Jukwaa la wapenzi wa mambo ya muziki wa Tanzania-

Breaking

Monday, April 19, 2010

Tanzania All Stars


Ukitaka kujua umahiri wa wanamuziki enzi hizo ni vizuri ukazisikiliza nyimbo za Tanzania All Stars. Karibuni nitazitundika wote tuzisikilize, katika wimbo wa Samora, Zahir Ally Zoro aliimba Kireno, Jabali aliimba Kiarabu, Aziz Varda Kihindi we bwana wee. Haya tujikumbushe kwa kuwataja majina wote unaowaona hapo juu.

10 comments:

Anonymous said...

Ngoja nijaribu. Hapo ni marehemu Hamisi Juma (wa pili kushoto), Fresh Jumbe (wa nne kushoto), marehemu Marijani Rajab (wa pili kulia) na Muhidin Mwalimu 'Gurumo' (kulia). Yule nyuma ya Marijani kama sijakosea ni marehemu Joseph Mulenga. Wengine siwakumbuki maana siku nyingi sana zimepita tangu 1985.

Anonymous said...

Mkuu,

Nasikia raha ile mbaya!!! Nasikia raha kwa sababu wakati Mzee Mapili na Marehemu Doser wanapita kufanya recruitment walikuja Kilimanjaro Hotel walipokuwa wanaishi wanamuziki wa Tanzanites nilikuwepo.

Nakumbuka watu walipiga picha nyingi sana pale Kilimanjaro hotel nyingine chumbani na nyingine kwenye balcony. Marehemu Kizibo akavaa kanzu rasmi kupiga picha na Marehemu Doser. Sikupiga picha na mtu yoyote siku hiyo. Ningejua kama ndiyo ilikuwa ni moja ya nafasi adimu ya kufanya hivyo ningelipiga na jamaa kadhaa.

Nasikia tena raha kwa sababu siku hiyo nilikuwepo Mbowe Hotel tangu vyombo vinafungwa hadi muziki unarekodiwa! Ilikuwa ni siku ya namna yake kwa wanamuziki wa Tanzania. Naweza kufananisha halaiki ya wanamuziki wa siku hiyo na wale Marekani walipokutana kurekodi We Are The World.

Mkuu,

Ile siku ilikuwa mwisho. Ilipofika zamu ya yule Dada wa Kisouth Africa -alikuwa anaitwa Ritz kama sikosei- kuimba kwenye nyimbo ya Samora alilia. Na mimi nikastuka machozi yananitiririka. Ghani ya Kiarabu aliyoitoa Marehemu Doser nywele zilinisimama.

Ile timu ilikuwa imetimia kila safu: Vocals, Strings, Brass (ilikuwepo mpaka picollo!), Percussions, Keyboards.

Wakati shughuli inaisha nikasikia sauti nene inaunguruma nyuma yangu ikisifia kazi iliyofanyika. Kugeuka kutazama anayeunguruma nani, nakutana na one tall slim figure on his usual dark sun goggles! One of the Tanzanias' finest bass player Mr Chris Kazinduki! Nadhani hiyo ndiyo iliyokuwa mara ya mwisho kumuona au pengine mara ya mwisho ilikuwa ni pale mitaa ya Shule ya Uhuru karibu na maghorofa ya Breweries.

Is there any chance kitu kama kile kikarudiwa tena?

Anonymous said...

Naanzia kulia Chongo, Marehemu Marijani Rajabu, nyuma Max bushoke, Fresh Jumbe, nani?, Mabruki, nani?, nani?

Anonymous said...

Nianze kwa kukupongeza bro Kitime kwa kazi nzuri unayoifanya ndani ya hii blog yako. Mimi ni mpenzi wa muziki na hasa muziki huo unaouandika sana ndani ya blog hii. Ninasikitika sana kuona nyimbo hizo zinapotea na kutoweka kabisa!
Nina maswali kadhaa naomba majibu toka kwako na wadau wapenzi wa muziki huu...
Kwanza ni nani mmiliki wa nyimbo hizo hasa zile zilizorekodiwa RTD enzi hizo,
Je naweza kuzipata? bendi kama Mwenge Jazz (enzi za Benno Villa,Mabruki Mohamed,Mgoro Mohamed,Musa Bomboko, Msafiri Haroub,Luza Elias,Farahani Mzee,...mpaka Mhina Panduka...yaani 1979 mpaka 1989; Bima(magnet84,tingisha); Safari Sound(nyekesye paralizee,masantula,duku duku,ndekule,power iranda,rashkanda wasaa); Kyauri Mpakani Voice(katakata mwendo wa jongoo....pamoja na vumbi nyuma!)na nyingi nyinginezo!,
Je naweza kumilikishwa haki za nyimbo hizo?
Bro Mwakitime na wadau naomba nasaha zenu

Anonymous said...

