Jukwaa la wapenzi wa mambo ya muziki wa Tanzania-

Breaking

Tuesday, March 16, 2010

The Tanzanites


Kabla ya kuwa na jina hili waliitwa the Barkeys, moja ya bendi za zamani sana Tanzania picha hii ya siku ya mwaka mpya 1991 itawapa watu kumbukumbu za kutosha. Bibie hapo mbele ni Juliet Seganga

10 comments:

Anonymous said...

Mzee Kitime umenikumbusha miaka ya 80's hiyo Band ya Barkeys ilikuwa inapiga Police Officers Mess wakati huo Waziri Ally anapiga kinanda sie tulikuwa tunaishi jirani na hapo wacha nakikumbuka kinanda chake nadhani ndio Band za mwanzo kuanza kupiga miziki ya kuiga

John F Kitime said...

Napata taabu kukuunga mkono maana Waziri Ally hajawahi kupigia Barkeys. Ana historia ya kupiga Taarabu na Lucky Star Tanga, pia alipiga muziki katika bendi iliyoanzishwa na marehemu mzee Nnauye, King'ita Ngoma Singida, akapigia Revolutions, JUWATA na Kilimanjaro Band ambapo yuko mpaka sasa. Ila ni kweli Barkeys walipafanya Police Mess pawe mahala pa makutano mazuri ya watu miaka ya themanini. Bendi za kupiga muziki wa kuiga zimeanza kitambo zaidi.

SIMON KITURURU said...

Hii ndio bendi iliyonisaidia kukumbatia vizuri wakati nacheza muziki enzi wako Simba Grill enzi za Kilimanjaro Hotel.:-)

John F Kitime said...

Siku hizi muziki wa kukumbatia umekuwa adimu kidogo au?

SIMON KITURURU said...

Siku hizi muziki wa wajanja sio wa kukumbatia na ukisikia asifiwaye ni mjanja basi staili yake kwenye dancing floor ni kama anafanya mchezo wa kumpa mimba mtu vile ki BONGO FLEVA au ki MUGONGOMUGONGO na chaupele mpenzi siku hizi hakuna.:-(

Lakini katika wote wa The Tanzanite nilimuona Mhina tu siku za hivi karibuni akiendeleza sijui wengine wako wapi.:-(

Anonymous said...

Kuna dada mwingine alikua anaimba na hii bendi, kuna uvumi alikua mtoto wa mchungaji jina lake silikumbuki ila walitupa raha sana enzi za ujana wetu pale Simba Grill kilimanjaro

Anonymous said...

Hv yule dada aliekuwa anaimba Tanazanite nadhani alikuwa akiitwa Betty yuko wapi? Namkumbuka sana wakati tunakuwa walikuwa wanapiga Kilimanjaro Hotel Pool side maana sie tulikuwa haturuhusiwi usiku tukawa tunajiiba siku za jpili nakumbuka walikuwa wanaimba miziki ya "KASSAVU" Halafu Mkubwa umenikumbusha Revolution ni kweli waziri Ally hauimba Barkeys nilijichanganya aliimba Revolution. Hv wale Cheza imba (Chezimba) walipotelea wapi

John F Kitime said...

Ni kweli yule binti mweupe mwenye macho mazuri Betty aliimbia Tanzaniate, nilipata taarifa alikwenda nje ya nchi, tutawauliza Tanzanites nadhani wanajua. Chezimba ilikufa zamani, wapenzi wake wa enzi za Twiga Hotel na Dodoma Hotel lazima wana mengi ya kusema kuhusu kundi hili. Nilikwisha muomba mmoja wa wanamuziki wake atupatie taarifa ya walikotoka nasubiri uhondo toka kwa Charles Mhuto. Nadhani unakumbuka nyimbo zao kama......... bisho Ntongo, macho nyanya mshumaa useme utakacho nitakupa....au.... fimbo ya babu fimbo spesheli....

Patrick Tsere said...

Yes Barkeys and now Tanzanites. Japokuwa baadhi yao hawako na kundi hili kama 'shemeji' yangu Kizibo aliekuwa akipiga tumba na akina Peti nafikiri na George Kapinga na mmoja jina limenitoka wengine bado wanaendelea kama vile Abraham Kapinga, Amato Kapinga, John Mhina na Yona Mgaza. Hawa vijana siyo siri wanayo nidhamu ya hali ya juu ambayo naweza nikaifananisha na ya Njenje. Hawa vijana mimi binafsi ninawafahamu kwa sababu walikuwa wadogo zangu shuleni miaka ya 1963 hadi 1965. Wakati huo tukisoma shule inayoitwa Salvatorian Convent School hivi sasa ndiyo makao makuu ya Baraza la Maaskofu kule Kurasini (TEC). Wakiwa Arusha wakipiga hoteli ya Mount Meru miaka ya 1980s hadi 1990s nilikuwa nao karibu.

Siyo siri na John naamini utakubaliana na mimi. Siri mojawapo ya bendi kudumu ni nidhamu ndani ya kundi. Na Tanzanite kwa hilo wameweza.

Anonymous said...

Betty alikuwa Japan kwa muda mrefu. Sasahivi yuko USA

Adbox