YOUTUBE PLAYLIST

Wednesday, May 26, 2010

Shakaza Eddy Sheggy




Mara baada ya kutoa ule wimbo maarufu wa Kisambaa Shakaza, Eddy Sheggy mwenyewe na Wasambaa wengine wakaanza kuitwa Shakaza. Eddy Sheggy alikuwa mwimbaji mzuri na mtunzi mzuri sana. Kati ya bendi alizopitia ni Super Rainbow, Vijana Jazz, Bantu Group, Washirika Stars. Picha mbili za juu ni Eddy akifanya onyesho na Super Rainbow katika uwanja wa Mnazi Mmoja, chini ni wakati akiwa Vijana Jazz

14 comments:

  1. Maabadi07:15

    'Mghoshi wa Kaaya' A Multi - talented Eddy, Will be missed forever....RIP!

    ReplyDelete
  2. Kwa kuongezea Eddy Sheggy aliimbia pia BIMA LEE. Alikuwa na staili yake ya kuimba akiwa ameziba sikio moja.

    ReplyDelete
  3. Mikausho Mikali10:46

    habari za kazi kaka ?
    pole na majukumu.Mimi nami ni mpenzi sana wa blog yako kwani inanikumbusha mbali saana.kuna kipindi uliahidi kuweka nyimbo za Tanzania All stars na kusema ukweli hizo nyimbo sijazisikia miaka kama ishirini na nne ..bado nazisubiria.pia ningependa kusikia wimbo wa MArijani unaoitwa jina lako chakubanga .. nitafurahi kama utaziweka hewani siku moja..

    kazi njema

    ReplyDelete
  4. Anonymous17:41

    balozi...pole na kikao. Ee bwana umenikumbusha mbali sana. Kwa kweli TZ tulikuwa na wanamuziki wazuri sana ila basi tu propaganda za hapa na pale za kukuza muziki usio na vipaji ndiyo unaua kabisa muziki wetu tena kwa makusudi za hongo za bia moja moja mitaani na kualikwa kwenye minuso. Eddy alikuwa ni mtunzi mzuri sana, napenda sana ule wimbo wake wa Milima ya kwetu na nyingine alipokuwa vijana 'kapu la Mjanja' Ila sina uhakika kama wimbo huu ni wake lakini vionjo vyake ni comedy tupu shinda hata ze comedy yenyewe.

    ReplyDelete
  5. Anonymous19:38

    Wakati huo nakumbuka vyombo vya habari vilikuwa vikimpamba sana Eddy Sheggy kuwa ni mwanamuziki msomi, nakumbuka alitoa wimbo wa "Mandela afunguliwe" and "Mandela afungiliwa" humo aliweka ghani za Kiinglish sio mchezo.

    Pia alikuwa na wadogo zake watatu ambao alikuwa kila bendi akienda lazima aende nao!

    ReplyDelete
  6. Perez21:59

    "...Tuulii eee, eee,
    Nikupe nini uridhike, tuli eee,
    Unihurumiee, Tuli eee,
    Cha kukupa siina, tuli ee, Unihurumiee, Mamaaa...

    Ufukara nilionaoe mamama,
    ufukara umekuwa kashfa, ya mapenzi yaangu.....kwaako, kwaako ee,

    Nikawa radhii, nikadiriki nafsi yangu eee...

    ....(tuli ee ee tuli ee)
    Nasikitikaa hiyoo (mama aa mama aa,
    Nasikitika hiyoo..."

    We acha tu!

    ReplyDelete
  7. Anonymous17:33

    Mdau wa hapo juu, huu wimbo si Tulie bali ni Julie na ulikuwa utunzi wa Madaraka Morris (kiwembe), ndani ya Washirika TZ Stars. Vocals: Madaraka, Sheggy, Double T (Toto Tundu - Muhina Panduka), na Adam Bakari (sauti ya Zege). Yaani hii ilikuwa ni timu ya kufa mtu....TZ muziki na vipaji vipo bwana asikudanganye mtu. Huyu balozi mwenyewe ni tishio, alitamba sana Sagha Rhumba na Malaine wake.

    ReplyDelete
  8. Ni wapi zinapatikana album au tungo za Bw. Sheggy? Nazitafuta kuzinunua mpaka sasa zijafanikiwa?

