Jukwaa la wapenzi wa mambo ya muziki wa Tanzania-

Breaking

Thursday, May 20, 2010

Mabrothermen get together

Pamoja na yote vijana walipenda sana kuparty, kwa kila kisingizio ilitengenezwa party kulikuwa na party every week end. Unamtambua nani hapa? Kati ya hawa ni wachangiaji wakubwa wa blog hii pengine watakumbuka walikuwa wapi siku hiyo mabitozi hawa.Katika picha 'soul brother no 1' yumo. Na MJ nae ndani hahahahahaha those were the days. Wazee Maro mnamuona? Dimando huyo wa pili toka kushoto picha ya juu, mpaka leo hataki kunenepa anataka kuvaa slimfit bado.Angalia walivyovaa!!!!

13 comments:

Anonymous said...

Nawatambua wa kwanza na wa pili picha ya juu. Sema nywele za Mh.MMJ sasa hivi zimepungua (kama zetu zote sasa hivi) na wa kwanza na wa pili picha ya chini. Thnks for the nostalgia trip. Jimmy.

Anonymous said...

Wakuu,

Ubitozi was social cult ya kinamna yake. To be a bitozi one Got to know how to carry yourself; Bitozi was dandy! Bitozi got have a good taste in dressing, music, and dance. Bitozi read novels and watch movies. Bitozi had to master the arts and sciences of flirting. A bitozi was either a brilliant student or worker. Bitozi was a towering figure, you could feel the presence of the Bitozi from how the Bitozi walk, talk and appearance. No bullshitting you are either a Bitozi au Gangwe/Mtemi au Bonge la Mshamba.

Those days kulikuwa na Mabitozi,siku hizi kuna nini?

Anonymous said...

Dr kitime,

Hii ilikuwa "GET IT TOGETHER PARTY" ya kukata shoka miaka ya 70´S ilifanyika Upanga,picha ya kwanza kushoto ni balozi mhs Mohamed Juma Maharage-James Brown mwimbaji wa The Groove Makkers,wapili simkumbuki,kati DJ Dimando wa Sea View Hotel,mwisho nafikiri alikuwa Freedom Hadebe dada yake alikuwa mwimbaji wa Afro 70.
Picha ya chini kushoto Mickey Jones(mimi) aliyekaa John Noah,DJ Dimando na Danny Last.

Mickey Jones

Anonymous said...

Dk John
ahsante kwa ukumbusho Party hii ilifanyika Upanga palikuwepo marehemu Kibo Marealle,Choggy Sly,Herbert Likindo,DJ Mark Twist wa Africana Hotel Disco na kina dada warembo wengi.
Samahani nimejichanganya kidogo dada yake Freedom Hadebe
alikuwa mwimbaji wa The Rifters baadaye The Sparks na dada yake Vulli ndiye aliyekuwa mwimbaji wa The Afro 70.
brother BLACKMANN atapata jibu la starehe za vijana na wanamziki wa zamani,tulwarithi wakubwa zetu Mbaraka Mwinshehe,Salim Abdalha,Dk Ufuta na Dk John Kitime baada ya hapo ukawa mwanzo wa kizazi kipya kama The Afro 70,The Safari Trippers,The Comets,The Groove Makkers,The SunBurst,The BarKeys,The Heroes.

Mickey Jones

Anonymous said...

Wakuu,

Mabitozi were full of everyting and current with Europe, the US and everywere. Kuna siku nilikuwa Mbowe Hotel Hotel pale chini tunajimwagia lager kwa kwenda mbele na machizi wanzangu wameshuka mtembani.Babake, nipo mimi, Hashim Baharia, Muharami, Wanted, Hashim Sakalaga, Wajina wangu Castro Mmakonde na machizi wengine. Mezani tulikuwa na msitu wa pombe mezani.

Then a Bitozi came in! He was Student, Singer(Barlocks or whatsoever Band and Dj pale Mbowe Hotel).Babake alinirusha stim akishout akisema "..Leo London ni minus 9 centigrade, OOh ni baridi sana"). Wakuu, damned it, nilikuwa sijaanza kusafiri. Bitozi huyu alinirusha stim kinoma.This is to say that Mabitozi walikuwa current and up to date na New York, London, or Paris.

Ye Man! Yes Brotherman! Sail on! Duu kinaaa! Ile mbaya! Hunaa!?? Namna gani? Hiyo ilikuwa misemo ya wakati huo.

Sammy Mnkande said...

J Kitime, you are an amazing dude ! Where do you get these pics? I was one of the early Bitozi's to go abroad in 1973 so I am not in any of these pics but I remember most of the guys. By the way I just hooked up with Freedom Hadebe and Ben Mhina on facebook. Mickey nimekuona kwenye pic and I remember you well,

Much thanks and keep it coming JK, yaani I really luv this blog

Anonymous said...

Du! Hiyo profile ya mabitozi imejitosheleza, sina maswali ya nyongeza, maana nilikuwa neno hili nalisikia toka vijana wa zamani lakini hii profile imejitosheleza.

Anonymous said...

Yees naikumbuka hii party ya nguvu pale upanga, thanks for the photo
MMJ

Anonymous said...

Picha ya juu wa mwisho kulia si mwingine ni "Tonny" Edward Suma kijana machachari mdogo wakwe Col Suma alikua airwing JWTZ, Tonny akiiishi makongo akisoma Kinondoni Muslim
MMJ

Anonymous said...

Tofauti kubwa kati ya mabitozi wa zamani na machekibob wa sasa ni kuwa (1) Kulikuwa na utamaduni wa kusoma enzi za mabitozi, vitabu, magazines, magazeti, n.k. Bookshops na maktaba zilikuwa na vitabu latest (at least up to 1981) kwa hivyo "movements na trends" na falsafa za kutoka nje (k.m. Black Power, hippies, na miziki yao, yaani soul na rock) zilikuwa zinaeleweka. Sasa hivi, ujuzi wa hawa machekibob ni wa juu juu tu (superficial) ndio maana focus yao ni nyembamba mno. (2) Mabitozi walikuwa katika kile kinachoitwa "active learning" (kusoma na redio). Machekibob wako kwenye "passive learning" (tv-runinga na porojo ya watu waliokwenda ughaibuni bila hata kumaliza sekondari). (3) Enzi za mabitozi stress haikuwa kali kama sasa kwa sababu kila mtu alikuwa anajua atapata ajira, therefore uadilifu ulikuwa mkubwa zaidi. Siku hizi machekibob (generation ya watoto wetu)wako stressed out kimaisha na kwa hivyo wameukumbatia utamaduni wa "shortcuts", matokeo yake ni kugusia fani mbalimbali juu juu bila kuzama katika fani moja ("Jack of all trades and a master of none syndrome"). Hata hivyo, bahati nzuri wako vijana ambao wana focus na ambao wanataka kujifunza vitu barabara. Hao ndio watakuwa wakombozi. Mwanafalsafa wa kiti cha uvivu; ex-bitozi.

Ex-bitozi, kwa kuongezea tu, wakakti huo mabrothermeni tulikuwa tunaona fahari kubwa kuwa watanzania, regardless of your origin,faith,etc. Wakati huo tulikuwa tunawacheka wakongomani kwa kujichubua na ambi. Sikuota hat siku moja kuwa tz itakumbwa na ndwele ya mkorogo na vijana kopoteza tz pride yao. What a shame. Mwene M.

Adbox