Hayawi hayawi.........

Hatimae inataka kuwa. Kama ambavyo wapenzi wengi wa Blog hii wamekuwa wanaomba,mwanga umeanza kuonekana kuwa itawezekana. Wenye afro zao wazitimue au wakachome tena nywele hahahaha, wenye raizon zao, wenye slimfit zao,(kama zitawatosha na hivyo vitambi), wenye superfly, pekos, maxi, midi, mini wazitoe vumbi maana wanamuziki wa zamani wameamua kuwa watafanya show moja kubwa ambapo wanamuziki wa toka enzi za buggy watapanda tena stejeni na kujikumbusha yalivyokuwa. Onyesho hilo ambalo pia litahusisha Madjs wa enzi hizo linategemea kufanyika mwezi July. Tayari Kilimanjaro bendi wametoa vyombo na eneo la mazoezi na wanamuziki kadhaa wamekwisha jitokeza kukubali kushiriki. Fuatilia katika blog hii upate kujua nani na nani watakuwepo. Mapato ya onyesho hilo yataenda kwenye huduma ambayo itatajwa baada ya siku chache.

Comments

Hatimaye.
Asanteni kwa hili. Naamini hii ni hatua ya kwanza katika kile ambacho wapenzi wa MUZIKI HALISI tumekuwa "tukililia" kwa mda mrefu.
Natumai hatua itakayofuata itahusisha KUWAENZI wasanii wengi walioifikisha sanaa ya muziki hapa ilipo na ambao wanaanza kusahaulika kwa kuwa tu hawakumbukwi na jamii.
Niliwahi andika kuwa NATAMANI KUONA SIKU YA MUZIKI WA DANSI NCHINI ambao utaenzi watu hawa na kazi zao. Kisha kuona HALL OF FAME wa muziki wa Dansi na wakithaminiwa vema
(http://changamotoyetu.blogspot.com/2010/02/natamani-kuona.html)

Natamani kuona siku hizi
Anonymous said…
Mkuu,

Naomba utoe ruhusu wadau watoe listi ya magwiji waifikiriayo kuwemo katika zoezi hili. Unasemaje?
John Mwakitime said…
Toa mapendekezo
Anonymous said…
Mkuu,

Kwa heshima na taadhima naomba urejeshe hii mada kuleni mwanzoni na utoe ruksa kwa wadau kuanza kutoa mapendekezo. Asante.

Popular posts from this blog

Marijani Rajabu

SITI BINTI SAAD

Western Jazz Band

Sikujua kama utabadilika - Simba wa Nyika

Mlimani Park Orchestra

Super Kamanyola ya Mwanza