Jukwaa la wapenzi wa mambo ya muziki wa Tanzania-

Breaking

Thursday, March 4, 2010

Jiving


Katika aina ya muziki ambao ulisababisha bendi kuanza katika mashule, ilikuwa ni aina ya muziki na kucheza ulioitwa 'jiving'. Shule nyingi zilikuwa na vikundi hivi, sekondari za kike na kiume zilishindana katika jiving. Muziki huu ulikuwa umetoka haswa Afrika ya Kusini. Siasa zikaingilia kati katika miaka ya mwishoni ya sabini na kuuwa jiving katika mashule mengi. Jiving ilikuwa inaambatana mara nyingine na filimbi kama alivyokuwa anapiga Spokes Mashiyane. Mbaraka Mwinyshehe ni matokeo ya muziki huu alikuwa bingwa wa kupiga filimbi. Pichani ni kikundi cha jiving cha Mkwawa High School The Skylarks Jiving Group, akiwemo mwandishi maarufu Danford Mpumilwa (watano toka kushoto) ambaye pamoja na kuwa mwimbaji wa Bendi ya shule hiyo Mkwawa Orchestra, aliendelea mpaka kufikia kuwa na bendi yake mwenyewe pale Arusha.

7 comments:

SIMON KITURURU said...

Hii staili bado mie naihusudu sana.

Asante kwa shule hii kwa kuwa kuna mambo sikuwa naoanisha JIVING nayo ikiwa moja wapo ni Marehemu MBARAKA ambaye baada ya WEWE kutamka ndio nastukia influence ya hii kitu katika kazi zake.

Anonymous said...

Mkuu,

Hawa kweli walikuwa wanajive na jina wakalichukua la Skylarks!

Spokes Mashiyane namzimia vibaya sana kwenye Pennywhistle kwela. Halafu kuna mwendawazimu Big Voice Jack Lerole kwenye pennywhistle jive na mzee mzima West Nkosi Sax kwela. Zis pipo when it kamzi tu Kwela na jive ni anbitebo!

Sasa hebu angalia maajabu ya kaburu pamoja na unyama wake wa apartheid hakuharibu kabisa musical identity ya Waafrika ya kusini. Lakini Tanzania huru kwa raha zetu tunaua pachanga na rumba letu huku tunachekelea.

Nadhani Tanzania ndiyo nchi ambayo inaweza kuingizwa kwenye Guiness Book of Records kwa Waziri wa Elimu na Utamaduni kupata kuwa major importer na mdau wa muziki wa kigeni " The Acudo Impact"!

Patrick Tsere said...

Mbona umemtaja Danford peke yake na umemsahau Askofu Kakobe na muziki wao 'Ligija Sound Sukisa'.
John nilipokuwa nasoma Mazengo Secondary mwaka 1970 na 1971 tulikuwa na kundi letu likiitwa The Merrymakers. Kiongozi wetu alikuwa Simon Jengo ambaye hadi leo ni mwimbaji mahiri haswa akiongoza Kwaya ya Azania Front KKKT.

Ama kweli tumetoka mbali. Yote ni heri hakuna cha kulalamikia.

John F Kitime said...

Mheshimiwa asante kwa kuingiza utamu, pamoja na kuwa nilicheza Ligija nilisahau hii staili, na kwa kweli sijamsahau Askof Kakobe maana nimemtaja katika listi ya wanamuziki wa Mkwawa, unajua bugi pale Community Center Iringa lilikuwa halinogi bila Mhashamu kuweko.

Anonymous said...

Mkuu,

Hii hint ya Mhashamu kuwa alikuwa mwanamuziki inaweza kuwa sababu ya baadhi ya vijana wanamuziki mashuhuri wa miaka ya 60 na 70 kuwa wafuasi wa kanisa lake. Kuna mwanamuziki mmoja kati wale waliosoma Minaki ambaye alitajwa humu katika makala zilizopita ni muumini wa kanisa la Mhashamu. Pia kuna mwingine alikuwa maarufu kwa kupiga drums kwenye bendi za maghorofani pia ni muumini wa kanisa la Mhashamu.

John F Kitime said...

Hiyo ni kama kunambia watu wanaingia CCM kwa kuwa walisoma Kibaha Education Center alikosoma Mkuu zaidi

Anonymous said...

Mkuu,

Inawezekana pia ni kama kusema NEC na Cabinet wapo baadhi ya mates waliosoma UDSM wakati mmoja na mkuu zaidi!

Adbox