Jukwaa la wapenzi wa mambo ya muziki wa Tanzania-

Breaking

Sunday, May 23, 2010

Patrick Pama Balisidya

Mwaka 1996 kwa ufadhili wa Ubalozi wa Netherlands lilifanyika tamasha kubwa la muziki Mnazi Moja, bendi kama Vijana Jazz, Polisi Jazz, Zaita Muzika, Maquis Original, Namtu Group, Shikamoo Jazz, zilishiriki. Hapa Patrick akishirikiana na Vijana Jazz, nyuma yake ni Fred Benjamin mwimbaji wa sauti ya kwanza Vijana Jazz, ambae naye ametangulia mbele ya haki. Siku hii alipiga wimbo wa Ni mashaka na hangaiko akishirikiana na Shikamoo Jazz

6 comments:

Anonymous said...

RIP brother Freddy tungo zako zilikuwa tamu sana kama katherine, Madereva, na wapambe Nuksi.

Balozi: Mwaka 1992 ulikuwa Vijana Jazz, ebu naomba unijazie huu ubeti wa Dudumizi katika ule wimbo wa 'Mtatumaliza.'

'je niambie wewe, mke wa mtu hutembea umelainika kama bamia na ..... mwilini, unataka nini weweeeee?

Tafadhali saidia, huu wimbo mtamu sana. Na asiyekuwa na hii kanda tafadhali tafuteni, thi is the best sagha rhumba kanda ever pamoja na ile ya VIP. Nani anabisha hapa?

Anonymous said...

Nakumbuka sana tukio hili, theme ya tukio ilikuwa 'tutunze mazingira'

Patrick alikiwa backed na Shikamoo Jazz hasa wale wazee wa ala za upepo walipiga vizuri sana moja ya wimbo maarufu wa afro 70 'ni mashaka yangalipo' katika beat ya chacha.

Ilikuwa live kupitia ITV, nalimwangalia Patrick katika feelings za mbali sana....nadhani ki-fikra alikuwa amekwenda mbali sana...hasa enzi za Afro 70.

Kwa mtazamo wangu yeye ni mmoja wanamuziki wazuri sana katika historia ya muziki wa Tanzania.

RIP Patrick.

-Muarubaini

Anonymous said...

Defeated but not resigned!

Anonymous said...

Bro Kitime,

Habari za majukumu?

Tafadhari naomba unifahamishe au wadau wanaotembelea blog hii ya muziki wa 'Bakulutu' wanisaidie pia, ni namna gani nitaweza kusizikiliza au kuwanazo hizo nyimbo ulizozitoa hapo kulia through 'MixPod.com'. Unajua ukishakuwa mtu wa 'Bakulutu' tena hata haya mambo yenu ya tekenologia hizi mpya yana sumbua kidogo.

Msaada wenu utadhaminiwa kwa dhati.

Mdau wa muziki wa 'Bakulutu'

Anonymous said...

Mh Kitime, wadau wakikuliza maswali basi uwasaidie kujibu! Au mpaka tuwe 'waheshimiwa fulani'?

Hapo awali nimekuuliza swali jinsi ya kupata nyimbo ulizoziweka kulia kwa blog yako! In fact, hata kusikiliza nimeshindwa! Kuuliza si UJINGA! Tell me what to do! Otherwise, if you don't need people to have/listen them then don't put them there!

Mdau wa muziki wa 'Bakulutu'.

John Mwakitime said...

Mheshmiwa kwenye blog hii wote waheshmiwa, tatizo hilo linanishangaza kiasi nimeomba kuonana na mtu mwenye ujuzi zaidi kutatua tatizo kwani kuna watu wengine wananiambia nyimbo wanazifaidi

Adbox