Jukwaa la wapenzi wa mambo ya muziki wa Tanzania-

Breaking

Saturday, April 17, 2010

Orchestra Fuka Fuka

Kuna mdau aliomba azione picha za bendi ya Fuka fuka,hapa ni picha zilizotangaza ujio wa Bendi hii ambayo ilitokana na Orchestra Kamale ya Kongo. Haikukaa Tanzania muda mrefu lakini ndio iliyomleta mwanamuziki Tchimanga Assossa ambaye ameamua kuishi Tanzania toka wakati huo

7 comments:

Anonymous said...

Bw. Kitime ahsante sana kwa kazi yako. nakushukuru tena kwa kunipostia hizi picha za FukaFuka. Vipi picha zako wewe pamoja na Sagha Rhumba? Hizi picha bwana nazikuza na kuweka ukutani kwangu kwani mie ni shabiki wa kutupwa wa muziki wa TZ, niko huku China kwa hiyo naboreka kwa kukosa uhondo wa zamani na wa sasa. Nafuatilia sana muziki wa nyumbani na ndiyo niupigayo kwenye cd zangu, sipendi muziki wa aina yeyote ila wa bongo dansi tu. Na wala sikibaliani nawe kuwa muziki wa dansi eti umekufa, muziki wetu ni mzuri sana ila vijana wa sasa wanamakusidi yao ya kutaka kuuua. Ahsante sana Bw. Kitime na Mungu akulinde.

Anonymous said...

Duh bw. kitime naona sasa wewe inabidi uwe balozi wetu kwetu wakereketwa wa muziki wa dansi. Aisee unatukumbusha mbali mno, sina cha kukupa ila natoa shukrani tena, ahsante sana.

Anonymous said...

hivi hawa fukafuka walikuja nchini mwaka gani, na hizi picha ilikuwa wakati wamekuja ama? Kingine, unataka kuniambia fukafuka ilifia tanzania? maana nakumbuka huyu jamaa mpiga solo wao kizunga alikuwa makassy kipindi kile makassy ilipokuja upya baada ya kina remmy, bati osenga, zagalo, fanfan, singa wa singa, albert tumba, kuhamia matimila.

Anonymous said...

Mkuu,

Ukirejea kwenye mada ya nyuma ya Tchimanga Assossa nilidokeza kwamba alikuja na Le Kamale na kuwa nakumbuka picha yao wakati walipokuja ukanisahihisha kwamba alikuja na Fuka Fuka.

Naona katika picha wameandika Fuka Fuka. Ex Kamale. Kumbukumbu yangu haikuwa imekosea sana. Au siyo?

Mwaka huo ulikuwa mwaka wa vijimambo kweli kweli. Kama nakumbuka vizuri ndiyo mwaka wa mabondia wetu kina Emmanuel Mlundwa, Mike Hatia, Lucas Msomba, Gerald Isack, Aloyce Nuti, Mabushi walipofanya vizuri sana kule Algiers, Algeria. Au siyo?

Anonymous said...

Mdau,
kweli kama kukosea ulikosea kidogo, kwani Fuka Fuka ni bendi iliyokuja kuundwa na kina Mulembu Mule Mule, Assossa, na kamanda wao Kizunga Ricos baada ya kutokea mtafaruku kule Les Kamale. Les Kamale ilikuwa inaongozwa na Nyboma wakati Mulembu akiwa msaidizi na ilikuwa chini ya usimamizi wa Veve Kiamangwana. Then Mulembu akashauri wenzake kina Assossa watoke kwani Kiamangwana alikuwa na mapenzi kwa Nyboma zaidi wakati nyimbo nyingi ama tuseme nzito za Les Kamale zilitungwa na Assosa (Masuwa), na Mulembu kama (Ayidjo), (Ngali ama sie tunauita Selebonge), n.k. Baada ya kutengana nayo Les kamale ikapoteza muelekeo wake na kufilia mbali. Nayo Fuka Fuka ikaja kufa kimiujiza baada ya wanamuziki wake kutawanyika hapa na pale. Mie nipo hapa Kinshasa. huku muziki wetu wa dansi wanaupenda watu ila hawawajuwi wanamuziki wetu. Napelekaga sana cd za muziki wetu kwenye party za kishikaji na watu wanaselebuka ile mbaya kwani unaleta radha tofauti sana na wa kwao.

Anonymous said...

Kitime wewe ni mwisho. Sikutegemea maishani mwangu kana ningekuja kuona picha ya huyu jamaa Kinzunga Ricos. Huyo jamaa alikuwa na kipaji cha hali ya juu sana cha kucheza na nyuzi za solo enzi hicho za 'makavasha' (cavacha). Alikuwa akichuana vikali na wakali wengine wa solo wa kavasha kama Djuke (Orchestre Kiam) na akina Mongoley na Lusuama Aspro wa Lipua Lipua. Big up sana!

Anonymous said...

Balozi Kitime uko juu. Tuletee mavituzz balozi wetu.

Adbox