Jukwaa la wapenzi wa mambo ya muziki wa Tanzania-

Breaking

Wednesday, April 28, 2010

DJ wa kwanza

Katika kuzungumza na watu kupata mambo kwa ajili ya blog hii, nimepata hili ambalo naomba maoni. Kijana wa zamani mmoja kaniambia DJ wa kwanza anaemkumbuka alikuwa akikaa maeneo ya Keko Cocacola, alikuwa Mkongo fulani ambae jina kamsahau. Je, kuna mwenye kumbukumbu kuhusu hilo?

7 comments:

Anonymous said...

kunajamaa mmoja wakati mimi nakuwa niliwa hi kwende kwenye disiko, hapo keko,katika ukumbi ulio kuwa ukijulikana kama "Lusaka by night" kamasija kosea.na DJ ambaye alitamba sana hapo aliitwa DJ "Fanta".sasa sijuwi kama alikuwa ndo dj wa kwanza,maana wakatiule miaka ya 77 mpaka 80 kakazangu walikuwa wananitorosha usiku tuna kwenda disiko lusaka.watu walikuwa wanasema yule dj asili yake kongo(zaire).
mdau uk

Anonymous said...

Balozi, naomba nitoke nje ya mada kidogo. Hapa nina albamu ya Vijana jazz ile ya 'VIP' na kuna mtu anataja majina ya wanamuziki wote wa vijana katika intro, yule mtu ni nani maana naona ana sauti kama ya eddy sheggy na eddy sheggy alikuwa hayupo Vijana wakati ule. Tafadhali nitajie ni nani? katika hii albam dogodogo alipiga solo katika wimbo upi, maana najaribu kutofautoisha ile mirindimo ya solo naona yote ni sawa tu.

John Mwakitime said...

Ni sauti ya John Kitime

Anonymous said...

ahsante balozi kama ni sauti yako kweli wewe ni mkali. balozi una sauti nzuri, the great, the fantastic vijana sagha rhumba....yeeee! wimbo wako wa mwisho vijana jazz ulikuwa ni upi, na uliiimba wimbo upi pale vijana?

Anonymous said...

eti balozi, zahoro bangwe wa msondo ni mpiga solo ama rhythm?

Anonymous said...

Anpiga solo na anapiga rhythm

Anonymous said...

Dj wa kwanza kwa kumbukumbu zangu alikuwa ni MARK TWIST. ali perform kwanza Kilimanjaro Hotel na baadye akawa DJ wa kwanza Sea View hotel. wengine mta kumbuka kwamba alivyoondoka Mark Twist sea view aliyemrithi pale alikuwa ni DJ Addy Sally ambaye kabla alikuwa drummer boy wa the Tonics Kabla kuwa DJ. later on several others Joined the proffession.

Adbox