YOUTUBE PLAYLIST

Wednesday, March 24, 2010

Dr Ufuta enzi hizo na sasa



John,

Mimi ni mmjoja kati wa fans wa blog yako. Nilikuwa Morogoro mjini na kwa bahati nzuri wakati napata chai ya jioni pale B1 restaurant akapita mwanamuziki mkongwe DOKTA UFUTA Nilifanya nae maongezi mafupi maana alikuwa na haraka kidogo akiwahi kazini, kwa sasa ni mlinzi wa usiku" babu mlinzi" katika moja ya makampuni ya ulinzi pale Morogoro. Tuliongea sana na nikakumbuka last article uliyotoa ya Cuban Marimba na jinsi alivyokuwa akionenaka kijana very hundsome. sasa kupitia taswira hizi chache hivi ndivyo alivyo.

Louie
(Dr Ufuta ndiye mwenye miwani katika hili ganda la santuri enzi hizo)

10 comments:

  1. Kaka John, kwanza kabisa nakupungeza kwa kazi nzuri unayoifanya. nimefurahishwa sana na uwepo wa blog hii inatakayotupatia mambo mbalimbali kuhusu muziki wa Kibongo. Kitu kizuri zaidi katika blog yako siyo kwamba inatupa habari, ni kwamba inatoa pia elimu na kutupa tafakari juu ya masuala mbalimbali katika anga ya Muziki. zaidi ya hapo kwa wanamuziki wa sasa inawapata kwelekeo juu ya future zao. Mimi niko pamoja na wewe na nitakuwa nikipa Updates kila nitakapokuwa nikikutana na suala la kimuziki huko ninakozunguukia.

    --
    Hassan Bumbuli
    Senior Editor
    Si Mchezo! Magazine
    P.O.Box 2065
    Patel Building 5th Flour Opp Kazi House
    +255 713 436153
    Dar es Salaam

    ReplyDelete
  2. Haya maelezo yana nguvu za ajabu.
    Tumkumbuke huyu na wengine wengi WALIOITUMIKIA NCHI NA SASA WAMETELEKEZWA.
    Mkumbuke Mzee Nyunyusa na ngoma zake, na wengine waliosaidia kusambaza na kutekeleza sera na mipango ya serikali kama GEZAULOLE ama hata walioitumikia jamii kwa kufunza mengi kupitia tunzo zao. Lakini sasa hivi wako wapi ama heshima, stahiki na haki zao ziko wapi?
    Niliwahi kuandika kuhusu wasanii katika toleo nililolipa kichwa cha habari WASANII KAMA CHOMBO CHA STAREHE CHA SERIKALI (http://changamotoyetu.blogspot.com/2008/10/wasanii-kama-chombo-cha-starehe-cha.html) na baadae nilikuja kujiuliza na kushiriki kuuliza kuwa NI LINI TUTAKAPOWAENZI WATU HAWA? (http://changamotoyetu.blogspot.com/2009/08/ni-lini-tutawaenzi-watu-hawa.html).

    Naamini kuna funzo la msingi katika picha na bandiko hili.
    TUJIFUNZE

    ReplyDelete
  3. kWA WALE AMBAO TUMESHATUMIKA HIVYO MARA MIA KIDOGO TUNAIJUA FRUSTRATION YAKE. Kwanza aslimia kubwa ya viongozi hufanya diplomasia ya kuonyesha meno tu lakini hawana interest yoyote ya wasanii na usanii wao, hivyo ni protokali tu inayowafanya wavumilie. Na ingekuwa wanajali wangekuwa japo wanajiuliza hawa jamaa wako hapa wamelipwa? Bahati mbaya kwa hili hakuna tofauti kati chama tawala na vile vinavyotaka kutawala

    ReplyDelete
  4. Ni changamoto katika maisha ya wanamuziki Tanzania juu ya nini kifanyike na pia kuwathamini na kuwaenzi wale wakongwe wa Muziki Tanzania naamini wapo wengi tu sasa hivi wamekwishasahaulika. Kitu kilichofanya hawa wakongwe wetu kuwa maskini mpaka leo hii naweza kusema ni utii waliokuwa nao juu ya sera za nchi yetu miaka hiyo maskini kumbe hawakujua kwamba haki zao zinaliwa.

    Naweza kusema hawa walikuwa wanamuziki wa ukweli kutokana na tungo zao, ujumbe wao na namna yao ya kuonekana jukwaani na nje ya jukwaa iliendana na mahadhi ya utamaduni wa kwetu Tanzania.

