Jukwaa la wapenzi wa mambo ya muziki wa Tanzania-

Breaking

Tuesday, April 13, 2010

Sokomokoooooooooo


Leo nimeona nianze kuanika picha nilizonazo hadharani , tukumbuke yalivyokuwa. Pichani ni Safari Trippers. Wapenzi wa Sokomoko mnakumbuka kipindi hiki. Hebu tupeane kumbukumbu

15 comments:

Anonymous said...

Kweli Mze Kitime wewe si mtu. Yaani hapa umenitoa mbali sana, yaani wewe sijuwi nikuambiaje. Duh lete mambo mzalendo mwenzetu.

BLACKMANNEN said...

Mzee Mwakitime,

Mimi ni mpenzi mkubwa sana wa miziki ya zamani. Nakupongeza sana kwa kutuletea kitu hiki Mtandaoni.

Nitakuwa nikikusumbua kila mara kwa maswali na maombi ya miziki ya zamani.

Juzi nilimwona pia Mzee Madaraka Nyerere katika Wavuti yake ya "muhunda.blogspot .com" akionyesha Wavuti ambazo huzitembelea, hii ikiwa ni mojawapo.

Bila ya kusubiri nilimtwanga ombi la kunieleza historia ya Bendi ya Mara Jazz "Wanasensera", chini ya aliyekuwa kiongozi wao Juma Nguzo.

Madaraka amenishauri nikutwange wewe ombi hilo, na pengine naweza kupata hata santuri au kanda za Wanasensera zikiwemo nyimbo za "Kitenge" au "Dada Chausiku". Niko tayari kuzinunua kwa bei yoyote.

This Is Black=Blackmannen

Anonymous said...

Kaka Kitime hapo namuona Chris Kazinduki huyo najua yuko mbele ya haki,hivi David Godon yuko wapi?naikumbuka sana ile nyumba yao pale Changombe.

Baraka Mfunguo said...

Viiiicky mtoto wa mamaaa mbona sasa umeadimika! Marijani Rajabu acha bana.

kipupwe said...

kwa kweli siku wepo ila kila nikisikiliza miziki yao inanikumbusha marehemu baba yangu

Anonymous said...

Mkuu,

Ngoja nianza kwa mtindo wako " jina lake ni Marijani Rajabu siyo Marijani Shabani. Shabani Marijani alikuwa ni kocha wa kandanda na Marijani Rajabu alikuwa mwanamuziki" Mara ya mwisho kumsikia Kocha Marijani ilikuwa ni katika miaka ya mwishoni mwa 70 au mwanzoni mwa 80 wakati FAT ya kina Said El-Maamry ilipotaka kutapeli kombe la Afrika kwa kuunda timu ya kitapeli ya Dar Rangers International. Sijui Kocha Marijani aliishia wapi?

Turudi kwenye Sokomokooooo!!!! Mwaka 1985 nilinunua kanda kadhaa za Safari Trippers pale Dar es Salaam Music Centre. Mwaka 1989 nilipita Tanga kutalii. Nilipokuwa navinjari mitaani nikapita kwenye duka la Muhindi mmoja Gulamabas J Ismailjee lililokuwa linauza kaseti.

Nilipoanza kuangalia zile kanda macho yaliniyoka na moyo kuanza kunidunda mpaka yule mwenzangu niliyekuwa naye akastuka na kuniuliza kama nipo ok.

Palikuwa na kanda za Bi Shakira na Lucky Stars Viva Frelimo na Zinginezo. Palikuwa na Frank na Dada Zake. Pia palikuwepo na Safari Trippers!

Niligeuka na kuwa kama mtoto mdogo aliyeingia kwenye duka la lawalawa huku ana pesa! Nilizinunua kanda zote nilizoziona ni nzuri kwangu. Nikamlipa yule Muhindi hata bila ya kumuomba anipunguzie bei.

Mwaka 2009 nikapata fursa ya kuzihamisha baadhi ya kanda zikiwemo za Safari Trippers toka kwenye kanda kwenda kwenye CD. Aliyenihamishia ni retired sound engineer mmoja mkali sana. Basi yule Mzee akakarabati pale palipokuwa na mushikeli na kuzi'remaster'. Baadaye nikazihamisha kuziingiza kwenye Ipod yangu.

Nimesikiliza miziki ya Trippers mara kadha na kuzisanifu. Mkuu, nilichokisikia humo na kukisanifu, ukisema "..Ehee!?.." Nitakueleza.

John Mwakitime said...

Eheee

Anonymous said...

