YOUTUBE PLAYLIST

Sunday, April 25, 2010

Mzee Joseph Nyerere


Mzee Joseph Nyerere alikuwa mpenzi sana wa Vijana Jazz Band. Nakumbuka siku za Jumapili ambapo Bendi ilikuwa na onyesho lake lililoitwa Vijana Day mara nyingi ungemkuta pembeni akisikiliza muziki na pengine akiomba special request. Ilikuwa ni burudani pale ambapo aliamua siku hiyo kucheza maana alikuwa na staili ya peke yake iliyofanya mtu apende kumuangalia. Historia inasema alisoma Tabora Boys na alikuwa Band Master wa bendi ya shule na alipendwa sana kutokana na mbwembwe zake alipokuwa akiongoza na kifimbo cha Band Leader. Mzee Joseph aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa TANU Youth League. Pichani akiwa jukwaani na Marehemu Hemedi Maneti katika Ukumbi wa Vijana Kinondoni, kwa mbali nyuma anaonekana Aggrey Ndumbalo akiwa ameshika gitaa na Said Hamisi muimbaji wa Vijana akiwa napiga makofi, wote wamekwisha tangulia mbele ya haki.

7 comments:

  1. Anonymous11:53

    Yaani wote uliowataja wametangulia mbele za haki, najua Joseph Nyerere na Maneti sikua Aggrey Ndumbalo na Saidi Hamisi pia.

    Hivi Said Hamisi si ndio alikuwa anaweza kuiga vizuri sauti ya Maneti?

    RIP Hamisi Saidi aka Misukosuko!

    ReplyDelete
  2. Ndiye huyo haswa misukosuko

    ReplyDelete
  3. Anonymous00:30

    Hivi Balozi, ulitoka lini Vijana Jazz?

    ReplyDelete
  4. Niliacha Vijana Jazz mwaka 1995

    ReplyDelete
  5. Anonymous08:35

    BW.KITIME,NAOMBA KUULIZA. HIVI ULE WIMBO WA VIJANA 'MAANA YA TANGA'....TANGA NI LA MSIBA ..AU KUTANGATANGA. NANI HASA ALIYEANZA KUUPIGA? KWANI KUNA WIMBO EXACTLY KAMA HUO ILA KWA KILINGALA, ULIOPIGWA NA ORCHESTRE VEVE, BENDI YA YULE MTAALAM WA KUPULIZA SAX, VERKEYS KIAMUANGANA MATETA!!

    ReplyDelete
  6. Kwa kweli nimeshasahau hata melody ya wimbo huo wa Tanga ngoja niusikilize. Huo wimbo wa Verckys unaitwaje?

    ReplyDelete
  7. Anonymous09:25

    JINA LA WIMBO WA VERKEYS LIMENITOKA KIDOGO...NITAJARIBU KUWASILIANA NA NDUGU YANGU ALIYEKO MWANZA YEYE ANAYO HIYO ALBUM YA VERKEYS YENYE HUO WIMBO..

    ReplyDelete

SAFARI ZANGU NA BENDI sehemu ya kwanza.

  TANCUT ALMASI ORCHESTRA  wakiwa Jamhuri Stadium Dodoma   Sikumbuki ni safari ngapi za kimuziki nilizowahi kuzifanya hapa nchini katika m...