Jukwaa la wapenzi wa mambo ya muziki wa Tanzania-

Breaking

Thursday, May 27, 2010

Mayaula Mayoni hatunae tena

Mayaula mayoni si jina geni kwa Watanzania. Pamoja na kuwa mwanamuziki mtunzi katika lile kundi maarufu la TP OK Jazz,chini ya Franco Luambo, Mayaula aliwahi kuwa mchezaji wa Young Africans. Mayaula alikuwa msomi mzuri wa Teknolojia ya Computer. Kwa miaka mingi karibuni alikuwa akaiishi Magomeni Mikumi Dar Es Salaam, huku akifanya kazi Ubalozi wa nchi yake hapa Tanzania.
Mayaula amefariki asubuhi ya tarehe 26 May 2010 huko Brussel Ubelgiji. Alikuwa na miaka 64. Mungu amlaze peponi pema. Sikiliza tungo yake hii akiwa na TP OK Jazz.

5 comments:

Anonymous said...

Mh Kitime, wadau wakikuliza maswali basi uwasaidie kujibu! Au mpaka tuwe 'waheshimiwa fulani'?

Hapo awali nimekuuliza swali jinsi ya kupata nyimbo ulizoziweka kulia kwa blog yako! In fact, hata kusikiliza nimeshindwa! Kuuliza si UJINGA! Tell me what to do! Otherwise, if you don't need people to have/listen them then don't put them there!

Mdau wa muziki wa 'Bakulutu'.

SIMON KITURURU said...

R.I.P!

Anonymous said...

Mimi nimeweza kusikiza wimbo huo na nyinginezo: it's simple. Je umuona huo mshale katikati ya picha? (1)Hakikisha kipaza sauti chako kiko "on". (2)Sogeza "cursor" yako kwa kutumia kipanya ("mouse") hadi kifikie kwenye mshale huo. Bofya shoto ("left-click") mara moja au mbili juu ya mshale huo. (3) Sasa tulia usikize muziki kipande hicho. Kama hukufanikiwa basi kompyuta yake in walakini: Tafahdali muone fundi wa kompyuta. Mimi mwenyewe.

Anonymous said...

Mdau (Time 09:56 uliyejitahidi kusaidia query yangu kwanza nashukuru kwa jitihada zako! Lakini nataka kukuambia sikuwa na maana hizo "nyimbo zenye picha" kwa courtesy ya 'YouTube', that's of course a straight forward to play them.

Labda kukuelewesha zaidi, nilikuwa nataka kujua jinsi ya ku-play nyimbo alizo-post Mh Kitime through 'MixPod' kulia kwa blog yake! Na kwa taarifa yako leo hata hizo nyimbo sizioni kabisa i.e 'MixPod' icon is not there!

Mdau wa 'Bakulutu'

Anonymous said...

Mdau wa 'Bakulutu'. Nimekuelewa sasa. Lazima nikiri kuwa hata mimi niljaribu kuzisikiza thru mixpod nikashindwa. Lakini kisingizio changu ni kuwa mimi ni mtu wa kizazi cha zamani. Mimi mwenyewe.

Adbox