Bw. Kitime ahsante sana, kweli unatufaa wakereketwa tulio mbali na nyumbani kwa ajili ya kubeba mabox. Asikudanganye mtu, narudia tena wasiwadanganye watu, huku nje bwana music wa bongo unapendwa sana na watu wa mataifa mengine. Marafiki zangu wakenya na mataifa mengine mpaka leo hii wanaulizia kama nina nyimbo za Mbaraka Mwinshehe, Sikinde, na baadhi ya bendi zingine. Kwa kweli muziki wetu unapendwa ila basi tu huko nyumbani mnashindwa ku-appreciate hii kitu mnabaki ku-support miziki ya kijinga kama vile fleva na mengine. Kwa kweli inasikitisha sana.

Anonymous said...

L to R: wa pili, Capt. Mabruki Mohamedi(Mwenge Jazz)

Anonymous said...

Bwana kitime nashukuru sana kwa kazi yako unayoifanya kuelimisha jamii ,nyimbo za zamani zilikuwa na ubunifu na pia bass ya miaka ya 80 ndio wacongoman leo wanaita ni bass ya ngwasuma lakini hiyo bass ilibuniwa na watanzania wenyewe walichofanya wacongo ni kuongeza speed lakini bass ya ngwasuma intokea kwenye muziki wa dansi kuanzia miaka ya 78 mpaka 80s. mimi niko uk ningependa kama kungekuwa na uwezo wa kupata waliokuwa wanmiliki bendi zaa oss,tan cut alimasi,uda jazz band ,tabora jazz,vijana jazz na dar international ,bima lee ddc mlimani ,mimi niko na studio ya mastering hapa uk ningependa kuzifanyia mastering nyimbo za zamani ili ziweze kuhifadhiwa katika hal yaya juu sababu hizo nyimbo za zamani ndio muziki wa kitanzania naomba sana hii bongo flava ni copy ya zouk na hip hop sio mziki wa tanzania nimesikia nyimbo za tancut kwa rafiki yako bwana kawele hapa uk si mchezo ningependa kama kuna uwezo na baraza la muziki tanzania tukafanya utaratibu wa kuzitowa na kusaidia jamii kuelewa nini maana ya muziki.muziki wa tanzania ni muziki wa dansi
yusef uk

Danstan said...

Bwana Kitime,

Nami naongezeka katika msururu wa kumwaga pongezi kwako. Unatukumbusha mengi, na utanogesha muziki wa kwetu.

Ila naomba kuchangia jambo tofauti kidogo hapa. Hizi taaifa unazotukumbusha zinasisimua na watu wanavyochangia inaonyesha wengine walikuwepo karibu au walishiriki katika masuala haya ya muziki. Sasa wakichangia na kujitaja wao ni nani, watuzidisha furaha zetu mara dufu kwani tutaweza kuwaliza mambo mbali mbali kwa ufafanuzi zaidi.

Kwa hiyo mchangiaji ambayo kwa mfano ni mdau husika, akiandika jina lake kata ANONYMOUS, inatupunguzia burudani sisi ambao tungependa kumuuliza zaidi ili kuboresha kumbukumbu na kupata burudani.

Natanguliza samahani kama nitakuwa nimeingilia uhuru wa watu.

Bwana kitime endelea kutupa burudani.

Anonymous said...

Marijani naweza kumfananisha na kocha wa Man United Sir Alex Ferguson. Alikuwa na uwezo wa ajabu wa kutambua vipaji. Alikuwa ni kiongozi pekee wa bendi ambaye aliweza kupiga dansi jioni hata baada ya kukimbiwa na wanamuziki wote asubuhi.

Anonymous said...

Brother . Hizo nyimbo nazitafuta sana .Zamani watu walikuwa wanajua mziki sio sasa

Adbox