Nani hawa? Picha ilipigwa Dodoma 1961


Nimepigiwa simu leo na mzee mmoja akanambia amesikia kuhusu blog hii na ana kitu cha kuchangia. Kanipa picha hii ambayo pengine ni ya zamani kuliko nyingi humu ndani. Kanambia siku moja 1961 alitoroka shule ili aweze kumwona mwanamuziki ambaye alimpenda kuliko wote. Alikuwa anasoma Dodoma wakati huo, na aliweza kupata picha siku hiyo picha hii naiweka kwenu. Swali, nani anaweza kuwataja wanamuziki waliomo katika picha hii.? Wanaoimba hapo wote ni marehemu, anaepiga gitaa yu hai na picha yake ya sasa iko katika blog hii.

Comments

Anonymous said…
Mkuu,

Ni Salum Abdallah!
Anonymous said…
JM, Huyu ni Marehemu Salim Abdallah (RIP).
Anonymous said…
Huyu ni ndiye aliyekuwa nyota wa enzi za mama zetu ni marehemu Salim Abdalah,mwimbaji mwingine simkumbuki,lakini mpiga gita sina uhakika nafikiri ni Dr Ufuta

Mickey Jones
Anonymous said…
Huyu siyo Salim Abdullah?
Anonymous said…
Na bendi yake ilikuwa ikiitwa Cuban Marimba Jazz Band. Hawa walikuwa Morogoro. Salim alifariki katika ajali ya gari 1960's kama vile Mbaraka Mwinshehe 1970's. May they rest in peace. Amin.
SIMON KITURURU said…
Najiunga na waliotangulia. Huyo ni Salum Abdallah. R.I.P!
John Mwakitime said…
Wanaoimba, kushoto Juma Kilaza na kati Salum Abdallah. Kwenye gitaa Ufuta
Anonymous said…
Mkuu,

Juma Kilaza alifariki lini? Namkumbuka kwa madaha yake na ninakumbuka nyumba yake iliyokuwa imepambwa kama mabasi ya Afghanistani au Vitenge vya kina mama pale mitaa ya Kingo, Morogoro.

Mwenyezi mungu Amlaze kwa Amani. Amen.

PS/ Kwenye nyimbo ya Afrika Muye Muye nikiisikiliza kule mwishoni huwa nacheka sana. Kwa yeyote mwenye hiyo nyimbo au CD ya Ngoma Iko Huku tafadhali sikiliza ili tucheke sote mambo ya Marehemu Juma Kilaza ikiwa ni sehemu ya kumbukumbu ya jinsi alivyotufurahisha kwa namna anuai.

Popular posts from this blog

Marijani Rajabu

SITI BINTI SAAD

Western Jazz Band

Sikujua kama utabadilika - Simba wa Nyika

Mlimani Park Orchestra

Super Kamanyola ya Mwanza