The Jets


Hawa ndio The Jets (1972), ambao baadae walikuja kuwa STC Jazz, ambayo ndio chanzo cha Biashara Jazz. Waliopo hapa wa kwanza Belino, Raphael Sabuni, Mgoro katika moja ya maonyesho yao. Marijanio Rajab alijiunga na kundi hili, na kuimba wimbo kama.... Ilikuwa usiku wa manane.

Comments

Anonymous said…
John
Mgoro unaemzungumzia hapo kwenye picha ni huyu mgoro mohamed full power wa bendi za jeshi?
Anonymous said…
Nakumbuka kabisa enzi za The Jets ingawaje ni miaka mingi imepita lakini bado tunawakumbuka
Kama kuna yeyote anayefahamu Belino,Rafael na Garrick Sabuni mdogo wa Rafael,ambaye alikuwa kundi moja na mimi "The Heroes" ningependa kujuwa walipo kwa sasa.

Mickey Jones
Denmark
Anonymous said…
BW.KITIME NAOMBA NIKUSUMBUE, HIVI MGORO MOHAMED BADO YUKO MWENGE? AU ILE BENDI NYINGINE YA JESHI, ANGA
John Mwakitime said…
Amekwisha staafu jeshi , japo anaendelea na muziki. Nitamtafuta atueleze yu wapi
John Mwakitime said…
Mickey Belino alishatangulia mbele ya haki miaka mingi, kabla ya mauti yake alipata bahati mbaya ya kukutwa na bunduki iliyotumika katika ujambazi nyumbani kwake na kosa hilo lilimsababishia kifungo.
Anonymous said…
Nasikitika kukuarifu kuwa nilisikia kutoka kwa rafiki yangu mmoja aliye Arusha kuwa Bro Raphael pia alifariki mwaka jana au mwaka juzi Nairobi na kuzikwa Arusha. pia aliniambia kuwa kina Gabriel, Cuthbert na Charlie wako Arusha na John yuko Mtwara (if I am not mistaken).

Popular posts from this blog

Marijani Rajabu

SITI BINTI SAAD

Western Jazz Band

Sikujua kama utabadilika - Simba wa Nyika

Mlimani Park Orchestra

Super Kamanyola ya Mwanza