Jukwaa la wapenzi wa mambo ya muziki wa Tanzania-

Breaking

Thursday, April 15, 2010

Belesa Kakere

Salehe Kakere, maarufu kama Belesa Kakere, hapa akitangaza kuhamia Orchestra Bima Lee. Hebu soma maelezo katika habari yake unapata picha kamili ya mwanamuziki huyu na kazi zake na historia yake kwa ufupi

4 comments:

Danstan said...

Sauti ya Belesa Kakere katika nyimbo alizoimba ilikuwa na utamu wa aina yake. Tunamkubali na kumkumbuka.

Bwana Kitime naomba niulize, Kakere yupo wapi? ameacha kabisa muziki? na Je, mwanamuziki wa kujitegemea Juma Kakere ni ndugu yake?

Asante sana

Anonymous said...

...kakere alikuwa na albamu ya solo akimshirikisha karama regesu wa msondo na khadija mnoga kama sikosei. ile bendi ilikuwa inaitwa Djakabe masters na ilibeba jina l awimbo wa Mama Mona. Ilikuwa ni albam kali kweli, na kama bado anapiga muziki tafadhali bw. kakere endeleza libeneke la ile albam, nimeipenda mno na bado ninayo mpaka sasa.

Anonymous said...

Hivi Bw. Kitime kuna huyu jamaa wa Tanga ana nduguye (si marehemu sheggy) wanapiga muziki mzuri sana ila jina la bendi yao sijalikamata vizuri. Cha kushangaza huyu jamaa pia anaimba ama ana sauti nzuri kama ya sheggy. Unaweza kunitajia bendi za tanga pengine ninaweza kulimbuka jina la bendi yake. Nilimsikia kwenye club raha leo mwaka 1996 nilipokuwa TZ kwa likizo fupi. Yaani nataka kujuwa jina la bendi yake ili nijuwe kama bado anapiga muziki. Kwa kweli alinifurahisha mno kwa kazi yake.

Kingine bw. kitime...kwa nini wewe na wanamuziki wengine msiandamane kupinga ma dj wa tz maana wanatuangusha mno. fleva si muziki wetu ila wao wnataka tuubeze kwa misingi ipi siijuwi? kuna uwezekano wowote hapa wa maandamano kama haya kweli?

Perez said...

Kakere naukumbuka ule wimbo wake akiwa na Bima Lee

"...Ndoto yetu ya siku nyingii mwana mamaa, imekuwa kweliii...
Ahadi yetu tuloipanga sikuu nyingi, tumeitimiza...
Utakumbuka tulikuwa wote siku nyingi, tangu tuko masoomoni, Remmyy tulipendana....
tukapanga tufunge ndoa mimi nawe...

Adbox