Jukwaa la wapenzi wa mambo ya muziki wa Tanzania-

Breaking

Sunday, March 28, 2010


Unamkumbuka msanii huyu?

9 comments:

Anonymous said...

Marehemu Omar Naliene.

Anonymous said...

John
Naliene alikuwa ni Kifaa! mpaka leo sijaona mbadala wake. Mungu amrehemu

Anonymous said...

Naliene, filimbi hata kwa pua inapulizwa hapo...oyayoo!

Anonymous said...

Mkuu,

Marehemu Omari Naliene alikuwa msanii mwenye vipaji lukuki tena vikubwa. Marehemu Omari alikuwa mchezaji,mwimbaji, mpigaji wa ala za ngoma, marimba ya mbao na ya mkono na filimbi, na alikuwa mwigizaji mzuri sana.

Marehemu nilianza kumuona akiwa katika kikundi cha Tanganyika Packers na baadaye DDC-Kibisa miaka ya mwisho wa 70 na mwanzoni mwa miaka ya 80. Wakati huo Tanganyika Packers Cultural Troupe na baadaye DDC-Kibisa ilikuwa inaongozwa na Mzee mmoja wa Kimakonde kama sikosei alikuwa anaitwa Mzee Bwanyenye. Yule Mzee alikuwa mfupi, mnene, mwenye machale usoni, anabeba usinga na kuvaa magwanda ya kijani iliyokolea with very serious and authoritarian aura/personality vitu ambavyo mtu yoyote aliyepata kumuona ingemuia vigumu sana kumsahau.

Marehemu Omar alikuwa manju katika ngoma kadhaa zilizokuwa zinachezwa na vikundi vya Tanganyika Packers na DDC-Kibisa. Wajihi wa umbo lake, jamali ya sura yake, kiada na lafudhi ya sauti yake, na umahiri wa uchezaji wake ulimfanya kuwa manju kamili/a distinguished five stars General Field Marshal.

Umanju wake aliudhihiri haswa wakati akipiga filimbi na kucheza ngoma ya Sangula na katika kuongoza na kucheza ngoma za Sindimba, Lizombe na Kitoto. Kikundi cha Tanganyika Packers chini ya Mzee Bwanyenye walikuwa ni wakali vibaya mno kwenye upigaji, uchezaji na uimbaji wa ngoma ya Sindimba na Marehemu Omari ndiye aliyekuwa manju wa ngoma hii. Ni lazima mwili ukusisimke pale walipokuwa wanaanza kuicheza ngoma ya Sindimba ukiisikia sauti ya Marehemu Omari ikitoa yowe la "..Eeeee harambee eeeee!!!! eeee eeee!!!.." na waitikiaji kuitikia "...Harambee eee.." Hapo ni kabla ya vinganga na mitonya kuanza kuchanganya na wachezaji kuanza kuvina. Ungemuona wala usingeweza kudhani kwamba Marehemu Omari hakuwa Mmakonde kutoka Mtwara bali Mpogolo kutoka Kilombero.

ITAENDELEA

Anonymous said...

Mkuu,

INAENDELEA

Vikundi vya sanaa vya miaka ya sabini na themanini kama Kikundi cha Taifa, JKT, JWTZ, Tanganyika Packers, Breweries,DDC-Kibisa, Super Mwongozo, Muungano Cultural Troupe etc vilikuwa vinajuimusha ngoma za asili,kwaya, tamthiliya,sarakasi na vikundi vingine vilikuwa vinaongezea na muziki wa dansi na taarabu. Marehemu Omari wakati akiwa DDC-Kibisa alikuwa yumo kwenye ngoma na tamthiliya.

Ndugu zanguni, Marehemu Omari alikuwa mwigizaji mzuri sana tena mno. DDC-Kibisa walikuwa na igizo lao moja ambapo Marehemu Omari alikuwa anaigiza kama Muhindi. Yaani katika hilo igizo Marehemu alikuwa anamuigizia Muhindi kuanzia sauti mpaka tabia zake bila ya punje ya kukosea. Hii inaashiria kwamba Marehemu Omari si tu alikuwa mwingizaji bali alikuwa msomi mzuri wa watu na tabia na tamaduni zao.

Baadaye Marehemu Omari aliingia kwenye muziki wa dansi au tuiite jazz au crisscross kwenye bendi ya Watafiti, Benebene na baadaye TatuNane. Kama uliwahi kuona maonyesho ya TatuNane au kusikiliza CD za TatuNane na ile ya Umoja ya Watafiti utakiri na kuafiki kwamba Marehemu Omari alikuwa ni mwanamuziki mwenye kipaji cha hali ya juu mno.

Kuna nyimbo ya Sangula ya TatuNane ambapo Marehemu Omari alikuwa anaongoza uimbaji na baadaye alikuwa anapiga filimbi. Good God! If you listen to that piece you wouldn't argue with me that Late Omar was wicked wizard! Na ungemuona kwenye show wakati wa nyimbo ya Sangula ungeelewa vizuri zaidi. Marehemu Omari kwenye ile nyimbo ya sangula alikuwa anaanza kwa kuimba huku sauti yake ikikimbizana na muziki wenye very fast tempo and heavy beats huku sauti yake ya kipekee ikiafikiwa na very beautiful brass don't know if it was Sax or Trumpet, unconventional bass line, guitar and drums and back vocals,aaarghh yaani ilikuwa hatari tupu!

Utamu wa mambo unakuja katikati ya ile nyimbo Marehemu Omari anapochukuwa filimbi na kuanza kuipuliza. Kama vile filimbi moja haitoshi anachukua na filimbi ya pili anazipuliza zote mbili kwa wakati mmoja. Baadaye anaona kwa nini nipulize filimbi mbili kwa mdomo mmoja? Guess what!? Anazihamisha toka mdomoni kwenda puani, si utani anazichomeka filimbi kwenye tundu za pua na kuanza kuzipuliza kwa pua with same tone and clarity! At this moment what will the audience do? As a matter of course, the audience will be mesmerised and hypnotized! Whatsoever, with hands down or up, sitting or standing you conceed the fact without a shadow of protest that Omari Naliene is the best!

Umeona Omari? Ulitupa mengi mazuri sana ndiyo sababu kwamba leo haupo pamoja nasi kimwili lakini kiroho upo nasi kila siku. Pumzika kwa amani rafiki yetu. Tunakuombea kwa
Mwenyezi Mungu akurehemu Marehemu Omari kwa amani. Amen.

Anonymous said...

Mkuu,

PS/ Si kwamba Marehemu Omari alikuwa ni mpiga ala, mchezaji, mwimbaji na muigizaji la hasha alikuwa pia ni fundi wa kutengeza/kuwamba ngoma na kutengeza marimba ya vibao. Nilipata kufika nyumbani kwake kule Yombo nikamkuta alikuwa na order ya kutengeza/kuwamba ngoma na kutengeza marimba ya vibao.

Michuzi said...

wachache watatokea kama omari naliene

Dr Morice Mwanyika said...

I wish ningekuwepo enzi hizo nimwone laivu

Anonymous said...

Namkumbuka sana Omari Naliene. Hivi wale vijana wengine aliokuwa nao Tatunane wako wapi siku hizi. Wengi wao nilisikia waliishia kuoa wanawake wa Kizungu!

Adbox