Jukwaa la wapenzi wa mambo ya muziki wa Tanzania-

Breaking

Tuesday, April 27, 2010

The Dynamites

Kikundi kingine toka enzi za miaka ya 69/70 hawa waliitwa The Dynamites. Hapa kwa kweli namtambua Salim Willis tu ambaye baadae alikuja kuwa mpiga second solo wa Afro70.

8 comments:

Anonymous said...

John,

mwishoni mwaka 69 na mwanzoni 70`s Dynamites walikuwepo walitikisa miji mingi,lakini kama ujuwavyo miaka ile ingawaje tulikuwa na vipaji vya kuzaliwa wengi katika fani ya mziki wa Tanzania,kulikuwepo na matatizo ya band nyingi kutokuwa na uwezo wa vyombo vya mziki ni band chache zilikuwa na vyombo nyingi za wakongo,Salim Willis alijiunga Afro 70 na wengine wakajiunga bendi zingine.

kujibu swali ulioulizwa:

Hauyo aliyekuuliza amekumbuka sawa kabisa,mimi nilikuwa meneja msaidizi katika bwawa la maofisa wa Polisi(POLICE OFFICER`S MESS)
Oysterbay/masaki.
Baba wa Taifa Mwl J.K.Nyerere na hayati Abeid Karume na mzee Rashid M. Kawawa walilifungua katika sherehe iliyofikia kileleni kwa maofisa wetu wa polisi.
Sisi tulipelekwa kulianzisha tulitokea wizara ya utalii wakati ule nilikuwa front office adminstration New Africa Hotel mara tuu baada ya kumaliza masomo ya utalii,nikiwepo New Africa Hotel na Police Oficers Mess nilibahatika kupata nafasi ya kuwa karibu na wanamziki wengi kutoka band tofauti starehe za zamani zilikuwa mahotelini kwa watalii.
Niliondoka nchini 1977 mpaka sasa bado nipo Scandinavien.

Mickey Jones
OLD BOYS-GENARATION OF 70`s

Patrick Tsere said...

Namkumbuka Otis "Hey Jude dont make it bad take your...and make it better, remember....

John Mwakitime said...

Mkuu Hey Jude ulikuwa wimbo wa Beatles, lakini katika kipindi cha Soul, Wilson Picket nae alitoa version yake

Sammy Mnkande said...

Huyo ambaye ame kneel down kulia ni Abdul Abubakar. Tulisoma wote Forodhani

Anonymous said...

Je, aliyesimama wa pili kulia ni Bashir aliyekuwa Sunbursts???

Patrick Tsere said...

John yeah ur right ulikuwa Beatles. Nimeuchanganya na "Direct Me".

Anonymous said...

Katika hawa Dynamites alikuwemo pia Cyril Kabarole alisoma Saint Josephs sasa Forodhani akiimba na kupiga rhythim, Mohamed Nyamka akipiga bass, Godfrey Manoni pia wa Saint Josephs akiimba
Mohamed Maharage Juma

Anonymous said...

Wakuu,

Mpaka mwishoni mwa miaka ya 70 ilikuwa bado ni rahisi kwenda muziki na kuwakuta wanafunzi wa shule za sekondari na wachache wengine wa shule za msingi wakiwa wapigaji.

Siku hizi siyo rahisi kukuta wanafunzi wa sekondari au vyuo wakiwa wanamuziki. Kuna maswali mawili ambayo yamenijia:

Swali la Kwanza, nini kilichokuwa kinawafanya wanafunzi wa miaka ya 60 na 70 kuweza kuwa wanamuziki?

Swali la Pili, kilitokea nini katika miaka ya 80 na kuendelea hata wanafunzi wakatoweka katika anga za muziki? Naomba katika hili swali la pili nifanunue ninaposema wanamuziki ninamaanisha waimbaji na wapiga ala na siyo Bongo Fleva au Muziki wa Kizazi Kipya kwa sababu hata kwenye Bongo Fleva na Mziki wa Kizazi Kipya wapo wanafunzi wanaorap na kutengeneza miziki kwenye kompyuta na synthesizer.

Adbox