Jukwaa la wapenzi wa mambo ya muziki wa Tanzania-

Breaking

Tuesday, March 2, 2010

Swali la Leo

Bendi gani iliimba wimbo- Mali ya mwenzio sio mali yako? Na dongo lilikuwa likielekezwa kwa nani?

2 comments:

Patrick Tsere said...

Waliimba akina Daudi Makwaia na Western Jazz 1966 kwa kuiiga wimbo wa Dr Nico Kasanda. Madongo nafikiri yalikuwa yakielekezwa Kilwa Jazz. Kwa sababu Kilwa walikuwa wanawapiku Western na Dar Jazz kuiga hasa nyimbo za Franco. Wakati huo Duncan Njilima alikuwa ameletewa Rashid Hanzuruni kutoka Tabora Jazz kama soloist mshirika. Hanzuruni alikuwa mahiri sana kuiga solo ya Kasanda.

John F Kitime said...

Mheshimiwa rudisha kumbukumbu, hili dongo lilikuwa la Kilwa wakiimbwa na Dar Jazz kutokana na wao kuringia ukumbi wao siku hizi maarufu Kwa Madobi pale Jangwani karibu na Klabu ya Yanga. Kilwa walikuwa wampepanga tu ule ukumbi.Ila maelezo yako mengine ni matamu sana. Maana baada ya muda si mrefu nadhani Duncan Njilima na wenzie walianzisha bendi ya African Quilado.
Na upigaji gitaa wa Hanzuruni ukiwa na uimbaji wa Daudi Makwaiya unasikika mpaka leo kwenye ule wimbo walioiga kwa African Fiesta..Napenda nipate lau nafasi

Adbox