YOUTUBE PLAYLIST

Sunday, April 25, 2010

Akina mama nao- Asia Darwesh


Asia Darwesh ni miongoni mwa wanamuziki wanaoheshimika sana katika jamii ya wanamuziki na wapenzi wa muziki waliowahi kusikia au kufurahia kazi zake. Katika picha hapo juu Asia ambae alikuwa mpiga Keyboards wa kutumainiwa anaoneka picha ya juu akiwa na King Kiki enzi za Double O, na chini akiwa Mk Sound. Asia aliwahi pia kupigia Bicco Stars ambapo yeye pamoja na Andy Swebe na Mafumu Bilali na wenzao (waliihama MK sound), waliweza kuipandisha sana chati bendi hii. Hatimae Asia aliweza kumiliki bendi yake na alipatwa na umauti akiwa na bendi yake ambayo ilifanya vizuri sana huko Uarabuni.

13 comments:

  1. Nakumbuka nyimbo zake za Bicco zaidi. Nakumbuka walivyokuwa wakitajwa pamoja na Any Swebe "Ambassador" na Mafumu.
    Lakini hata MK Group nako aliacha kumbukumbu nzuuri saana.
    Itabidi kufanya mpango wa kuunganisha makala hizi na Audios zake.
    Asante kwa mara ya Tena Uncle Kitime

    ReplyDelete
  2. Anonymous08:44

    BW.KITIME, HIYO PICHA YA JUU,HUYO MWIMBAJI WA KWANZA KUSHOTO SIYO KAPELEMBE KOKO? ALIYEIMBA WIMBO WA JEAN PIERRE...'WATOTO WA JEAN PIERRE MUNAWAONA VILE WANATESEKA YOYO...' NAMFANANISHA VILE! NA HUYO ALIYENYUMA YA KIKKI KAMA MOHAMED IDD VILE..HEBU NIKUMBUSHE BW. KITIME.

    ReplyDelete
  3. Ndiye mwenyewe

    ReplyDelete
  4. Anonymous09:57

    HIVYO HIYO 'X' MAANA YAKE KISHATANGULIA? OH! ALALE PEMA.

    ReplyDelete
  5. Anonymous12:35

    Anonymous 22:44

    Yule aliyenyuma ya King Kiki nadhani ni Zahoro Bangwe ambaye sasa yupo Msondo.

    -Muarubaini

    ReplyDelete
  6. Ni kweli Zahoro Bangwe kwa sasa yuko Msondo, kwenye Bass yuko Mohammed Iddi , Drums Matei Joseph, waimbaji ni King Kiki na Kapelembe koko, kinanda Asia Darwesh, hizi zilikuwa enzi za nyimbo kama Kitoto chaanza tambaa, Lamanda na kadhalika.

    ReplyDelete
  7. Ni kweli Zahoro Bangwe kwa sasa yuko Msondo, kwenye Bass yuko Mohammed Iddi , Drums Matei Joseph, waimbaji ni King Kiki na Kapelembe koko, kinanda Asia Darwesh, hizi zilikuwa enzi za nyimbo kama Kitoto chaanza tambaa, Lamanda na kadhalika.

    ReplyDelete
  8. Anonymous17:35

    Machozi yananilengalenga nikiwakumbuka wanamuziki mahiri wa kike waliotamba miaka ya 80 na 90 kama Asia Darwesh (RIP), Rahma Shally (RIP), Kida Waziri na Tabia Mwanjelwa. Kuondoka kwao katika anga la muziki kumetuacha wapweke

    ReplyDelete
  9. Anonymous17:38

    Hivi Anna Mwaole yuko wapi?

    ReplyDelete
  10. Balantanda20:57

    John,kwa kweli unaleta raha mkuu....Asia kwa kweli nilikuwa namkubali mnooo...Naukumbuka wimbo wa Muuza Chipsi wa Bicc Stars wanakindumbwendumbwe ulioimbwa zaidi na Kinguti System(last tyme nilisikia yuko uarabuni na bendi ya Jambo Survisors akiwa na mwanamama Mlasi Feruzi wakatoa kibao kitamu cha Maproso)

    Ombi maalum kwako John;je unaweza ukaanza angalau kutuwekea vipande vya nyimbo mlizotamba nazo miaka hiyo(hasa za vijana Jazz),kama yawezekana tusaidie tafadhali...Binafsi napenda kusikiliza nyimbo ambazo ni utunzi wako9kama sikosei) kama Malaine na Nyongise......Pia naomba ukiweza niwekee nyimbo au mashairi ya nyimbo za Mfitini na Mvuvi Kinda..

    Natanguliza shukrani

    Mdau Balantanda

    ReplyDelete
  11. Balantanda21:12

    Mkuu,mimi ninaomba utupe machache kuhusu malkia hawa wengine wa Muziki wa Tanzania wa miaka hiyo

    1.Tabia Mwanjelwa
    2.Kida Waziri
    3.Rahma Shally
    4.Nanah Njige
    5.Emma Mkelo 'Lady Champion'

    Balantanda

    ReplyDelete
  12. Anonymous09:55

    JM, je Stella Amri yuko wapi siku hizi? namkumbuka from late 60's na early 70's nilipokuwa nikisoma.

    ReplyDelete
  13. Balantanda,
    Nadhani Tabia Mwanjela yupo Ujerumani na bado yupo kwenye fani ya muziki hali kadhalika Kida Waziri ambaye yuko Arusha.
    Rahma Shalli, Nana Mjige 'Mzuri' na Emma Mkelo wote wameishatungulia mbele ya Haki.

    ReplyDelete

SAFARI ZANGU NA BENDI sehemu ya kwanza.

  TANCUT ALMASI ORCHESTRA  wakiwa Jamhuri Stadium Dodoma   Sikumbuki ni safari ngapi za kimuziki nilizowahi kuzifanya hapa nchini katika m...