    Bw. Kitime naomba ufanye utafiti kuhusu wapi zinapatikana kazi za wanamuziki au bendi za zamani. Na ikiwezekana uweke bandiko (post) kwenye blogu yako matokeo ya utafiti wako.

    Tupo wengi tunaohitaji kununua na kuweka kumbukumbu wa miziki ya zamani lakini tunakwama wapi kwa kuzipata hizo nyimbo.

    Naomba kuwasilisha
    Mdau
    Faustine
    http://drfaustine.blogspot.com/

    ReplyDelete
  9. Anonymous18:24

    Kweli kabisa wapenzi wa muziki wa dansi tupo wengi na tunasikitishwa sana na ma-dj wa bongo kwa kutaka kuua muziki wetu kwa makusudi.

    ReplyDelete
  10. Anonymous21:19

    madaraka morris yu wapi?maana ananikumbusha mbali sana.enzi za 92 pale sinza.watunjatanjata walikuwa wanatoa burudani safi sana.WIMBO WA KENGE KUTOROKA MAJINI KUKIMBILIA MTONI.niliupenda sana.bila kusahau baba mkwe tapeli.
    MDau wa Norway

    ReplyDelete
  11. Anonymous21:19

    madaraka morris yu wapi?maana ananikumbusha mbali sana.enzi za 92 pale sinza.watunjatanjata walikuwa wanatoa burudani safi sana.WIMBO WA KENGE KUTOROKA MAJINI KUKIMBILIA MTONI.niliupenda sana.bila kusahau baba mkwe tapeli.
    MDau wa Norway

    ReplyDelete
  12. Madaraka Morris yuko Tabora alikuwa akipiga Tabora Jazz

    ReplyDelete
  13. Anonymous17:17

    Wakuu,

    Faustine,

    Miziki ya zamani inapatikana kwenye maduka kadhaa ya Ulaya, Marekani na kwenye mitandao.

    Ninaweza kukutajia baadhi ya CDs ambazo unaweza kuzitafuta kwa majina yake kwenye google na ukapata wauzaji wake:

    1: Tanzania Hit Parade / Various Artists

    2: Dada Kidawa / Sister Kidawa -Various Artists

    3: Muziki wa Dansi / Various Artists

    4: Sikinde /Orchestra Mlimani Park

    5: Sungi / Orchestra Mlimani Park

    6: Pepea / Simba wa Nyika

    7: Amigo / Les Wanyika

    8: Masimango / Morogoro Jazz

    9: Ngoma Iko Huku / Cuban Marimba

    10:Zanzibara 3: The 1960s Sound of Tanzania

    11:Zanzibara 5: Hot in Dar 1978-1983 / Various Artists

    12: Umoja / Watafiti

    13: Bongoland / TatuNane

    14: Tanzania Beat / TatuNane

    15: Swahili Music ( Tanzania & Kenya) 1930 - 1955 / Various Artists

    16: The Rough Guide to the Music of Tanzania / Various Artists

    17: Legends of East Africa / Orchestra Makassy

    18: Nyota / Black Star Musical Club

    19: The Best of Msondo Ngoma / Msondo

    20: The Great East African Trip / Various Artists

    21: Chela chela Vol 1/ Shikamoo Jazz

    22: Leila / Bana Marquis


    Nina hakika unaweza kupata baadhi ya hizi CDs kama ukizitafuta kwenye google na utawapata wauzaji wake.

    Ukizipata utafaidi ile mbaya. Juzi nilikuwa naifaidi Nacheka cheka Kilwa Leo! Babakee, ilinibidi niirudie mara kadhaa maanake zile sauti za waimbaji, midomo ya bata na maguitar nilikuwa sijawahi kuistukia kama mitamu namna ile.

    Nakutakia kila la heri.

    ReplyDelete
  14. Naomba kujua ubini wa Sheggy ? NI Shekabughe? Shekiondo ? Shemahonge??Shebughe??

    Pili hiki kibao cha SHAKAZA kulikuwa na maana gani na kilikitoka mwaka gani ?

    ReplyDelete

SAFARI ZANGU NA BENDI sehemu ya kwanza.

  TANCUT ALMASI ORCHESTRA  wakiwa Jamhuri Stadium Dodoma   Sikumbuki ni safari ngapi za kimuziki nilizowahi kuzifanya hapa nchini katika m...