    ReplyDelete
  5. Anonymous10:14

    Tunzo za mwaka huu ambazo zinafanyika kwa mwaka wa 11 sasa zimepangwa kutolewa kwenye Ukumbi wa Diamond jijini Dar es Salaam, Mei 14.

    Wanaowania tuzo ya Mwimbaji bora wa kike.



    Lady Jaydee
    Mwasiti Almasi
    Maunda Zorro
    Vumilia Mwaipopo
    Khadija Yusuph




    wanaowania tunzo ya Mwimbaji bora wa kiume.
    Marlow
    Banana Zorro
    Mzee Yusuph
    Alikiba
    Christian Bella


    Wanaowania Albamu Bora ya Taarab



    Jahazi Modern Taarab (Daktari wa Mapenzi),
    5 Stars Modern Taarab (Riziki Mwanzo wa Chuki),
    Coast Modern Taarab (Kukupenda Isiwe Tabu),
    New Zanzibar Star (Powa Mpenzi)
    East African Melody (Kila Mtu Kivyakevyake).



    Tunzo ya Wimbo Bora wa Taarab inawaniwa na


    Daktari wa Mapenzi’ na ‘Roho Mbaya Haijengi’ (zote Jahazi Modern Taarab), ‘Wapambe Msitujadili’, ‘Riziki Mwanzo wa Chuki’ (zote 5 Stars Modern Taarab) na ‘Kukupenda Isiwe Tabu’ (Coast Modern Taarab).

    Tunzo ya Wimbo Bora wa Mwaka inawaniwa na


    Marlow ‘Pii Pii-Missing my Baby
    Diamond (Kamwambie)
    Banana Zorro (Zoba)
    Hussein Machozi (Kwa Ajili Yako).



    Tunzo ya Wimbo Bora wa Kiswahili kwa upande wa bendi ni


    Machozi Band (Nilizama),
    African Stars Band-Twanga Pepeta (Mwana Dar es Salaam),
    Top Band (Asha),
    FM Academia (Vuta Nikuvute)
    Extra Bongo (Mjini Mipango).



    Tunzo ya Albamu Bora ya Bendi inawaniwa na


    African Stars Band ‘Twanga Pepeta’ (Mwana Dar es Salaam),
    Kalunde Band (Hilda)
    Msondo Ngoma Music Band (Huna Shukrani).

    Kwa upande wa Tunzo ya Wimbo Bora wa R&B, wanaoiwania ni


    Belle 9 ‘Masogange’,
    Diamond (Kamwambie),
    AT na Stara Thomas (Nipigie),
    Maunda Zorro (Mapenzi ya Wawili)
    Steve (Sogea Karibu).



    Tunzo ya Wimbo Bora wa Asili ya Kitanzania unawaniwa na


    Mrisho Mpoto (Nikipata Nauli),
    Machozi Band (Mtarimbo),
    Offside Trick (Samaki),
    Wahapahapa Band (Chei Chei)
    Omari Omari (Kupata Majaaliwa).



    Wanaowania Tunzo ya Wimbo Bora wa Hip Hop ni


    Joh Makini (Stimu Zimelipiwa),
    Quick Racka (Bullet),
    Chid Benzi (Pom Pom Pisha),
    Mangwea (CNN) na Fid Q (Iam a Professional).




    Tunzo ya Wimbo Bora wa Reggae inawaniwa na


    Hemedi (Alcohol),
    Dabo Ft. Mwasiti (Don’t Let Go),
    Man Snepa (Barua)
    Matonya Ft. Christian Bella (Umoja ni Nguvu).




    Kwa upande wa Tunzo ya Wimbo Bora wa Ragga, wanaoiwania ni



    Dully Sykes (Shikide),
    Bwana Misosi (Mungu yuko Bize),
    Drezzy Chief (Wasanii)
    Benjamin wa Mambo Jambo (Fly)



    Tunzo ya Rappa Bora wa Mwaka inawaniwa na



    Chokoraa,
    Ferguson,
    Kitokololo,
    Totoo ze Bingwa
    Diouf.



    Tunzo ya Msanii Bora wa Hip Hop ni
    Joh Makini
    Fid Q
    Chid Benz
    Mangwea
    Profesa Jay.



    Tunzo ya Wimbo Bora wa Afrika Mashariki inawaniwa na


    Blue 3 Ft. Radio and Weasal -Good Life ‘Where you are’,
    Kidumu Ft. Juliana (Haturudi Nyuma),
    Cindy (Na Wewe),
    Radio and Weasal - Good Life (Bread and Butter)
    Kidumu akitupa karata na wimbo ‘Umenikosea’.