Mkuu,

M'mhuu, jasti imejini jamani yaani unasikiliza remastered ya:
-Mkuki Moyoni
-Roza Nenda Shule
-Usiache Mbachao
-Wenye Nguvu
-Nasikia Maneno
-Georgina
-Rafiki Si Mtu Mwema
-Sauti Yako Nyororo
-Kucheka na Furaha
-Arusi

Kama haitoshi unaendelea kusikiliza
-Sokomoko Ndani ya Nyumba
-Nyerere wa Tanzania
-Mkanye Mwana (Baba Rukia)
-Hanifa
-Wazalendo
-Sikutegemea Kupatwa na Matatizo
-Heshima ya Mtu Kufanya kazi
-Matinda Lea Mwanao
-Salama
-Jirekebishe
-Hebu Niambie
-Shani
-Tazama Wewe Mary
-Tukacheze Sokomoko
-Enyi Ndugu wa Mtoto

Jasti imejini unazisikia hizo nyimbo zikiwa remastered baada ya miaka takribani thelathini na ushehe au arobaini toka kwenye Ipod kupitia earphones za Sennheiser PX 100!? Kama siyo kujitafutia ugonjwa wazimu utakuwa unatafuta nini?

Unazisikiliza kwa karibu sana halafu unasawiri Dar ya 1974 hadi 1979. Halafu unakumbuka Ford Transporter moja lililokuwa linabeba wanamuziki. Unakumbuka Taksi ya Safari na Muziki ya Barafaa na Magoma. Unakumbuka Princess Bar mitaa ya Mchafukoge pale Ofisi za NUTA Mnazi Mmoja.

Unawakumbuka baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki. Unasikia furaha halafu unasikia uchungu kwamba kile unachokisikiliza hakipo tena na baadhi ya wale waliokiunda wametangulia mbele ya haki. Unawakumbuka baadhi yao ambao ulizoeana nao. Unakumbuka siku za mwisho ulipowaona baadhi yao wakiwa siyo tena wale waliokuwa wakati ule. Unawaombea dua kwa Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema Awarehemu kwa Amani. Amen.

Huishii hapo. Unasikiliza na kuisanifu ile miziki na kuifanyia tathimini. Unasema nitaielezea tathimini ya miziki hii kwa jinsi nilivyoielewa halafu nisikie maoni ya wadau wengine.

Mkuu, hapo ndipo nilipotamatikia. Asante.

PS/Mwaka 2007 nilinunua CD moja inaitwa The Great East African Trip kwenye CD 1 ya hiyo compilation ndiyo nilipopata kuisikia Georgina orijino iliyokuwa Digitally remastered. Niliisikiliza hiyo nyimbo mara mia kidogo.

Patrick Tsere said...

John!!!Phew!!Huyo jamaa maelezo yake hata mimi yamenisafirisha mbali. Wafaransa wanasema c'est la vie yaani haya ndiyo maisha.Lakini miziki ya zamani mimi binafsi hunipa raha sana. Actually I become nostalgic. Lo!!Haya bwana.

John Mwakitime said...

Niwe mkweli raha sana blog hii, unakumbushwa enzi za raha na ujana na loh enzi za kusindikiza wasichana bila kujali matope ya Frelimo, huku roho yako ikisuuzika, na enzi ya kuandika maneno ya nyimbo kama mkuki moyoni na kumpelekea mpenzi wako, nae anaona umemthamini sana. Leo unapeleka kwanza Blackberry na unaweza ukatupiwa usoni pia hahahaha

WIM said...

Nakumbuka enzi hizo nikiwa likizo kutoka Mkwawa High School ilikuwa lazima kwenda 'boogie' za Sokomoko pale Princess Bar. Those were the days. Asante sana.

Anonymous said...

Bw. Kitime unda bendi yako. Ahsante sana kwa utoaji habari wako!

ismail fundikira said...

DUH HUYO JAMAA HAPO JUU NI KIBOKO YAANI KANIRUDISHA MBALI SANA! NAKUMBUKA ENZI HIZO NILIKUWA NAIMBA HIZO NYIMBO MTAANI KABLA HAZIJATOKA REDIONI. NAKUMBUKA SIKU MOJA MADI TUMBO ALILIA WAKATI AMEACHIWA ATAMBE NA RYTHM YA BABA RUKIA MPAKA MARIJANI ILIBIDI ASAVE MAANA ALISHIDWA KUENDELEA SIJUI KWA NINI? kama kuna mdau aisaidie maana bado najiuliza! sijui mdadi ulipitiliza!!!!

Anonymous said...


...Ismail, wewe nahisi utakuwa ni miongoni mwa lile kundi la watoto nikiwemo na mimi waliokuwa wanasoma Chang'ombe PSkul ambao tulikuwa tukitoka shule tunapitia nyumba fulani pale Chang'ombe ambako Trippers walikuwa wanachukulia mazoezi karibu na akina Simkoko na tukaanza kuimba nyimbo za Roza nenda shule na Georgina hata kabla hazijarekodiwa Studio...!!

Anonymous said...

Rest in peace DAVID GORDON...

Adbox