YOUTUBE PLAYLIST

Wednesday, May 26, 2010

SABA SABA






Ile siku ya kuvaa slimfit,jackson 5, raizon na muziki ulioendana na kipindi hicho inazidi kukaribia. Vikao vya matayarisho vinaendelea. Wanamuziki ambao watapanda jukwaani siku hiyo ni wale wa enzi zile na kupiga muziki wa enzi zao, tunategemea kusikia wakongwe hao wakiporomosha muziki kutoka sehemu mbalimbali za dunia. Pichani ni washiriki wa kikao kilichoendelea leo 26/5/2010. Waliohudhuria Waziri Ally,Ahmad Dimando, Juma Ubao,Crispin Stephan, Godfrey Mahimbo,Kanku Kelly, Jerry Tom, John Kitime.

7 comments:

  1. Anonymous08:19

    John!
    Ni wazo adhimu kuwa na onesho kama hilo tene inatakiwa kuwe na mualiko maalum kwa vijana wa kileo wanaopiga miziki ya dans waone wazee wao wanafanya nini na walipata kufanya nini. Pianingependa kujua iwapo kama kuna uwezekano wa kutoa mialiko binafsi kwa wanamuziki ngulu wanaoishi nje ya nchi kama wakina dulla wa abdallah, seif rengwe wakina mhutto na wengine. Ingependezakama kungekuwa na vionjo toka kwao. Pia wangealikwa watu kama wakini Dr. ufuta kwa heshima tu ili watu wawaone hata kwa usiku huo mmoja. na wengine walio hai ambao pengine ni walinzi ama wanakazi nyingine mbali mbali za kuwapa riziki. Hebu lifikirieni na hilo. vinginevyo mko juu na uwe ndio mwanza wa mambo yenye maana kamahaya badala ya kufanya sherehe za kuwaalika na maseneta kushangilia kile kinachoitwa TUNZO

    ReplyDelete
  2. Anonymous14:42

    Sawa wakuu,
    Vikao viendelee nasi washabiki tupate mafanikio mazuri ya sherehe za sabasaba,nilisoma humu kama Dk Ufuta yupo mji fulani
    mimi ni mmojawapo wa washabiki wake tungependa kumsikia siku hiyo kama "vidole" havijashikwa na ganzi la uzeeni. Tunavifuatilizia vikao vyenu wakuu.

    mickey Jones

    ReplyDelete
  3. Anonymous18:02

    JUMAMOSI NILIMSIKIA ASSOSSA TBC FM AKIELEZEA MPANGO ULIOPO KULE KINSHASA WA WANAMUZIKI WAKONGWE KUANDAA ONESHO LA PAMOJA KUCHANGISHA PESA KWA AJILI YA KUWASAIDIA WANAMUZIKI WALIOPATA KUTAMBA SIKU ZA NYUMA LAKINI HAWAKUBAHATIKA KUPATA MAFANIKIO KIMAISHA.
    BINAFSI NILIFARIJIKA KUSIKIA KUSIKIA HABARI HIZO KWANI KWA NAMNA MOJA AU NYINGINE ZINAONESHA NI JINSI GANI WENZETU WANAVYOJISIKIA VIBAYA KUONA WENZAO WALIOKUWA NAO KWENYE FANI WANAHANGAIKA NA MAISHA.
    NILIWAHI KULIHOJI/KUSHAURI HILI KWENYE BLOGU HII NIKITOLEA MFANO WA MZEE KUNGUBAYA AMBAYE KAMA MTU ULIBAHATIKA KUONA MAHOJIANO YAKE NA TELEVISION YA CHANNEL 10 SIKU ZA NYUMA NI WAZI KABISA CHOZI LINGEKUDONDOKA.
    WANAMUZIKI WETU WA ZAMANI MKIONGOZWA NA NDUGU KITIME MNAWEZA KUKAA CHINI MKALIFIKIRIA HILI ILI ANGALAU HAWA WAZEE WALIOTOA MCHANGO MKUBWA KUPITIA SANAA HII YA MUZIKI ANGALAU WAPATE MAHALA PAZURI PA KUISHI.
    NAAMINI WATANZANIA WENGI WATAKUWA TAYARI KUSHIRIKIANA NANYI.

    ReplyDelete
  4. Perez22:09

    Kitime tuko pamoja.
    Siku hiyo mtupe na sisi vijana wa zamani tusio wanamuziki lakini tunajua kuimba, nafasi ili nasi tuimbe kidogo.

    Waziri namuomba siku hiyo apige ule wimbo wa ETE aliopiga na JUWATA Jazz.
    Kile kinanda alipiga si kawaida wangu.

    "...Pendo lako kwa mume wako oo,
    lilisababisha mwenzio, kuachika bure..,

    Nyumbani ulipoondoka, alikuendea kinyume yakakufikaa maradhii.

    Mapenzi ya wake wawili, hayawezi kuwa ya ukweli, (oooo lelelile)
    yangelikuwa ya ukweli Ete ee, yasingekufika

    Ungelijuaa mama mapema...."

    We acha tu!

    ReplyDelete
  5. Anonymous07:38

    Ete muendelezo

    Ungeyajuaaa mama mapema katu usingejitosa ukewenza umekuponza Etee ee watesekaa

    Mapenzi ya wake wawili hayawezi kuwa ya kweli yangelikuwa ya kweli Etee ee yasingekukuta

    Tutajitahidi nduguzo maradhi yakutokee, mola atkusaidia ndiye mwenye uwezoo.

    Kwenye wimbo huo acha kinanda hata sax limepigwa kwa ufundi wa hali ya juu.

    Perez unaukumbuka na ule wimbo 'ENYI DADA ZEU? (hii ni meli tu naipakua)' elezea.

    Somboko anafahamu lolote kuhusu hii blogu? manake ana maelezo mazuri sana kuhusu muziki wa enzi hizo tunaomba mchango wake.

    ReplyDelete
  6. Perez13:37

    "ENYI DADA ZETU" siukumbuki huo ndugu yangu. Hebu nikumbushe kidogo maneno yake. Labda nimeusahau kidogo

    ReplyDelete
  7. SENETA WA MSONDO11:39

    MDAU NAAMINI UNAPOSEMA SOMBOKO UNA MAANISHA YULE MCHAMBUZI MAHIRI WA MUZIKI WA ZAMANI KATIKA RADIO STATIONS MBALIMBALI HUSUSAN RFA NA REDIO UHURU,KAMA NDIVYO HIVYO YULE ANAITWA RAJABU ZOMBOKO KWELI MCHANGO WAKE UNAHITAJIKA HUMU UNCLE KITIME,

    ReplyDelete

SAFARI ZANGU NA BENDI sehemu ya kwanza.

  TANCUT ALMASI ORCHESTRA  wakiwa Jamhuri Stadium Dodoma   Sikumbuki ni safari ngapi za kimuziki nilizowahi kuzifanya hapa nchini katika m...