YOUTUBE PLAYLIST

Wednesday, April 7, 2010

Kwaya

Kwaya, kama neno lenyewe linavyoonekana ni neno la mapokeo likimaananisha aina ya utamaduni wa mapokeo. Ni neno lililotokana na neno 'choir'. Uimbaji wa kikundi cha watu. Muziki huu umepitia mabadiliko mengi yakitokana na sababu mbalimbali. Kwaya ilikuweko mwanzoni katika mashule na katika makanisa, baadae ikawa sehemu ya burudani hasa ikipata msukumo kutoka kwaya za Kusini mwa Afrika. Kwa wale waliokuwa maskauti wanakumbuka kuwa kwaya kilikuwa kipengele muhimu katika route march. Katika harakati za kutafuta uhuru kwaya zilichukua umuhimu sana katika kuhamasisha jamii. Lakini kama ilivyo kwenye muziki wa aina nyingine, muziki huu ulitokea kuwa na mabingwa wake. Si rahisi kumsahau Mzee Makongoro kama uliwahi kumsikia. Alikuwa na nini cha ziada? Mzee huyu alianzisha staili yake mwenyewe ya kwaya. Wakati kwaya nyingi zikiiga muziki wa Jiving wa South Africa yeye alikuja na kitu kipya ambacho bahati mbaya kimekosa mrithi. Karibuni tuliangalie hili swala la kwaya. Je tunaelekea wapi?

7 comments:

  1. Anonymous10:24

    Mkuu,

    Kuleni kuku, mayai, mboga, samaki, maziwa
    Na kujenga nyumba safi pa kulala pawe bora!

    Nyingine:

    Dereva kalewa pombe! haa! Sawa hiyo!?
    Haataa, hiyo si sawa dereva wacha vituko!

    Hizi ndizo beti za nyimbo za kwaya ya Makongoro ninazozikumbuka. Kulikuwa na Makongoro na mwingine jina lake nimelisahau walikuwa na mtindo wa uimbaji unaofanana.

    Ile ya Marehemu Mzee Mwinamila Hiari ya Moyo nayo tunaweza kuiweka katika kundi la Kwaya?

    Halafu kuna vikundi vya Wagogo vya kina baba na kina mama na mchanganyiko wa kina baba na kina mama nao huimba unison/pamoja (maneno mengine ya kimuziki magumu kuyapata kwa Kiswahili)wale nao tunaweza kuwaweka katika mtindo wa Kwaya? Halafu kuna waimbaji wa makundi/kwaya wa Kisukuma, Kimasai, Kinyamwezi, Kichaga na wengineo. Wale pia tunaweza kuwaweka katika mtindo wa Kwaya?

    Kuna CD fulani zinaitwa Tanzania: Chants Wagogo/Wagogo Songs. Nyingine Tanzania: Music of the Sukuma Composers of Sukumaland. Na nyingine inaitwa Tanzania Vocals, Tanganyika 1950 Gogo, Nyamwezi, Sukuma , Chagga, Maasai. Hizi CD zina waimbaji wa kimakundi/kwaya wa kiasili kabisa. Nyimbo zilizomo kwenye hizi CD zinawezakuwa chachu nzuri sana ya mjadala huu.

    ReplyDelete
  2. Anony 12:24
    Mkuu hizo CDs za nyimbo za makabila zinapatikana wapi?

    ReplyDelete
  3. Nimejaribu kuangalia kwenye soko la Amazon nimezikuta baadhi. Jambo jingine ambali linajitokeza ni hilo la kuonekana kuwa kulikuwa na kwaya za kiasili, kitu ambacho linaletaleta changamoto ya mjadala katika mada hii. Nadhani changamoto inaweza kuwa kama ilivyo katika neno muziki. Hili ni neno ambalo chanzo chake ni neno la Kijerumani. Swali ni kwa kuwa hatuna neno la kiasili likiwa sawa na maana muziki, je kulikuwa hakuna muziki kabla ya Wajerumani? Hali ilikuwaje?

