YOUTUBE PLAYLIST

Tuesday, May 18, 2010

Taarab ya Tanga


Katika miaka ya 50 wanawake tisa wa Tanga walijikusanya na kuanzisha wakaanzisha kikundi cha kuimba walichokiita Raha til Fuad maana yake Raha ya Moyo. Akina mama hawa chini ya bibie aliyeitwa Mama Akida au aka Mama Lodi, waliendesha kikundi chao wakiwa wanaimba nyimbo za Siti Binti Sadi na tungo zao ambazo waliimba katika melody ya nyimbo za kihindi zilizotamba wakati huo. Kundi hili liliendelea na kuanza kuruhusu wanaume kujiunga hasa wakiwa wapiga vyombo. Hata mtoto wa Mama Akida, Akida Jumbe hatimaye alijiunga na kundi hili kama mpiga accordion kwenye mwaka 1962. Kundi hili ambalo baadae lilikuja kuitwa Young Noverty,liliendelea mpaka kukaweko na mgawanyiko uliozaa kundi la Shaabab Al Waatan. Hapa ndipo kukaanza mtindo wa kuweko kundi pinzani jambo ambalo kwa njia ya ajabu sana limekuwa linadumu kiasi cha miaka kumi kumi. Miaka ya 1960s Young Noverty na Shabaab al Waatan, 1970s Lucky Star Musical Club na Black Star Musical Club, 1980 Golden Star Taarab na White Star Taarab, 1990, Babloom Modern Taarab na Freedom Modern Taarab. Taarab ya Tanga ndo haswa inastahili kuitwa modern Taarab, kwani wao hawkufuata taarab ile iliyoletwa Zanzibar enzi ya Sultan Seyyid Barghash, kundi la taarab hii lilikuwa dogo na vyombo vyake vilikuwa pamoja na Gitaa la besi, gitaa la solo, drums bongos ,akodion au kinanda. Nyimbo zao zilikuwa fupi na si ndefu kama za Kizanzibari., nyimbo zilitegemea mipigo ya ngoma za asili za kumbwaya na chakacha na hata baadaye mitindo kama rumba,bossa nova ilitumika kama mapigo. Na Taarab ya Tanga ndio iliyoanzisha moto wa vikundi vya taarab Tanzania Bara. Moshi kulikuwa na New Alwatan,AzimioTaarab, na Blue Star Taarab , Arusha-Blue Star Taarab,Dodoma-Dodoma Stars,Kondoa –Blue Stars,Mbeya-Magereza Kiwira, Mwanza-ujamaa Taarab, Bukoba –Bukoba Stars, na muendelezo huu uliingia mpaka Burundi kutokana na mwana muziki mmoja alie julikana kama Athmani Mkongo, alitoka Burundi na bendi yake kufika Tanga akawa mwanamuziki mahiri wa Taarab na hata kuipeleka kwao Burundi.(Pichani Waziri Ally wa Kilimanjaro Band, wakati huo akiwa Lucky Star akipiga kinanda)

4 comments:

  1. Anonymous21:02

    waziri ally ndio huyu aliyekuwa msondo ngoma?

    ReplyDelete
  2. Huyo jamaa alikuwa anakigonga kinanda sio Masikhara akiwa Msondo enzi za akina Lusungu. Sikiliza wimbo wa MWENDA POLE na MAPENZI YA WAKE WAWILI "ETHEL". Alikuwa akikizimua sio mchezo.

    ReplyDelete
  3. Anonymous12:14

    Ukitaka kujua kuhakiki umahiri wa Waziri Ally sikiliza wimbo wa msondo utunzi wa Belesa kakere enzi hizo unaitwa Sogea karibu.Kwa wakati ulitokea mgomo wa wapuliza sax na trumpet. Na kama kawaida walio baki wakajipanga na kilichofuatia pale ni Waziri kupewa jukumu la kuziba pengo lile kwa organ ya yamaha. Hebu Kitime muombe waziri atupatie taswira zake alipokuwa msondo na kinanda chake cha kanisani. Alitisha

    ReplyDelete
  4. Anonymous16:36

    Kama kuna wimbo ambao Waziri (Kisinger) alipapasa kinanda hasa akiwa msondo basi ni ulee 'ENYI DADA ZETU (hii ni meli tu naipakua)'

    Jamani naombeni msaada wapi naweza kupata dvd ya on the rumba river ya papa wendo hapa dar

    ReplyDelete

SAFARI ZANGU NA BENDI sehemu ya kwanza.

  TANCUT ALMASI ORCHESTRA  wakiwa Jamhuri Stadium Dodoma   Sikumbuki ni safari ngapi za kimuziki nilizowahi kuzifanya hapa nchini katika m...