Jukwaa la wapenzi wa mambo ya muziki wa Tanzania-

Breaking

Thursday, March 11, 2010

Nawaachia wananchi waseme 2
5 comments:

Patrick Tsere said...

John unakumbuka tulipokuwa pale Iringa nilikuwa navaa viatu hivi. I remember mwaka 1976 nilivinunua duka la Bora vikizuwa shs 250 jozi moja. Kwa mshahara wangu wa shs 500 kwa mwezi wakati huo sikujali kufa njaa.Vilikuwa ghali kweli. Ukiweka juu yake suruali ya pecos (bell bottom) na nywele za Afro ah bwana mbona unaonekana kijana wa kisasa haswa. Unakumbuka? Hahaha. I wish we had video cameras those days.

Anonymous said...

Mkuu,

Zilikuwa ni enzi za ubitozi, 1974 to 1976. Miziki ya kina Kirk Douglas, Osibisa, Ojays, Sunburst, Barkeys, Trippers, Afrosa, Jimmy Cliff pia alituswafi nyoyo.

Local bands zilizovuma wakati huo NUTA Jazz Band ilikuwa numero uno katika viwanja vya watoto wa nyumbani (Mpenzi Zarina mpaka mtondogoo itanikuna). Kuruka ukuta ilipigwa na nani?

Kipindi hicho ndiyo ulikuwa ujio wa Boma Liwanza na Marquis Du Zaire. Pia Sosoliso ndiyo walisikika na Tres Madjes.

Ubitozi, Laizon, Pecos, Slimfit, Bumping, Kavasha, klimplin, dengliz, maxi, mini, Bora Shoe, Bata ndiyo ilikuwa social image.

Richard Matiko aliishiwa wapi?

Anonymous said...

John, nina HIS MASTER'S VOICE kinanda kama kuna mtu anataka kama mapambo.

John F Kitime said...

Bei? mi naitaka

Mr.Nullo said...

Daah! Zamani wazee wetu mlikula sana bata! Nowdays mavazi mazuri yapo lakini kwa upande wa dada zetu mengi ni nusu uchi

Adbox