    Tunzo ya Mtunzi Bora wa Nyimbo ni



    Mzee Yusuph
    Mrisho Mpoto
    Lady Laydee
    Banana Zorro
    Mzee Abuu, Fid Q


    Tunzo ya Watayarishaji Bora wa Muziki

    Lamar
    Marco Chali
    Hermy B
    Allan Mapig0
    Man Water


    Video Bora ya Muziki wa Mwaka inawaniwa na


    Lady Jaydee (Natamani kuwa Malaika)
    Diamond (Kamwambie),
    AY (Leo)
    Banana Zorro (Zoba)
    C Pwaa (Problem).



    Tunzo ya Wimbo Bora wa Afro Pop inawaniwa na


    Banana Zorro (Zoba)
    Alikiba (Msiniseme)
    Marlow (Pii Pii Missing My Baby)
    Mataluma (Mama Mubaya)
    Chegge (Karibuni Kiumeni)




    Tunzo ya Msanii Bora Anayechipukia


    Belle 9
    Diamond
    Barnaba
    Quick Racka
    Amini


    Tunzo ya Wimbo Bora wa Kushirikiana inawaniwa na


    AT - Stara Thomas (Nipigie)
    Mangwea Ft. Fid Q (CNN)
    Barnabas Ft. Pipi (Njia Panda)
    Mwana FA Ft. Profesa Jay na Sugu (Nazeeka Sasa)
    Hussein Machozi Ft. Joh Makini (Utaipenda).

    ReplyDelete
  6. Bwana Kitime,

    Niko katika suala hili hili la wanamuziki wa zamani, kuishia katika maisha duni au kufanikiwa....niulize, je, unamfahamu mwanamuziki wa Kongo, Boni Efokoko aliyewahi kuwa na bendi mbali mbali hapo Tz? Aliwahi kupiga bendi gani na alikuwa akishiriki katika ala ipi?

    Danstan

    ReplyDelete
  7. Anonymous07:53

    Jamani niliomba msaada wa hiyo player hapo pembeni, lakini comment yangu haikutolewa imekuwaje? Maana nikitaka ku play inaruka wimbo mmoja kwenda mwingine bila kuimba chochote! Bw. Kitime nisaidie!

    ReplyDelete
  8. Mkuu ngoja nijaribu kubadilisha settings tuone kama itasaidia, samahani kwa kukosa raha

    ReplyDelete
  9. Anonymous19:45

    Mzee Kitime tunashukuru sana kwa kazi yako ya kutuhabarisha na kutukumbusha mambo ya muziki hasa ule wa zamani.
    Nina swali moja kuhusu majina ya utani ya wasani (vijana wa siku hizi hupenda kutumia neno aka). Kwa mfano Dr Ufuta na Dr Remmy. Nini hasa kiini cha wanamuziki hawa kuitwa (kujiita) Dr. Inawezekana ni kwa sababu ya umahiri wao ktk fani au chombo walichokuwa wakipiga katika bendi zao?
    Zamani kulikuwa na matangazo ktk magazeti yakionyesha bendi gani inapiga wapi. Ktk matangazo haya, nakumbuka vizuri kuona Dr Remmy Ongala akiwa amejipamba kwa vitu vya asili kama vile hirizi, vibuyu (sina uhakika kama ni neno la kiswahili au kingoni). Je inawezekana hii ilichangia kwa Remmy kupewa U-Dr, hasa akifananishwa na waganga wa jadi?
    Kuna bendi moja aliibuka kipindi fulani, iliikuwa inaitwa The Mk Beats (wana Tukunyema mpaka chini) ikiongozwa mtu mzima Shem Kalenga. Nafikiri huyu mzee amesahaulika kidogo, kama unaweza kutupa historia yake fupi tutafurahi.
    Nakumbuka wimbo wake mmoja ulikuwa unaimbwa .. ndela ombwe x2.. (sina uhakika kama nimepatia. Ulikuwa ukianza kwa horn ya treni na mwimbaji akisema Kigoma, Tabora, Jijini DSM.
    Shukrani mkuu

    ReplyDelete

SAFARI ZANGU NA BENDI sehemu ya kwanza.

  TANCUT ALMASI ORCHESTRA  wakiwa Jamhuri Stadium Dodoma   Sikumbuki ni safari ngapi za kimuziki nilizowahi kuzifanya hapa nchini katika m...