    ReplyDelete
  4. Anonymous18:08

    Mkuu Faustine,

    Hizi CD zinapatikana kwenye maduka makubwa ya rekodi haswa mitaa ya Ulaya na Amerika. Pia unaweza kununua kutoka mitandaoni kama alivyokuelezea Mkuu kwenye soko la www.amazon.com au www.sternsmusic.com

    Sternsmusic ni moto mara moja. Ukiorder wanakufikishia mzigo wako within 5 days. Wapo London pale kwenye kituo cha underground cha Warren Street. Amazon huwa wanachukua muda kidogo kama upo nje ya eneo lao kama Afrika, Marekani, Ulaya, au Australia.

    Mkuu,

    Mjadala wa Kwaya unaanza kukolea. Nikiwasikiliza Ladysmith Black Mambazo na nikiwasikiliza waimbaji wa Kimasai au wa Kigogo ninapata tofauti mbili kubwa kwamba Ladysmith Black Mambazo walikuwa wanaimba kwa Kizulu na wakati mwingine Kiingereza lakini Wagogo na Waamasai wao wanaimba kwa Kimasau au Kigogo tu. Tofauti ya pili Ladysmith Black Mambazo walilijua soko na kwa hivyo walijipanga kibiashara zaidi ya ya Wamasai au Wagogo ambao kwaya zao ni kwa ajili ya shughuli za kijamii yao zaidi kuliko biashara.

    ReplyDelete
  5. Kuna kitu umegusia ambacho ni kiini kizuri cha majadiliano. Wagogo na wamasai wanaimba kwa ajili ya shughuli za kijamaii...... kama nilivyogusia hapo juu, makabila yetu hayakuwa na neno linaloweza kutafsiri muziki, na hivyo kuchukua neno la Kijerumani muziki, tatizo si kuwa hawakuwa na muziki, bali kwao muziki ulikuwa na maana nyingine kabisa. Kwa ujumla tunaweza kusema walikuwa na 'ngoma'. Ngoma ilikuwa na maana nyingi. Chombo cha muziki...ngoma za mashetani..ngoma za mavuno, msiba, na kadhalika, zilikuwa na maana zaidi ya kusikiliza tu kwa ajili ya burudani kama ilivyo sasa, ndio maana unasema Black Mambazo wamekaa kibiashara zaidi. Kuna tofauti nyingine ya kiutaalamu wa muziki, scale wanazoimbia Black Mambazo ni tofauti kabisa na za Wagogo na Wamasai, kwetu tuliopata uonjo wa mfumo wa kwaya za kizungu akili inawahi kututuma tuone kwaya ya Black Mambazo inauzika zaidi. Karibu

    ReplyDelete
  6. Blackmannen03:58

    Nyimbo za zamani zilisheheni Mashairi na misemo ya kiswahili sio kama ilivyo sasa.

    Kwa mfano Mzee Makongoro katika wimbo wake wa "Madereva", alianza hivi....."Mtikisiko wa Wimbi, Maji Ya Kipwa Kimbia, Ukimsifu Mgema Tembo Atalitia Maji....Madereva wenye fujo yafaa kuwakimbia".

    Mtu unaburudika kwa wimbo na hapo hapo unajifunza kitu, kama sio lugha.

    This Is Black=Blackmannen

    ReplyDelete
  7. John Kitime, eh! Maneno sina kutathmini namna unavyofanya kazi nzuri kusaidia kutoa picha ya historia na fani ya muziki wa Tanzania. Kazi hii ingehitaji kufanywa muda mwingi na vyombo vya habari, lakini wapi. Wasomi? Wapi. Hongera sana kaka. Hatua itakayofuata ni kuweka hii hii blogu katika fani mbalimbali za sinema, vitabu na kadhalika kusudi vizazi vijavyo vifaidi. Niliwahi kukuandikia barua pepe lakini sijui kama uliipata?

    ReplyDelete

SAFARI ZANGU NA BENDI sehemu ya kwanza.

  TANCUT ALMASI ORCHESTRA  wakiwa Jamhuri Stadium Dodoma   Sikumbuki ni safari ngapi za kimuziki nilizowahi kuzifanya hapa nchini katika m...