, hawa walikuja anzisha Bar Keys baadae ikawa Tanzanites bado wapo katika fani
    Balozi Maharage Juma

    ReplyDelete
  5. Anonymous00:29

    John ? hivi aliyekuwa Mh Diwani mahali fulani mkoa wa dodoma Shebby Mbotoni alikuwa mwanamuziki wa Afro 70??na je alikuwa anashiriki chombo gani??

    ReplyDelete
  6. Anonymous08:45

    Shabby Mbotoni alikuwa akipiga saxophone na bass guitar katika Afro band, kwa taaluma alikuwa mhasibu
    MMJ

    ReplyDelete
  7. Anonymous10:37

    Mdau hapo juu!

    Ni kweli kaka Shebby Mbotoni alikuwa Afrosa pamoja na marehemu ndugu yake Yusuph 'Lule',chombo sikumbuki ila kaka Sheby hivi sasa ni hamsa salawat pale Dom!

    Mdau Muddy

    ReplyDelete
  8. Anonymous18:39

    Dk.John Mwakitime,
    Nafikiri uzee umenifika kileleni,nashindwa kuelewa kabisa kwa nini niliwasahau vijana chipukizi kina Kapinga.
    Nawapeni kofia wewe na balozi mhs Maharage Mohamed Juma kwa kumbukumbu.
    wale katika mtihani wa kwanza kama alivyotukumbusha balozi walikuwa watoto zetu kina Omar Sykes.vijana
    chipukizi tulikuwa wote pamoja karibuni kila wikiendi katika ma-Gigi/buggy sehemu mbalimbali.
    Nategemea kuwepo katika sherehe za vijana wa zamani mwezi July ukituwekea ratiba kamili.
    Nafurahi kusikia balozi mhs Maharage pia atakuwepo ni miaka mingi na marafiki zetu wengi wametoweka duniani tumebakia wachache saana itakuwa vizuri kukutana tena.
    Nitaomba ruhusa kwa balozi mhs Mohamed maharage(James Brown) The Groove Makkers, kukuletea picha ya ukumbusho wa vijana katika sherehe za Party miaka ya 70`s picha hiyo ilipigwa tukiwa katika party ya "GET IT TOGETHER" iliyofanyika Upanga.
    Mickey Jones

    ReplyDelete
  9. Anonymous12:34

    Bother Mickey
    Tafadhali hebu rusha hiyo picha natumaini kina Mack Salamba na Gershom wamo pichani
    BALOZI MMJ

    ReplyDelete
  10. Anonymous14:45

    Dk John,

    Nitaipeperusha picha ya Party ya Upanga iliyopigwa na mwanapicha Madohora katika hiyo picha zaidi ya balozi mhs MMJ pia yupo brother "Eddy-Afro" wa mitaa ya
    Somali-Gerezani alikuwa kaka wa msichana mrembo Shakira Osman. Sijuwi ndiyo Eddy huyu namsoma kila mara katika ukumbi huu wa mzee John

    ReplyDelete
  11. Anonymous19:04

    Mimi Eddy si mzee John, ila nilkuwa mtaa wa mkunguni (60's)na baadaye mindu upanga (70's). Siku ikiwadia nikijaaliwa kutoa picha moja au mbili wadau wa miaka hiyo watanitambua (wale ambao uzee haujawaathiri...LOL) By the way nadhani namkumbuka mtu unayemwit Eddy afro wa mitaa ya gerezani. All the best. "mzee" Eddy.

    ReplyDelete
  12. Anonymous14:19

    vizuri ndugu Eddy kutufahamisha nitafurahi kuziona picha ulizonazo mji haukuwa mkubwa kama sasa,wengi tunafahamiana majina na sura,huyu jamaa wa somali-gerezani wengine walimwita "Eddy" na wengine walimwita "Moddy" nategemea tutakutana tena kwa mzee njenje hii july/August tukipata ratiba kamili ya balozi John Kitime.
    mickey Jones

    ReplyDelete
  13. Anonymous22:00

    Wakuu,

    Miye bado nimekwazwa na picha hii. Ikiwa kama huyo aliyeshika guitar ni Abraham Kapinga na picha ilipigwa mwaka 1974 nakwazwa. Kwa sababu Abraham Kapinga wa mwaka 1974 alikuwa anafanana na Abraham Kapinga wa 2010 (Abraham kaumbwa kwa dongo la aina yake). Kama kuna mtu ana picha ya Abraham Kapinga (au Abraham wenyewe) ya 1974 na ya sasa naomba ailete ili kwamba muafiki au muipinge hoja yangu.

    Asante.

    ReplyDelete
  14. Anonymous16:37

    Micky, tukijaaliwa kukutana ntakustua. Enjoy your spring dude!

    ReplyDelete
  15. Micky!
    Ukweli wa washkaji kwenye picha ni Vijana wa Jerry Six kutoka magomeni mikumi siku walipopata kijiko kutoka kwa Afro 70 Band mara ya kwanza. Kutoka kushoto ni Paul Same (Alias Pierro) Salum willis, Paul Mhuto, Ahmed Max (RIP, Steven Balisidya, Msafiri(Almasi´s Brother) na dogo mwenye gitar ni Charles Mhuto na sio Abraham Kapinga. It was the same year that Jerry Six was born 1974.

    Musa Jay

    ReplyDelete
  16. Anonymous06:01

    UKO SAWA Abraham Kapinga hayumo kwenye picha hiyo





    ReplyDelete

SAFARI ZANGU NA BENDI sehemu ya kwanza.

  TANCUT ALMASI ORCHESTRA  wakiwa Jamhuri Stadium Dodoma   Sikumbuki ni safari ngapi za kimuziki nilizowahi kuzifanya hapa nchini katika m...