YOUTUBE PLAYLIST

Wednesday, May 19, 2010

Magwiji wa kweli

Hawa wanamuziki kama unavyowaona wanapiga saxophone , walikuwa na mengi zaidi wanafanana walikuwa pia wanaweza kupiga vizuri vyombo vingine, japo hawakuwahi kuwa bendi moja lakini wote waliwahi kuwa katika bendi zilizorekodi muziki ambao unapendwa mpaka leo ni akina nani na walipiga vyombo gani na walipitia bendi gani?

8 comments:

  1. Anonymous14:43

    Huyu kwenye picha ya chini ni marehemu Abel Balthazar. Huyo mwingine wadau wengine wasaidie kutukumbusha.

    ReplyDelete
  2. Anonymous17:20

    Lile solo la Balthazar katika Msondo ya miaka ya 1970 lilikuwa si mchezo. Ni solo ambalo liliipa Msondo utambulisho kiasi kwamba hata ukisikia kibao cha bendi hiyo kwa mara ya kwanza unajua huo ni Msondo. RIP Abel Balthazar.

    ReplyDelete
  3. Anonymous18:37

    Sina uhakika lakini nafikiri huyu ni Shabby Mbotoni mwana Afrosa na Abel Balthazar mwana msondo
    Mickey Jones

    ReplyDelete
  4. Anonymous19:51

    Solo la Balthazar liliitambulisha Msondo kama gitaa la Luambo lilivyoitambulisha TP OK Jazz miaka hiyo. Hata leo hii, solo la Msondo bado lina mirindimo ya Balthazar, zaidi ya miaka 30 baada ya yeye kuondoka katika bendi hiyo.

    ReplyDelete
  5. Anonymous22:11

    Hapa nimeshinda mimi: Huyu wa juu ni Shabby yule wa Afro 70, na huyu wa chini bila kufuta tongotongo zangu ni Baltazar wa Nginde ambaye alikuwa Msondo enzi hizoooooooooo!

    ReplyDelete
  6. Duh, ndugu yangu Mickey Jones, kumbe wewe sio mwenzangu. Wewe ni wale wazee wa mjini ambao hawakupenda kupitwa na mambo.

    Mickey Jones, wewe ni wale wazee wanaoenda na wakati, kwa sababu kuna mambo mengi ya "kileo" unayachanganua vizuri kuliko hata vijana wa kileo tunaowategemea kutuelimisha.

    Mickey Jones, hata akina "Mtakatifu Simon Kitururu", vijana wa kisasa umewafunika.

    Mickey Jones, nimekutana na wewe kwa mara ya kwanza "Bongocelebrity". Umekuwa ukinivutia katika utoaji maoni yako yaliyoenda shule.

    Mickey Jones pamoja na Mzee John Kitime, mchango wenu kwetu sisi Watanzania ni mkubwa sana, japo kila mmoja wenu ana nafasi yake katika hilo.

    Tunawashukuru sana na tunawaomba msichoke kutuendeleza kwa kutufungua masikio kwa yale ambayo hatukuwa tunayajua zamani.

    It's Great To Be Black=Blackmannen

    ReplyDelete
  7. Anonymous09:20

    Mdau hapo juu utakuwa umepatia...nimeangalia kwa makini picha ya kwanza huyo ni kaka Shebby Mbotoni hahahahaaaaaaaaa!

    ReplyDelete
  8. Hapo ni Shabby Mbotoni na Abel Balthazar

    @BLACKMANENN: :-)

    ReplyDelete

SAFARI ZANGU NA BENDI sehemu ya kwanza.

  TANCUT ALMASI ORCHESTRA  wakiwa Jamhuri Stadium Dodoma   Sikumbuki ni safari ngapi za kimuziki nilizowahi kuzifanya hapa nchini katika m...