YOUTUBE PLAYLIST

Thursday, May 20, 2010

Top Ten Show


1989/90 Radio Tanzania kwa ushirikiano na Umoja wa Vijana na CHAMUDATA waliweza kuendesha mashindano makubwa ya bendi yaliyoshirikisha karibu bendi zote Tanzania. Haijawahi kutokea project kubwa namna hiyo ya muziki na vigumu kuelewa kama itawezekana tena katika mazingira ya sasa. Pichani ni Vumbi na marehemu Mbwana Cocks katika picha iliyotoka gazeti la Uhuru wakiwa katika jukwaa Vijana Kinondoni. wakati huo Cocks alikuwa ndo ametoka Vijana Jazz na kuhamia Orchestra Maquis Original, akawa anapiga second solo, rythm akisindikizwa na William Masilenge, solo akiweko Vumbiiiiiiiiiiii

4 comments:

  1. Ni kwamba Dekula Kahanga=Vumbi, huwezi kuamini kuwa ni Mzee wa miaka hiyo. Hata ukimwona sasa hivi anaonekana ni yanki kabisa, sijui anakula nini ndugu yetu huyo kuukarabati uzee.

    Sisi wengine tumejitahidi kuukarabati uzee kwa kuweka pamba za nguvu, lakini wapi. Tunaonekana chokambaya tu. Kaaaazi kweli kweli.

    This Is Black=Blackmannen

    ReplyDelete
  2. Anonymous13:21

    Ndugu Blackmannen,nilikua jirani ya Dekula Kahanga katika Mtaa wa Makanya M'Kondoa Mwaka 1989/90,nafkiri kinacho msaidia kujitunza ni nidhamu,baada ya Kazi ulikua humuoni Mitaani ao Vilabuni, yeye alikua akishinda Nyumbani kwake akipapasa Gitaa.

    ReplyDelete
  3. Anonymous15:39

    Vumbi Dekula na Nguza sijui nani alikuwa zaidi..kwa kweli enzi hizo zilitisha huku Maquis, huku Vijana, huku Sikinde raha tupu!

    ReplyDelete
  4. Anonymous15:56

    Nakumbuka sana tulivyokuwa tukisota na Dekula Vumbi katika foleni katika tawi la Muhimbili la benki ya NBC mwishoni mwa miaka ya 80 na mwanzoni mwa miaka ya 90. Licha ya kipaji chake cha kucharaza gitaa, Vumbi hakuwa akijiona 'supastaa' kama walivyo wanamuziki wa sasa ambao hata kupanda daladala au kusalimia watu wanaona ni kama kujifedhehesha. Vumbi alikuwa ni mtu wa kawaida tu na ni mfano wa kuigwa.

    ReplyDelete

SAFARI ZANGU NA BENDI sehemu ya kwanza.

  TANCUT ALMASI ORCHESTRA  wakiwa Jamhuri Stadium Dodoma   Sikumbuki ni safari ngapi za kimuziki nilizowahi kuzifanya hapa nchini katika m...