Jukwaa la wapenzi wa mambo ya muziki wa Tanzania-

Breaking

Thursday, May 20, 2010

Choggy Sly

Nahisi najua Choggy Sly angesema nini angekuwa hai kama angejua nimeweka picha hii hapa, God he was a great guy. Pembeni yake ni mwanamuziki kutoka South Africa Vuli, aliyefanya mengi katika muziki nchini akiwa na dada yake Nini aliyekuwa akiimbia Afro70.Vuli baadae alikuwa akipiga trumpet katika kundi la Lucky Dube

7 comments:

Anonymous said...

Hilo buti la vuli ni kiboko. Kofia ya Choggy (RIP) ndio sisemi. Man, those were the days. The swinging, golden 70s.

Anonymous said...

Choggy...RIP. Ahsante mkuu kwa picha ya Vuli. Vuli 72, 73 yayari alikuwa anasikiliza na kupiga jazz. I mean the guy was really deep into music kama balozi wetu JKitime. Wakati huo musician ulikuwa huwezi ku-"fake" kama sasa: either you could play an instrument or you couldn't or you could singg or couln't...hakukuwa na half-way house. Ex-bitozi.

Anonymous said...

Wakuu,

Yah men! hii mashine Vuli ilikuwa inatwanga, inakoboa, na kusaga muziki. Hii mashine ilikuwa inaswing, tena kwa ufasaha, kwenda chombo chochote iwe vya kugonga, vya kubonyeza, vya kupapasa au vya kupuliza hali kadhalika kuimba. Mwanamuziki anayeweza kufanana naye kwa mbali ni Mabruki au Abdallah "Dullah" Mnanga au Athanas Lukindo au George Kapinga. Kama sikosei bendi yake ya mwisho kupigia akiwa Tanzania ni The Revolutions. Mabruki na Mohamedi wanaweza kutupa habari zaidi.

Choggy naye ilikuwa mashine ya kiaina yake. Kabla hajawa Dj alikuwa mwanamuziki. Ulikuwa ukienda disco na kusikiliza upangaji wake wa muziki ulikuwa unapata raha ya aina yake. He didn't care if the hit was latest or old alikuwa anasokomeza miziki kufuatana na utamu wake na muafaka na muziki utakaofuata. Choggy could talk, Choggy could joke, Choggy could amuse, Choggy could irritate, he was everything a social being could be. Surely we miss him. Marehemu Choggy Mungu Amlaze Pema Peponi. Amen.

Anonymous said...

Dk John,
Leo umenikumbusha mbali saaana kunitundikia hawa marafiki zangu
Vulli alikuwa akipiga vyombo vyote sax,piano na drums,marehemu Dj Choggy Sly alikuwepo kila Disco, huu ulikuwa ujana/ubitoz wa 70`s ahsante kwa kumbukumbu.
Mickey Jones

Mlevi said...

Bwana Kitime utuambie Chogi yuko upande gani na Vuli ndio wa upande gani.

Usi tek fo granted kwamba kila mtu anamjua Chogi Slai.

Asante

John Mwakitime said...

Kushoto ni Vuli aliyevaa kofia ya Jackson 5 ni Choggy

Mlevi said...

Asante Kitime. Sasa nimeshakufaham. Ubarikiwe sana.

Adbox