Tancut almasi Orchestra enzi hizo


Tancut Almasi Orchestra, hapa wakiwa Jamhuri Stadium Dodoma. Bahati mbaya Ray, Hashim, Kalala, Zacharia wameshatangulia mbele ya haki. Kuna utata kuhusu alipo Mohamed Shaweji. Uniform zinapendeza
(Kutoka kushoto.. Ray Mlangwa, Bakari Buhero, Hashim Kasanga, Mohamed Shaweji, John Kitime, Kalala Mbwebwe, Kawelee mutimwana,Abdul Mngatwa, Kibambe Ramadhan, Zacharia daniel, Akuliake 'King Maluu' Salehe)

Comments

Danstan said…
Bwana Kitime hapo umenifurahisha. Kama wiki mbili tatu zilizopita niliwahi kuchangangia hoja hapa na nikazungumzia TANCUT na uniform zao zilivyopendeza. Wakati huo mkipiga uwanja wa Jamhuri. siku za jumapili mnapokuwa safarini Dodoma. Nilikuwa nasoma Mazengo lakini nilikuwa natoroka na kuja kuwaoneni hadi mwisho wa onyesho.
Nami swali langu siku zote lilikuwa yuko wapi Mohammed Shaweji? Maana sauti yake ilikuwa burudani sana.
Anonymous said…
Mkuu,

Nimekutumia ujumbe kuhusu Hashim naomba usiuchapishe nilichanganya habari. Kuna Hashim na Kulwa walikuwa blowers waliotokea kwa Father Canute. Kulwa alipita Vijana na baadaye nilimuona Ndekule. Hashim alikwenda Magereza Kiwira na baadaye alikuja Dar akazunguka bendi kadhaa. Akapotea baada ya blowing section kupotea katika bendi zetu za kisasa.
Anonymous said…
Mkuu,

Asante sana kwa kuliafiki ombi langu na kwa maelezo kuhusu Kulwa Milonge.

Marehemu Father Canute alizalisha blowers wengi sana. Katika Product zake yupo mpuliza trumpet ambaye alienda mpaka Simba Wanyika na baadaye Tanzanites. Mara ya mwisho nilimuona miaka ya mwanzoni mwa 90 pale TAZARA club tukaongea lakini sikumuuliza alikuwa na bendi gani kwa wakati huo.
Anonymous said…
Miaka michache iliyopita nilikuwa na taarifa kuwa Mohamed Shaweji yupo Nairobi. Hiyo ni kama miaka mitano nyuma. Kwa sasa sina habari zake, sijui wadau wengine.
Anonymous said…
Mkuu,

Nakunukuu:

"..Huyu Hashim Kasanga wa Tancut hajawahi kupiga blowing, alijaribu kujifunza wakati tuko wote TX Seleleka akaacha. Aliacha muziki akaokoka na kubadili jina na dini na Kuitwa Abraham akaajiliwa kama mlinzi, akauwawa na majambazi waliokuja kuiba katika petrol station aliyokuwa akilinda..."

Masikini mja huyu kwa maelezo niliyonukuu napata picha alihangaika na wakautoa uhai wake katika aina ya kuhuzunisha sana. Pamoja na yote nina imani amepumzika kwa amani. Amen.

Popular posts from this blog

Marijani Rajabu

SITI BINTI SAAD

Western Jazz Band

Sikujua kama utabadilika - Simba wa Nyika

Mlimani Park Orchestra

Super Kamanyola ya Mwanza